settings icon
share icon
Swali

Tarumbeta saba za Ufunuo ni gani?

Jibu


Tarumbeta saba zimeelezewa katika Ufunuo 8: 6–9:19 na 11:15–19. Tarumbeta saba zimo katika hukumu ya mihuri saba, hivi kwamba muhuri wa saba huita malaika wanaopiga tarumbeta (Ufunuo 8:1-5). Hukumu zilizotangazwa na tarumbeta saba zitafanyika wakati wa dhiki katika nyakati za mwisho.

Tarumbeta ya kwanza. Wakati malaika wa kwanza anapiga tarumbeta, duniani kutakuwa na "mvua ya mawe na moto uliochanganyika na damu" (Ufunuo 8:7). Theluthi moja ya miti ya dunia itachomeka katika pigo hili, na nyasi yote kuchomeka. Hukumu hii ina uhusiano wa karibu na lile pigo la saba kule Misri (angalia Kutoka 9:23-24).

Tarumbeta ya pili. Mbinguni malaika wa pili anapiga tarumbeta. Matokeo ni kwamba "kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto kikatupwa baharini" (Ufunuo 8:8). Theluthi moja ya bahari ikawa damu, theluthi moja ya meli ikazama, na theluthi moja viumbe vya bahari vikafa (Ufunuo 8:9). Hukumu hii na sawia na lile pigo la kwanza kwa Misri (ona Kutoka 7:20-21).

Tarumbeta ya tatu. Hukumu ya tarumbeta ya tatu ni kama ile ya tarumbeta ya pili, tofauti tu ni maji safi ya ulimwengu, masiwa, mito badala ya bahari. Hasa, "na nyota kubwa iliyokuwa ikiwaka kama taa" ikaanguka kutoka mbinguni na kutia sumu theluthi moja vianzo vya maji (Ufunuo 8:10). Nyota hii imepewa jina Uchungu, na watu wengi wanakufa (Ufunuo 8:11). Katika nyanja ya mimea, machungu ni mmea unaofanana na kijiti unaojulikana kwa uchungu wake mkubwa na sumu yake.

Tarumbeta ya nne. Tarumbeta ya nne kati ya zile saba inaleta mabadiliko mbinguni. "Kisha malaika wa nne akaipiga tarumbeta yake, na theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota zikapigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga ikawa giza. Theluthi ya mchana ikawa haina mwanga na pia theluthi ya usiku" (Ufunuo 8:12)

Kufuatia hukumu ya nne ya tarumbeta, Yohana anabainisha onyo maalum linalotokana na tai anayeruka angani. Tai huyu analia kwa sauti kubwa, akisema, "Ole! Ole! Ole wa watu waishio duniani, kwa sababu ya tarumbeta ambazo malaika hao wengine watatu wanakaribia kuzipiga!" (Ufunuo 8:13). Kwa sababu hii, tarumbeta ya tano, sita na saba zinarejelewa kwetu kama "ole tatu."

Tarumbeta ya tano. Tarumbeta ya tano (ole wa kwanza) unatokea kwa pigo la kutisha la "nzige za kipepo" ambazo zinafamia na kutesa wenye hawajaokoka kwa miezi mitano (Ufunuo 9:1-11). Pigo linaanza kwa "nyota" kuanguka toka mbinguni. Nyota hii kuna uwezekano ni maliaka aliyeasi na amepewa "ilipewa ufunguo wa lile Shimo" (Ufunuo 9:1). Analifungua lile Shimo, na kuachilia kundi la "nzige" kwa "nguvu kama zile za nge wa duniani" (Ufunuo 9:3). Nzige hao hawaguzi mimea ya dunia; badala yake, wanaenda moja kwa moja kwa wale "watu ambao hawana muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao" (Ufunuo 9:4). Kwa miezi tano, nzige hawa wanawatesa watu, ambao uchungu wao ni mkubwa mno kiwango kwamba watatamani heri wafe, "lakini kifo kitawakimbia" (Ufunuo 9:6). Nzige hawarusiwi kuua mtu yeyote, bali kuwatesa.

"Nzige" hawa kishetani wana "mfalme," ambaye ni malaika wa lile Shimo (Ufunuo 9:11). Katika Kiebrania jina lake ni Abaddon, na katika Kiyunani jina lake ni Apollyon, linalomaanisha "Mwangamizi." Nzige zenyewe zinaelezewa kwa maneno yasiyo ya kawaida: zinaonekana kama "farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita" (Ufunuo 9: 7). Wanavaa kitu kama "taji za dhahabu," na nyuso zao ni za kibinadamu (Ufunuo 9: 7). Wana nywele "kama nywele za wanawake" na meno "meno yao yalikuwa kama ya simba" (Ufunuo 9: 8). Wana dari kama za chuma, na mabawa yao yanasikika kama "ngurumo za farasi wengi na magari mengi yakikimbilia vitani" (Ufunuo 9: 9). Kama nge, wana miiba katika mikia yao (Ufunuo 9:10). Maelezo haya yamesababisha tafsiri nyingi tofauti: je! Haya ni maono ya helikopta, ya wapiganaji wasomi, ya jeshi lenye nguvu za kishetani, au la viumbe halisi kutoka shimo la kuzimu? Hatutajua kwa uhakika hadi itakapotokea.

Tarumbeta ya sita. Tarumbeta ya sita (na ole wa pili) inahusisha kushambuliwa kwa kundi lingine la mapepo (Ufunuo 9: 12-21). Pindi tu baada ya tarumbeta ya sita kupigwa, sauti kutoka kwa madhabahu ya Mungu inaamuru kuachiliwa kwa "Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati" (Ufunuo 9:14). Malaika hawa wanne walikuwa wamewekwa kifungoni kwa sababu ya kusudi hili: kufanya uharibifu wakati wa dhiki (Ufunuo 9:15). Malaika hawa waovu wanne huongoza wapanda farasi wasio wa kawaida wa maelfu kwa maelfu kuua theluthi moja ya wanadamu (Ufunuo 9:16). Wapanda farasi wamevaa vifuani "dirii vifuani zenye rangi nyekundu sana kama ya moto na yakuti samawi na kiberiti" (Ufunuo 9:17). Farasi wao wana "vichwa vya simba, na moto, moshi na kiberiti vilitoka vinywani mwao," na "mikia yao ilikuwa kama nyoka" (Ufunuo 9: 18-19). Wanaua kwa vinywa vyao na kwa mikia yao.

Licha ya ukali na hofu ya mapigo haya, manusura duniani bado wanakataa kutubu. Wanaendelea katika ibada zao za sanamu, mauaji yao, uchawi wao, uasherati wao, na wizi wao (Ufunuo 9: 20-21).

Kunachofuata tarumbeta hukumu ya tarumbeta ya sita ni kimya. Yohana anaona malaika akishuka kutoka mbinguni akiwa ameshika hati ndogo mkononi. Ahadi inapeanwa kwamba "malaika wa saba atakapokaribia kuipiga hiyo tarumbeta yake" (Ufunuo 10:7), na Yohana anaambiwa kwamba atabiri zaidi (Ufunuo 10:11). Inayofuata ni maelezo ya mashihidi wawili ambao watahubiri Yerusalem na kufanya miujiza kabla wauawe. Baadaye Mungu atawafufua na kuwapeleka mbinguni (Ufunuo 11:1-13).

Parapanda ya saba. Parapanda ya saba (na ole wa tatu) inapigwa, na papo hapo kuna sauti kubwa mbinguni ikisema, "Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atatawala milele na milele" (Ufunuo 11:15).

wazee ishirini na wa nne wanesema, "Wakati umewadia … na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia" (Ufunuo 11:18). Ni wazi Mungu anataka kukamilisha mambo yote mara moja. Katika mlio wa parapanda ya saba hekalu la Mungu linafunguka minguni na "Ndipo hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe" (Ufunuo 11:19).

Na huo ndio mwisho wa hukumu saba za parapanda. Yote yametayarishwa kwa malaika saba na mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu. Malaika hawa wamesimama ndani ya hekalu lililofunguliwa sasa, na wako tayari kusonga mbele na kuleta hukumu za mwisho duniani (Ufunuo 15).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tarumbeta saba za Ufunuo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries