settings icon
share icon
Swali

Nimepewa talaka. Ninaweza kuoa kulingana na Bibilia?

Jibu


Kila mara tunayapokea maswali kama “Nimepewa talaka kwa sababu hii nah ii. Ninaweza kuoa tena? “Nimepewa talaka mara mbili- ya kwanza kwa sababu ya uzinzi wa mke/mke wangu, ya pili hatupatani. Ninamchumbia mwanamume ambaye amepewa talaka mara tatu- ya kwanza kupatana, pili uzinzi wake mwenye, na tatu uzinzi kwa mke wake. Tunaweza kuoana?” maswali kama haya ni magumu kuyajibu kwa sababu Bibilia haiendi kwa undani kuhusiana na hali mbalibmbali ya kuoa tena baada ya talaka.

Chenye tunaweza kujua kwa ukweli ni mpango wa Mungu ni wanandoa kudumu katika ndoa siku zao za uai (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:6). Ruhusa pekee ya kuoa tena baada ya talaka ni uzinzi (Mathayo 19:9), hii pia inajadiliwa sana katika Wakristo. Uwezekano mwingine ni ule wa kutorokwa-wakati mwanandoa mke/mume asiyeamini anapomwacha mwanandoa mwingine ambaye ni muumini (1 Wakorintho 7:12-15). Ukurasa huu ingawa haiuzungumzii swala la kuoa tena, bali wamelazimika kukaa katika ndoa. Itaonekana kuwa ngono, au kuadhirika kimawazo vibaya itakua sababu ya kutosha kwa talaka, na labda kuoa. Bibilia hasa haifunzi haya vilevile.

Tunajua mambo mawili kwa ukweli. Mungu anachukia talaka (Malaki 2:16), Mungu ni wa huruma na husamehe. Kila talaka hutokea kwa sababu ya dhambi, pengine kwa mmoja wa wanandoa ama wote. Je! Mungu husemehe talaka? Kamwe talaka sio ndogo kuliko dhambi zingine na inaweza samehewa. Msamaha wa dhambi zote uko tayari kupitia kwa imani katika Yesu kristo (Mathayo 26:28; Waefeso 1:7). Ikiwa Mungu anaisamehe dhambi ya talaka, je! Hiyo inamaanisha ya kwamba uko huru kuoa tena? Haitajiki kamwe. Mungu wakati mwingine huita watu wabaki vile walivyo (1Wakorintho 7:7-8). Kukaa peke yako isitazamiwe kwamba kama laana au adhabu, bali kama nafasi kumtumikia Mungu kwa moyo wako wote (1 Wakorintho 7:32-36). Neno la Mungu linatuambia, ingawa ni vyema kuoa tena kuliko kusumbuka na tamaa za mwili (1 Wakorintho 7:9). Hata hivyo hii wakati mwingine hutumika kwa ndoa baada ya talaka.

Kwa hivyo, unaweza kuoa/kuolewa tena? Tunaweza kujibu swali hilo. Hiyo ni juu yako kuamua na mwanandoa mwenzako, na wa muimu sana ni Mungu. Ushauri pekee tutakao kupa ni kuwa uombe kwa Mungu akupe hekima kuhusu anachokutaka ufanye (Yakobo 1:5). Omba kwa mawazo yaliyo ya kweli, na kwa ukweli kabisa muulize Mungu aweke haja zake katika moyo wako (Zaburi 37:4). Tafuta mapenzi ya Mungu (Methali 3:5-6) na ufuate uongozi wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nimepewa talaka. Ninaweza kuoa kulingana na Bibilia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries