settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini juu ya talaka na kuoa tena?

Jibu


Kwanza ni muhimu kukumbuka maneno ya biblia katika malaki 2:16a: “ nachukia talaka, asema Bwana Mungu wa Israeli,” kulengana na biblia,mpango wa Mungu juu ya ndoa ni iwe ushikamano wa siku zote za mwanadamu duniani. “ Hata si wawili tena bali mmoja. Kwa hivyo kile Mungu amekiunganisha mwanadamu asikitenganishe” (mathayo 19:6). Mungu antambua ya kwamba kwa kuwa ndoa ni ya wenye dhambi wawili, talaka haina budi kutokea. Katika agano la kale aliweka shaeria za kulinda haki za watalaka hasa wanawake (kumbukumbu la torati 24:1-4). Yesu akasema sheria hizi zilitolewa kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu lakini hayakuwa mapenzi ya Mungu (Mathayo 19:8).

Utofauti wa maoni juu ya talaka na kuoa tena unatokana na maneno ya Yesu katika Mathayo 5:32 na 19:9. “isipokuwa kwa habari za uasherati” ndicho kipengele peke yake ambacho Mungu anatoa ruhusa ya talaka na kuoa tena katika maandiko. Wengi hutafsiri maneno haya kuwa ni kile kitendo cha zinaa kinachofanyika baada ya kuolewa. Katika mila na desturi za wayahudi mke na mme walihesabiwa kuwa wameoana toka wakati wa kuposwa kwa msichana. Kitendo cha mapenzi kilichofanyika wakati huu pia kingehesabiwa sababu ya kutosha talaka.

Neno la kigiriki lilitafsiriwa kumaanisha uasherati ni neno linaloweza kumaanisha kila aina ya uchafu wa kimapenzi kama zinaa, uasherati, ukahaba na kadhalika. Yesu anathibitisha kuwa talaka inakubalika mahali uchafu huu wa kimapenzi unapotendeka. Kitendo cha ngono ni cha umuhimu mkubwa katika ndoa “nao wawili watakuwa mwili mmoja” (mwanzo 2:24; Mathayo 19:5; waefeso 5:31). Kwa hivyo kosa la kufanya kitendo hicho nje ya ndoa inaweza kuwa sababu mwafaka ya talaka. Kama ni hivyo basi pia Yesu alikuwa na hoja ya kuoa tena. Katika kusema “na kuoa mwingine” (Mathayo 19:9) inathibitisha talaka na kuoa tena vinakubalika. Jambo muhimu ni kutambua ya kwamba ni wale waathiriwa na hali mbaya ya mapenzi nje ya ndoa pekee wanaokubaliwa kuoa tena. Kukubaliwa huku,ijapokuwa hakukutajwa moja kwa moja katika maandiko, ni huruma ya Mungu kwa yule aliyetendewa dhambi wala si kwa aliyetenda dhambi ya zinaa. Katika maandiko haya hayaelezi kama mwenye kutenda dhambi ya zinaa naye aruhusiwa kuoa au la.

Wengine hukubali wakorintho wa kwanza 7:15 kama maandiko yanayokubali kuoa tena kama mke ama mume asiyeamini akimtalaki mumewe au mkewe. Maandiko hapa hayasemi aoe tena ila tu yanagusia sehemu ya ushirikiano wao kuwa hafungwi aendelee na ndoa hiyo kama asiyeamini anataka talaka. Katika haya yote ni muhimu kujua kuwa jambo uslikuwa na uhakika nalo juu ya Mungu usilitende.

Kitendo hiki cha zinaa si sharti la talaka bali ni nafasi ya talaka. Hata kitendo hiki kikitendeka, kwa neema ya Mungu, mke na mme wanaweza kunusuru ndoa yao kwa kusameheana. Mungu ametusamehe mengi. Tunaweza kuiga mfano wake hata kiasi cha kusamehe dhambi ya zinaa (waefeso 4:32). Lakini mara nyingi watu hukosa toba halisi katika swala hili hata kiasi cha kuishi katika maisha ya zinaa. Hapo ndipo Mathayo 19:9 hutumika. Wakati mwingine watu huoa mapema baada ya talaka hata kama Munhu baado anawataka wakae bila ndoa. Mungu wakati mwingine huita mtu akiwa peke yake ili ushirika wake na Mungu usitatizwe na mtu. (wakorintho wa kwanza 7:32-35). Kuoa tena baada ya talaka ni mapenzi ya mtu binafsi lakini haimaanishi kuwa ndilo suluhisho pekee.

Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa talaka za wakristo zimekuwa nyingi karibu sawa na za wale wasioamini duniani kote. Biblia inasisitiza kuwa Mungu hapendezewi na talaka (malaki 2:16 ) na kusameheana huko na kupatana upya ni alama mwafaka ya mwenye imani maishani (luka 11:4; waefeso 4:32). Mungu anatambua kuwa talaka itatendeka hata kati ya wanawe. Mwenye kutalakiwa au mwenye kuoa tena asijisikie kuwa hapendwi na Mungu sawa na wengine kama jambo hili limetukia maishani mwake wala si sawa na mathayo 19:9. Mungu hutumia hata hali ya dhambi ya mwanadamu kukamilisha mapenzi yake mema.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini juu ya talaka na kuoa tena?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries