settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kutafuta ufalme wa Mungu kwanza?

Jibu


Yesu alisema kutafuta kwanza ufalme wa Mungu katika Uhubiri Wake wa Mlima (Mathayo 6:33). Maana ya mstari huu ii wazi kama inavyoonekana. Tunapaswa kutafuta vitu vya Mungu kama kipaumbele juu ya mambo ya ulimwengu. Kimsingi, inamaanisha sisi tunapaswa kutafuta wokovu ambao ni wa asili katika Ufalme wa Mungu kwa sababu ni wa thamani zaidi kuliko utajiri wa ulimwengu wote. Je! Hii inamaanisha kwamba tunapaswa kupuuza kazi nzuri na ya kila siku ambayo inasaidia kuendeleza maisha yetu? La hasha. Lakini kwa Mkristo, lazima kuwe na tofauti katika mtazamo wao. Ikiwa tunatunza kazi ya Mungu kuwa kipaumbele-kutafuta wokovu wake, kuishi kwa kumtii, na kushiriki habari njema ya ufalme pamoja na wengine-basi atatunza mahitaji yetu kama alivyoahidi-na ikiwa huo ndio mpango, hofu yatoka wapi?

Lakini tunajuaje kama tunatafuta ufalme wa Mungu kwanza? Kuna maswali tunaweza kujiuliza. "Je, mimi hutumia wapi nguvu zangu? Je! Muda wangu wote na pesa zangu zimetumiwa kwenye bidhaa na shughuli ambazo hakika zitaangamia, au katika huduma ya Mungu- ambayo matokeo yanaishi milele? "Waumini ambao wamejifunza kumtii Mungu kwanza wanaweza kupumzika katika nguvu hii takatifu: "... na hayo yote mtazidishiwa."

Mungu ameahidi kuwalipa walio wake, akiwatimizia mahitaji yao yote (Wafilipi 4:19), lakini wazo lake la kile tunachohitaji mara nyingi ni tofauti na chetu, na wakati wake utakuwa mara kwa mara atatimiza matarajio yetu. Kwa mfano, tunaweza kuona haja yetu kuu kuwa utajiri au maendeleo, lakini labda Mungu anajua kile tunahitaji hasa na wakati wa umaskini, kupoteza au kutengwa. Wakati haya yanatokea, tuko katika kundi nzuri. Mungu alimpenda Ayubu na Eliya, lakini alimruhusu Shetani kumteza Ayubu (yote akiyaona), naye akamruhusu mwanamke mwovu, Yezebeli, kuvunja roho ya nabii Wake Eliya (Ayubu 1-2; 1 Wafalme 18-19). Katika matukio hayo yote, Mungu alifuatisha majaribu hayo kwa urejeshwa na udumisho.

Mambo haya "mabaya" ya ufalme yanakabiliana na ukatili ambao unapatikana duniani kote, kinachojulikana kama "Injili ya mafanikio." Idadi kubwa inaongezeka ya walimu wa uongo wanaokusanya wafuasi chini ya ujumbe "Mungu anataka uwe tajiri!" Lakini falsafa hiyo sio ushauri wa Biblia-na kwa hakika sio ushauri wa Mathayo 6:33, ambao sio mtindo ya kupata utajiri, bali ni maelezo ya jinsi Mungu anavyofanya. Yesu alifundisha kwamba lengo letu linapaswa kuwa mbali na dunia hii-hali yake na uongo wake-na kuwekwa juu ya mambo ya ufalme wa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kutafuta ufalme wa Mungu kwanza?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries