settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini kuna tafsiri nyingi tofauti za Wakristo?

Jibu


Biblia inasema kuna "Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja" (Waefeso 4:5). Kifungu hiki kinasisitiza umoja ambao lazima uwepo katika mwili wa Kristo sababu zote tumejazwa na "Roho mmoja" (mstari wa 4). Katika mstari wa 3, Paulo anaweka anawaita kwa unyenyekevu, upole, uvumilivu, na upendo- ambao yote ni muhimu kuhifadhi umoja. Kulingana na 1 Wakorintho 2:10-13, Roho Mtakatifu anajua mawazo ya Mungu (mstari wa 11), ambayo Yeye hufunulia (mstari wa 10) na kuwafundisha (mstari wa 13) kwa wale ambao hukaa ndani yake. Shughuli hii ya Roho Mtakatifu anaitwa kutiwa mwanga.

Katika ulimwengu kamili, kila muumini kijukumu ataitafiti Biblia (2 Timotheo 2:15) kwa maombi anategemea ujazo wa Roho Mtakatifu. Kama inavyoonekana wazi, hii dunia si kamilifu. Si kila mtu ambaye ana Roho Mtakatifu kweli anasikiliza Roho Mtakatifu. Kuna Wakristo ambao wanamhuzunisha Roho (Waefeso 4:30). Uliza msomi yeyote hata mwalimu bora kabisa darasani ana njia yake ya kuendelea na wanafunzi ambao huonekana kukataa kusoma, haijalishi mwalimu anafanya nini. Hivyo, sababu moja watu mbalimbali wana tafsiri tofauti ya Biblia ni kwamba baadhi yao hawamsikizi Mwalimu - Roho Mtakatifu. Zifuatazo ni baadhi ya sababu nyingine za tofauti mbalimbali ya imani miongoni mwa wale wanaofundisha Biblia.

1. Kutoamini. Ukweli ni kwamba wengi ambao wanadai kuwa Wakristo hawajawahi kuzaliwa tena. Wao huvaa nembo ya "Ukristo" lakini hakuchakuwa na badiliko la kweli mioyoni mwao. Wengi ambao hawaiamini Biblia kuwa na mamlaka ya kweli na kuifundisha. Wao wanadai kuzungumza kwa niaba ya Mungu na bado wanaishi katika hali ya kutoamini. Wingi wa tafsiri ya maandiko hutoka kwa vyanzo hivi.

Ni vigumu kwa kafiri kutafsiri maandiko kwa usahihi. "Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maan kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni" (1 Wakorintho 2:14). Mtu mwenye hajaokoka hawezi kuuelewa ukweli wa Biblia. Yeye hana ujazo wa roho. Zaidi ya hayo, hata kuwa mchungaji au msomi wa mambo ya kidini haimwakikishii mtu wokovu.

Mfano wa machafuko yaliyotokana na kutoamini hupatikana katika Yohana 12:28-29. Yesu anaomba kwa Baba, akasema, "Baba, litukuze jina lako." Baba anajibu kwa sauti inayosikika kutoka mbinguni, ambayo kila mtu yeyote aliye karibu huisikia. kumbuka, hata hivyo, tofauti katika tafsiri: "Umati ambao ulikuwa pale ulisema ulisikia sauti hiyo kama radhi; wengine walidai kuwa malaika alikuwa anaongea naye. "Kila mtu alipata habari sawa, taarifa kueleweka kutoka mbinguni na bado kila mtu alipata kusikia kile alitaka kusikia.

2. Ukosefu wa mafunzo. Mtume Petro anaonya dhidi ya wale ambao hutafsiri maandiko vibaya. Anahusisha mafundisho yao ya uongo katika sehemu kwa dhana kwamba wao ni "wapumbavu" (2 Petro 3:16). Timotheoi anaambiwa kwamba "Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neon la kweli" (2 Timotheo 2:15). Hakuna njia ya mkato kwa tafsiri sahihi ya Biblia, sisi tumeamurishwa kujifunza.

3. Ufafanuzi mmbaya. Makosa mengi yamekuzwa kwa sababu ya kushindwa kutumia ufafanuzi mzuri (sayansi ya kutafsiri maandiko). Kuchukua mstari nje ya mazingira yake unaweza kuleta uharibifu mkubwa kwa nia ya mstari. Kutozingatia mazingira pana ya sura na kitabu, au kushindwa kuelewa mazingira ya kihistoria / kitamaduni pia husababisha matatizo.

4. Upumbavu wa neno lote la Mungu. Apolo alikuwa muhubiri mashuhuri na fasaha, lakini alijua ubatizo wa Yohana tu. Hakuwa anamjua Yesu na utoaji wa wokovu wake, hivyo ujumbe wake ulikuwa haujakamilika. Aquila na Priscilla walomchukua kando na "kumwelezea zaidi njia ya Mungu kwa undani" (Matendo 18:24-28). Baada ya hapo, Apolo anahubiri juu ya Yesu Kristo. Baadhi ya vikundi na watu binafsi hii leo wana ujumbe haujakamilika kwa sababu watilia makini vifungu fulani na kutupilia nje vifungu vingine. Wao hushindwa kulinganisha maandiko kwa maandiko.

5. Ubinafsi na kiburi. Ni huzuni kusema, tafsiri nyingi za Biblia ni msingi mwenyewe kwa mtu binafsi, upendeleo na mafundisho yake hafifu. Baadhi ya watu huona fursa ya kunufaika kibinafsi na kukuza "mtazamo mpya" katika maandiko. (Angalia maelezo ya walimu wa uongo katika waraka wa Yuda.)

6. Kushindwa kukomaa. Wakati Wakristo hawakomai vile inawapasa, utunzaji wao wa neno la Mungu umeathirika. "Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maan hata sasa ninny ni watu wa tabia ya wmilini." (1 Wakorintho 3:2-3). Mkristo mchanga hayuko tayari kwa "nyama" ya neno la Mungu. Kumbuka kwamba ushahidi wa Mwili wa Wakorintho ni mgawanyiko katika kanisa lao (mstari wa 4).

7. Mkazo usio na maan wa utamaduni. Baadhi ya makanisa hudai wanaamini Biblia, lakini tafsiri yao daima huchujwa kupitia mila imara ya kanisa yao. Mahali utamaduni na mafundisho ya Biblia zinahitilafiana, utamaduni hupewa kibao mbele. Hii kwa ufanisi hupunguza mamlaka ya neno na kuipa mamlaka uongozi wa kanisa.

kwa mambo ya muhimu, Biblia kwa wingi ii wazi. Hakuna kitu cha utata kuhusu uungu wa Kristo, hali halisi ya mbinguni na kuzimu, na wokovu kwa neema kupitia imani. Katika baadhi ya masuala yasiyo na umuhimu, hata hivyo, mafundisho ya maandiko hayako wazi, na hii kwa kawaida inaongoza kwa tafsiri tofauti. Kwa mfano, hatuna amri ya moja kwa moja katika Biblia inayoongoza mawasiliano au mtindo wa muziki wa kutumia. Wakristo waaminifu, na wa kweli wanaweza kuwa na tafsiri tofauti ya vifungu kuhusu masuala haya muimu.

Jambo muhimu ni kuwa dogmatic ambapo maandiko ni na kuepuka kuwa wa mfumo wa imani ambapo maandiko hautambui. Makanisa lazima yajitahidi kufuata mfano wa kanisa la kwanza katika Yerusalemu: "Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali" (Matendo 2:42). Kulikuwa na umoja katika kanisa la kwanza kwa sababu walikuwa imara katika fundisho la mitume. Kutakuwa na umoja katika kanisa tena wakati sisi hurudia mafundisho ya mitume, na kusaahu mafundisho mengine, kivutio, na ujanja ambayo yameingia kanisani.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini kuna tafsiri nyingi tofauti za Wakristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries