settings icon
share icon
Swali

Je! Yamaanisha nini kuwa mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27)?

Jibu


Katika siku ya mwisho ya uumbaji, Mungu akasema, “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu” (Mwanzo 1:26). Na hivyo Akamaliza kazi yake kwa “uguzo wake mwenyewe.” Mungu alimuumba mwanadamu kutoka kwa udongo na akampa uhai kwa kumwekea pumzi yake (Mwanzo 2:27). Vilevile, mwanadamu ni kiumbe tofauti katika viumbe vyote alivyoviumba Mungu, vyote vikiwa na mwili wa nyama na wa ndani nafsi/roho.

Kuwa na “sura” ya Mungu yamaanisha, kwa ufupi, kwamba tuliumbwa tumfanane Mungu. Adamu hakumfanana Mungu kwa kuwa na mwili wa nyama na damu. Bibilia inasema kwamba “Mungu ni roho” (Yohana 4:24) na kwa hivyo anaishi bila kuwa na mwili. Ingawaje, mwili wa Adamu ulidhihirisha maisha ya Mungu vile yalikuwa makamilifu kwa afya na haukutishika na kifo.

Sura ya Mungu yamaanisha mwili wa ndani wa mwanadamu. Unatofautisha mwanadamu kutoka ulimwengu wa wanyama, na kumweka mwanadamu kufaa mamlaka Mungu alimuumbia kuwa nayo katika nchi (Mwanzo 1:28), na kumwezesha kuwa na ushirika na muumba. Mwanadamu anamfanana Mungu, kimawazo, tabia na maisha ya furaha.

Kimawazo, mwanadamu aliumbwa kama kiumbe kiwezacho, kuwa na uwezo wa kuamua. Kwa njia nyingine, mwanadamu anaweza kuwaza na kuchagua. Hii ni taswira ya hekima na uhuru wa Mungu. Wakati wowote mtu anaweza vumbua/gundua chombo (mashine), aandike kitabu, airembeshe picha ya nchi aliyoichora, na afurahie kucheza ngoma, afanye hesabu, ama avipatie viumbe majina, na hivyo anatangaza kuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.

Kitabia, mwanadamu aliumbwa kwa utakatifu na ukamilifu ukiambatana na, taswira ya utakatifu wa Mungu. Mungu akaona kila kitu alichokifanya (mwanadamu akiwemo) na akakiita “chema sana” (Mwanzo 1:31). Fikra zetu au “dira ya tabia” ni dalili ya ile hali ya asili. Popote mtu anaandika sheria, na kugeuka kutoka dhambi, kuisifu tabia njema, au kujishuku na hatia, hii inadhibitisha dhana kwamba tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.

Katika maisha ya ushirika, mwanadamu aliumbwa ili awe na ushirika. Hii inadhihirisha hali ya utatu wa Mungu na upendo wake. Katika Edeni, uhusiano wa mwanadamu ulikuwa na Mungu (Mwanzo 3:8 yamaanisha ushirika na Mungu), na Mungu akamuumba mwanamke wa kwanza kwa sababu “Si vyema huyo mtu awe pekee” (Mwanzo 2:18). Kila wakati mtu anapooa, anatengeza urafiki, kumpusu mototo, au kushiriki kanisa, ni kuonyesha kuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.

Sehemu ya kuumbwa kwa mfano wa Mungu ni kwamba Adamu alikuwa na uwezo wa kufanya uamuzi. Ingawa alipewa hali takatifu, Adamu akafanya uamuzi wa dhambi na kuasi kinyume na muumba wake. Kwa kufanya hivyo, Adamu akaiaribu sura ya Mungu ndani yake na akaupitisha huo ubaya kwa kizazi chake chote (Warumi 5:12). Hata hii leo bado twaibeba hiyo sura ya Mungu (Yakobo 3:9), lakini bado twavibeba vidonda vya dhambi kimawazo, kitabia, kimaisha ya kawaida na hata kimwili twaonyesha madhara ya dhambi.

Habari njema ni kwamba Mungu anamwokoa mtu binafsi, anaanza kurejesha sura ya kiasili ya Mungu, kuumbwa “mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli” (Waefeso 4:24). Huo wokovu upo tu kwa neema ya Mungu kupitia kwa imani katika Kristo Yesu aliyetuokoa kutoka dhambi ambayo ilitutenganisha na Mungu (Waefeso 2:8-9). Kupitia Kristo tumefanywa viumbe vipya kwa mfano wa Mungu (2Wakorintho 5:17).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Yamaanisha nini kuwa mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries