settings icon
share icon
Swali

Historia ya sulubu/kusulubiwa ni gani? Sulubu ilikuwa ya namna gani?

Jibu


Usulubu ulibuniwa na kutumika na makundi ya watu wengine, lakini "ulitimilishwa" na Warumi kama namna ya mauaji ya mwisho kwa kuteswa. Kumbukumbu ya awali ya historia ya kusulubiwa mwanzo wake ulikuwa mwaka wa 519 Kabla ya Kristo, wakati Mfalme Daria wa Kwanza wa Ajemi aliwasulubisha maasimu wake wa kisiasa 3,000 katika Babeli. Kabla ya Waajemi, Waashuru walijulikana kwa kuwatesa watu. Wagiriki na Watunisia baadaye walitumia usulubisho pia. Baada ya kusambaratika kwa Ufalme wa Alexander Mkuu, Seleucid Antiochus IV Epiphanes aliwasulubisha Wayahudi waliokataa tabia ya Kigiriki.

Kusulubiwa kulikusudiwa kudhalilisha kwa kiwango cha juu cha aibu na kumtesa mwadhiriwa. Sulubu ya Kirumi ilifanyika hadharani ili wale wote waliona karaha hiyo wangezuiliwa kutokana na kukaidi serikali ya Kirumi. Sulubu ilikuwa ya kutisha sana kwamba ilikuwa imetengewa tu wahalifu wabaya zaidi.

Mwathiriwa wa sulubu kwanza alikuwa anadhibiwa au kuchapwa vibaya sana, mateso ambayo yenyewe yalikuwa yanahadharisha miasha. Kisha alilazimishwa kuubeba msalaba mkubwa uliotengezwa kwa mbao hadi mahali pa kusulubiwa. Kuubeba uzito huu haukuwa wa uchungu pekee baada ya kichapo, bali uliongeza kiwa cha aibu kadiri na mwathiriwa alipokuwa akibeba silaha ya mateso na kifo chake. Ilikuwa sawia na kjichimbia kaburi mwenyewe.

Wakati mwathiriwa alipofika mahali pa kusulubiwa, angevuliwa uchi ili kumwaibisha zaidi. Basis angelazimishwa kunyoosha mikono yake, ambapo iligongelewa misumari. Misumari iligongelewa katiki kiwiko/kifundo, na sio katika kitanga, ambayo hii ilizuia misumari kutoka kwa kuvuta kwa mkono. (katika nyakati za zamani, kiwiko kilichukuliwa kuwa sehemu ya mkono.) kuwekwa kwa misumari katika kiwiko pia kulisababisha uchungu mkali wakati misumari ilikuwa inagandamiza mishipa inayopita mkononi. Mlingoti wa msalaba uliinuliwa juu na kukazwa ndio uweze kusimima kipindi chote cha sulubu.

Baada ya kuukaza ule mlingoti wa juu, watekelezaji mauaji vile vile waligongerea msumari katika mguu wa mwathiriwa, mguu mmoja ukiwa juu ya mwingine, huku msumari ukipita kati kati ya kila mguu, magoti yakiwa yamekunjika kidogo. Kusudi la msumari ilikuwa kuzidisha uchungu.

Pindi mwathiriwa alifungiliwa msalabani, uzito wake wote ulihimilishwa na misumari, ambayo ingesababisha uchungu katika mwili wake wote. Mikono ya mwathirwa ilinyoshwa kwa namna ambayo ingesababisha kiharusi na kupooza katika musuli wa kifua, kuifanya ngumu kupumua isipokuwa sehemu ya uzito ulibebaka kwa miguu. Ili apate kupumua mwathirwa alilazimika kujisukuma juu kwa miguu yake. Fauka ya kustahimili uchungu mkali uliosababishwa na msumari katika miguu yake, mgongo wa mwathiriwa ungekwarusana na mlingoti wa msalaba.

Baada ya kuchukua pumzi ili apunguze makali ya uchungu katika miguu yake, mwathiriwa ghafula alianza kuanguka chini tena. Kitendo hiki kilitia uzito katika kiwiko na tena kusugua mgongo wake dhidi ya msalaba. Walakini, mwathiriwa hangeweza kupumua akiwa katika nafasi ya dari, kwa hiyo kabla ya muda mrefu mateso tena yangeanza. Ili apumue na kujunusuru uchungu kiasi ambao ulisababishwa na misumari katika kiwiko chake, mwathiriwa angelazimika kuweka uzito katika misumari ya miguu na kujisukuma juu. Ili apunguze baadhi ya maumivu yaliyosababsihwa na misumari ya miguu, mwathiriwa angelazimika kutia uzito katika misumari iliyotiwa katika kiwiko na kushuka chini. Katika hali yoyote uchungu ulizidi.

Usulubu iliongoza katika kifo cha pole pole. Baadhi ya waathiriwa wangeishi takribani siku nne msalabani. Kifo kilitokna na msongo wa moyo pindi mwathiriwa alipoteza nguvu ya kuendelea kujisukuma juu kwa migu yake ili apate pumzi zaidi. Ndio waarakishe kifo miguu ya mwathiriwa ilivunjwa ili kumzuia kujisukuma juu ili apate pumzi; na hivyo msongo wa roho ungefuata muda mfupi (ona Yohana 19:32).

Sulubu baadaye ilipigwa marufuku na Mfalme wa Kirumi Konstantine katika karne ya nne.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Historia ya sulubu/kusulubiwa ni gani? Sulubu ilikuwa ya namna gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries