settings icon
share icon
Swali

Je, somo la Roho Mtakatifu ni nini?

Jibu


Somo la Roho Mtakatifu ni somo kuhusu Mungu-Roho Mtakatifu, Mtu wa tatu wa Utatu. Inajibu maswali mengi muhimu kuhusu Roho Mtakatifu.

Je Roho Mtakatifu ni nani/ni nini? Kuna maoni mengi potovu kuhusu nafsi ya Roho Mtakatifu. Wenginehuona Roho Mtakatifu ni kama nguvu ya kushangaza. Wengine wanaelewa Roho Mtakatifu kuwa kama nguvu isiyo na nafsi hai ambayo inapatika kwa wafuasi wa Kristo. Je! Biblia inasema nini kuhusu uthibitisho wa Roho Mtakatifu?

Ni lini/ni namna gani tunapokea Roho Mtakatifu? Mjadala huu ni tata kwa sababu huduma za Roho Mtakatifu mara nyingi huchanganywa. Upokeo/umimino wa Roho hutokea wakati wa wokovu. Kujazwa kwa Roho mchakato unaoendelea katika maisha ya Mkristo.

Je! ubatizo wa Roho Mtakatifu ni nini? Ubatizo wa Roho Mtakatifu unaweza kufafanuliwa kama kazi ambayo Roho wa Mungu anamweka muumini katika ushirika na Kristo na ushirika na waumini wengine katika mwili wa Kristo dakika ya wokovu.

Je! ninawezaje kujazwa na Roho Mtakatifu? Ni muhimu kutofautisha kati ya kumiminiwa na kujazwa na Roho. Ujazo wa kudumu wa Roho sio wa baadhi ya waumini, bali kwa waumini wote. Hii ni tofauti kabisa na ujazo wa kiamri wa Roho katika Weaefeso 5:18).

Je! karama za miujiza za Roho ziko kwa ajili ya siku hizi? Hili si swali la kuwa Roho Mtakatifu anaweza kumpa mtu karama ya miujiza. Swali ni, je! Roho Mtakatifu bado anatoa karam za miujiza hii leo. Zaidi ya yote, kikamilifu tunatambua kuwa Roho Mtakatifu ako huru kuepana karama kulingana na mapenzi yake (1Wakorintho 12:7-11).

Wakristo wengi wako na mtazamo usio wa kibiblia kuhusu Roho Mtakatifu. Baadhi wanaelewa Roho Mtakatifu kuwa na uwezo au nguvu tumepewa na Mungu. Hii sio kibiblia. Somo la Roho Mtakatifu linafunza kuwa Roho Mtakatifu ni nafsi, iliyo na akili, hisia na nia. Roho Mtakatifu ni aliyekuja kwa niapa ya Yesu duniani (14:16-26; 15:26; 16:7). Roho mtakatifu hupokewa katika wokovu (Warumi 8:9) na miliki ya kudumu ya kila muumini katika Kristo (Waefeso 1:13-14). Uchunguzi wa Roho Mtakatifu hutusaidia kuelewa masuala haya na kutambua jukumu la Kibiblia la Roho Mtakatifu katika maisha yetu hii leo.

Somo la Roho Mtakatifu ni la umuhimu zaidi kwa Mkristo. Katika kurasa za Maandiko tunakutana ana kwa na na mtu wa tatu katika Utatu, Mungu mwenyewe katika roho, na tunaona huduma yake kwetu. Kupitia kwake, tunamjua upendo wa Mungu kwetu "wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia" (Warumi 5:5). Kuelewa huduma ya Roho Mtakatifu ni kupata furaha katika jukumu lake kama mfariji wetu (Yohana 16:7; Matendo 9:31) ambaye hatusaidii na kutufariji pekee, bali anakuja kwa usaidizi wetu wakati mioyo yetu imelemewa kiwango hatuwezi kuomba usaidizi (Warumi 8:26). Wakati tunatafuta kufahamu Roho Mtakatifu tunapata furaha kuwa haishi ndani yetu pekee, bali milele kamwe hawezi kutuacha (Yohana 14:16). Kweli hizi zote zinawekwa ndani ya mioyo yetu wakati tunachunguza zaidi habari za Roho Mtakatifu.

Aya nzuri ya muhtasari wa somo la Roho ni Yohana 16:8-11, "Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi, kwa habari ya haki, kwa sababu ninakwenda kwa Baba, nanyi hamtaniona tena, kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa."

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, somo la Roho Mtakatifu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries