settings icon
share icon
Swali

Kwa nini sehemu kubwa ya ulimwengu bado sio ya kiinjilisti?

Jibu


Maagizo ya mwisho ya Yesu kwa wafuasi wake yalikuwa "basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari"(Mathayo 28:19-20). Tunajua kwa kusoma kitabu cha Matendo ya Mitume kwamba wanafunzi walifanya hivyo tu. Baada ya Roho Mtakatifu akishuka juu yao, wakaanza kutangaza ujumbe wa Mungu kwa ujasiri (Matendo 2:4). Mungu aliwapa uwezo wa ajabu wa kuzungumza kwa lugha zingine ili watu kutoka nchi nyingi za kigeni kusikia habari njema (Matendo 2:6). Watu hao waliamini na kisha wakachukua ujumbe wa Mungu wa wokovu katika nchi zao, na injili ikenea.

Licha ya mashambulizi katika historia zima ya kuondoa kabisa Ukristo, ujumbe wa Injili unaendelea kuenea kama maisha yanabadilishwa na upendo wa Yesu. Wamisionari wameacha kila kitu kusafiri katika mikoa ngumu ili kuleta habari njema kwa wenyeji huko. Kupitia uinjilisti wa kibinafsi, redio, televisheni, mtandao, fasihi, na njia nyingine nyingi, watu duniani kote wanasikia wokovu wa Yesu na kuitikia. Tunasikia Waislamu katika nchi zilizofungwa kupata maono na ndoto na katika hii Yesu anawaonekania na wanaridhika kwa utambulisho Wake kama Mwana wa Mungu. Bado, kama wakazi wa dunia wanavyoongezeka, hivyo ndivyo ilivyo idadi ya watu wasiofikiwa na habari. Licha ya juhudi za kanisa, mamilioni ya watu bado hawajapata kusikia kuhusu Yesu. Kwa kweli, baadhi ya maeneo ya ulimwengu ambayo yalikuwa na uwepo mkubwa wa Kikristo, kama vile Uturuki na Afrika Kaskazini, sasa ni ngome za dini ya uwongo.

Sababu moja ambayo sehumu kubwa ya dunia bado ni isio ya kiinjilisti ni kutokana na umbali wa makundi ya watu fulani. Wachunguzi bado wanagundua watu wa kikabila na vijiji hadi hapa nje ya ramani kwamba hakuna mtu aliyejua juu ya kuwepo kwao. Kuhusiana na hilo, vikundi vya watu wengine huzungumza lugha ambazo wamishonari bado hawajafumbua, hivyo kuwasiliana nao ni karibu haiwezekani kabisa. Bado makabila na mataifa mengine ni maadui kwa watu wa nje au Wakristo kwamba kuwafikia ni hatari. Wengi wamejaribu kuwafanya wanafunzi makundi kama hayo na kupoteza maisha yao katika mchakato, na mipaka ya nchi imekua kukazwa tu.

Bado sababu nyingine ya sehumu kubwa ya dunia vado ni isio ya kiinjilisti ni kutojali kati ya Wakristo wengi katika tamaduni za Magharibi. Maneno ya Yakobo yanaweza kutumika kwa sisi ambao ni matajiri ikilinganishwa na ulimwengu wote: "Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashake yenu yanayowajia. Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. . . . Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa ..."(Yakobo 5:1-5).

Hiyo ni maneno makali kwa masikio yetu, lakini tunapaswa kujichunguza wenyewe ili tuone ikiwa yanatumika kwa mtazamo wetu kuhusu rasilimali zetu wenyewe. Yesu alifundisha kwamba tunapaswa "jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele" (Luka 16:9). Kwa maneno mengine, lazima tutumie rasilimali zetu katika ulimwengu huu ili kuendeleza kazi ya Mungu; matokeo yake yatakuwa watu wengi mbinguni.

Je! Tunaona fedha zetu kama zetu wenyewe kutumia kwa raha zetu? Au kama utoaji kutoka kwa Mungu kutumiwa chini ya uongozi Wake? Je! Tunafikiri wakati wetu kama wetu kuufanya tupendavyo? Au kama zawadi kutoka kwa Mungu kuutumia katika kutekeleza mapenzi Yake? Je! Tunafikiria vipaji vyetu kama vitu vinavyotumiwa tu kushawishi kwa faida ya kibinafsi? Au je, tunaviona kama zawadi kutoka kwa Mungu kuzitumia kama atakavyotaka? Je! Tunawaangalia maskini na wale wa mataifa maskini wakati wa kuamua jinsi ya kutumia rasilimali zetu? Je! Mungu ametuita kwa ujumbe wa kigeni lakini tunakataa? Je! Yeye ametuita ili tusaidie mjumbe au huduma fulani katika sala, lakini mara nyingi tunawasahau? Je, sisi ni wasimamizi wazuri wa utoaji ambao Mungu ametupa, na je, sisi ni makini kuutumia kama anavyokusudia? Je! Tunatafuta ufalme Wake kwanza na kushiriki katika kuenea kwa injili kwa njia ambayo ametuita kwa hali yetu ya maisha? Moja ya sababu watu wengi hawajasikia injili ni kwamba watu wa Mungu wanakataa kuchukua injili kwao. Hebu tusiwe wa kuzoea kwa injili kwamba tunashindwa kutamani kuiona ikienea na kufanya kile tunaweza kufanya kazi hadi mwisho huo.

Katika Mathayo 11:21-24 Yesu anazungumzia miji ambapo alikuwa amehubiri na kufanya miujiza, bado walikuwa wamekataa kumwamini: "Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingelifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe." Hii inaonekana kusema kwamba Mungu atatufanya kuwajibika kwa fursa ambazo tumepewa (Mathayo 10:14-15). Kwa kuwa Mungu ni hakimu mwenye haki (Zaburi 7:11), tunaweza kuamini kwamba Yeye atafanya yaliyo sawa wakati watu wasiofikiwa wamesimama mbele Yake siku ya hukumu. Hata hivyo, sisi pia tutatoa akaunti ya kama tulikuwa tunatii amri Yake ya kuwaambia juu Yake (Mathayo 12:36; 2 Wakorintho 5:10).

Kila Mkristo ana fursa nyingi za kusaidia kutatua tatizo la watu wasio na uinjilisti. Kama mazingira yako yanaruhusu, unaweza kufanya moja au zaidi ya yafuatayo:

• Kutoa kwa mashirika ya misheni.

• Kusaidia watoto masikini kupitia idadi yoyote ya mashirika ya misaada ambayo yanakidhi mahitaji ya kimwili na ya kiroho ya watoto kote ulimwenguni.

• Mwombe Bwana ikiwa angekuwezesha kuwa mtumishi wa wakati wote.

• Chukua safari ya misheni ya muda mfupi kwenye sehemu isiyofikiwa. Kwa kukadiria mahitaji ya watu moja kwa moja, sisi mara nyingi huchochewa na shauku ya kuwafikia. Mashirika mengi yenye ufanisi yalianza wakati mtu mmoja aliona hitaji.

• Ikiwa una ujuzi wa lugha, uwe mtafsiri wa Biblia.

• Acha kufanya udhuru kwa sababu ya hofu au uvivu. Ikiwa Mungu anakuita, Yeye atakukimu.

• Kadiria talanta zako, vipawa, na rasilimali ili kuona nini kinachoweza cha manufaa kwa kueneza injili kwa watu ambao hawajafikiwa. (Mifano: leseni ya rubani, ujuzi wa shirika, utajiri wa fedha, ujuzi wa mitambo, ujuzi wa matibabu, nk)

Alipopaa mbinguni, Yesu aliwapa ujumbe Wake kwa watu wachache. Angeweza kusafiri zaidi kuliko alivyofanya wakati wa huduma Yake duniani. Angeweza kufanya safari za kimishonari ambazo Paulo alifanya. Angeweza kutuma malaika kuhubiri injili kila mahali. Lakini hakufanya kitu chochote kati ya hivyo. Badala yake, aliwapa ujumbe muhimu zaidi ulimwenguni kwa watu walio na makosa. Bado ujumbe huo umebadilisha ulimwengu kwa sababu wale watu waliojazwa na Roho walikuwa tayari kutoa yao yote. Wakati kila mtu anayedai kumfuata Kristo pia ana nia ya kutoa yote, tunaweza kupunguza tatizo la watu wasio na uinjilisti kwa utukufu wa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini sehemu kubwa ya ulimwengu bado sio ya kiinjilisti?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries