settings icon
share icon
Swali

Je! Masimulizi tofauti kutoka vitabu vinne vya Injili zinaweza patanishwa?

Jibu


Matukio yanayozunguka ufufuo wa Yesu yanaweza kuwa magumu kuyaweka pamoja. Lazima tukumbuke mambo mawili: kwanza, Habari ya ufufuo wa Yesu ilitoa msisimuko mkubwa kule Yerusalem, na kwa machafuko yaliyofuatia watu walitawanyika kwenda pande tofauti. Makundi yalitawanyika, na makundi mbali mbali tofauti yalitembelea kaburi, pengine zaidi ya mara moja. Pili, waandishi wa Injili hawakujaribu kutoa simulizi ya upana; kwa meneno mengine, Mathayo, Marko, Luka, na Yohana hakuwa na nia ya kutuambia kila simulizi kamili ya ufufuo au kila tukio jinsi yaliyotokea.

Katika makabiliano na wapingamizi kuhusu ufufuo wa Yesu, Wakristo wako katika hali "wasio weza kushinda." Ikiwa simulizi ya ufufuo inaweza kuainishwa kikamilifu, wakosoaji watadai kwamba waandishi wa Injili njama kwa Pamoja. Ikiwa simulizi ya ufufuo ina tofauti, wakosoaji watadai kuwa Injili inajikanganya yenyewe na kwa hivyo haiwezi kuaminika. Ni ubishi wetu kuwa simulizi ya ufufuo inaweza kuainishwa na haijikanganyi yenyewe.

Walakini, hata kama simulizi ya ufufuo haiainiki kikamilifu, hiyo haifanyi kuwa isiyo ya maana. Kwa tathimini yoyote ifaayo, simulizi ya ufufuo kutok vitabu vinne vya Injili ni ushahuda thabiti wa walio shuhudia. Kweli kuu-ni kuwa Yesu alifufuka kutoka kwa wafu, na Yesu aliyefufuka aliwatokea watu wengi-ni mafundisho wazi katika kila kitabu cha Injili. Kutofanana kwa simulizi ni "masuala pande." Waliona malaika wangapi kule kaburini, mmoja au wawili? (Labda mtu mmoja aliona malaika mmoja, huku mtu mwingine akiona malaika wawili). Yesu aliwaonekania wanawake wangapi, na alimwonekania nani kwanza? (huku kila kitabu cha Injili kikiwa na utaratibu tofauti kidogo juu ya kuonekania, hakuna hata moja ya Injili inadai kupewa utaratibu mwafaka.) Kwa hivyo, huku simulizi ya ufufuo ikionekana kutoambatana, haiwezi kuthibitishwa kuwa simulizi hizi zinahitilafiana.

Hapa kuna uwiano uwezekanao wa simulizi ya ufufuo wa Kristo na kuonekana kwake baada ya ufufuo kwa namna ya utaratibu:

Yesu amezikwa, na wanawake kadhaa walishuhudia (Mathayo 27:57-61; Marko 15:42-47; Luka 23:50-56; Yohana 19:38-42).

Kaburi ilifunikwa na askari akawekwa kuilinda (Mathayo 27:62-66).

Angalau wanawake 3, wakiwa ni Pamoja na Mariamu Magdalene, Mariamu mamake Yakobona Salome walitengeneza manukato ya kupeleka kaburini (Mathayo 28:1; Marko 16:1).

Wale wanawake walifika kaburini na kulipata tupu. Mariamu Magdalene akawaacha wale wanawake wengine pale kaburini na kukimbia kuwaambia wanafunzi wa Yesu (Yohana 20:1-2).

Malaika akashuka kutoka mbinguni na kubingirisha lile jiwe, na kuketi juu yake. Kulikuwa na mtetemeko na wale askari wakazimia (Mathayo 28:2-4).

Wanawake bado wakiwa wangali kaburini wakawaona malaika wawili ambao waliwaambia kuwa Yesu amefufuka na kuwaambia waamurishe wanafunzi wa Yesu waende Galilaya (Mathayo 28:5-7; Marko 16:2-8; Luka 24:1-8).

Wale wanawake wakaondoka na kuleta Habari njema kwa wanafunzi (Mathayo 28:8).

Baada ya wale askari kujiamsha, walipiga repoti kwa viongozi kuhusu kabru tupu, na viongozi hao wakawapa askari rushwa waseme kuwa mwili uliibiwa (Mathayo 28:11-15).

Mariamu mamake Yakobo na wanawake wengine, wakiwa njiani kwenda kuwatafuta wanafunzi, wanamwona Yesu (Mathayo 28:9-10).

Wanawake hao wakawaelezea wanafunzi chenye waliona na kusikia (Luka 24:9-11).

Petro na Yohana wanakimbia kaburini, kuona kama lii tupu, walipata sanda za kaburi (Luka 24:12; Yohana 20:2-10).

Mariamu Magdalene walirudi kaburini. Anawaona malaika, na baaday anamwona Yesu (Yohana 20:11-18).

Baadaye siku hiyo Yesu akamtokea Petro (Luka 24:34; 1Wakorintho 15:5).

Bado siku hiyo hiyo, Yesu alimtokea Kleopa na mwanafunzi mwingine njiani kuelekea Emau (Luka 24:13, 32).

Jioni hiyo, hao wanafunzi wawili waliwapasha wale kumi na mmoja yalitokea (Luka 24:32-35).

Yesu anawatokea wanafunzi kumi-Tomaso hakuwa (Luka 24:36-43; Yohana 20:19-25).

Yesu anawatokea kumi na mmoja wote-Tomaso akiwemo (Yohana 20:26-31).

Yesu anawatokea wanafunzi saba kando mwa bahari ya Galilaya (Yohana 21:1-25).

Yesu aliwatokea takribani wanafunzi 500 kule Galilaya (1Wakorintho 15:6).

Yesu anamtokea kakaye wa kambo Yakobo (1Wakorintho 15:7)

Yesu anawapa amri wanafunzi wake (Mathayo 28:16-20).

Yesu anawafunza wanafunzi wake Maandiko na kuwaahidi kuwatumia Roho Mtakatifu (Luka 24:44-49; Matendo 1:4-5).

Yesu anapaa kwenda mbinguni (Luka 24:50-53; Matendo 1:6-12).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Masimulizi tofauti kutoka vitabu vinne vya Injili zinaweza patanishwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries