settings icon
share icon
Swali

Je, Mwanzo sura ya 1 inamaanisha saa 24 halisi za siku?

Jibu


uchunguzi wa makini wa neno la Kiyahudi la "siku" na mazingira ambayo linaonekana katika Mwanzo itaongoza katika hitimisho kwamba "siku" ina maana halisi ya kipindi cha saa 24 cha muda. Kiebrania neno yom lilotafsiriwa katika Kiingereza "siku" linaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Yaweza maanisha kipindi cha muda wa saa 24 ambao dunia inachukua mzunguko kwenye mhimili wake (kwa mfano, "kuna masaa 24 kwa siku"). Inaweza rejelea kipindi cha mchana kati ya asubuhi na jioni (kwa mfano, "hukuwa na joto kiazi wakati wa mchana lakini baridi kidogo wakati wa usiku"). Na inaweza rejelea kipindi wakati usiojulikana (kwa mfano, "mbeleni katika siku za babu yangu ..."). Linatumiwa kwa kurejelea kipindi cha saa 24 katika Mwanzo 7:11. Limetumiwa kurejelea kipindi cha mchana kati ya asubuhi na jioni katika Mwanzo 1:16. Na litumiwa kwa kurejelea kipindi kisichojulikana cha wakati katika Mwanzo 2:4. Hivyo, linamaanisha nini katika Mwanzo 1:5-2:2 wakati limetumika kwa kushirikiana wa idadi ya kawaida (yaani, siku ya kwanza, siku ya pili, siku ya tatu, siku ya nne, siku ya tano, siku ya sita, na siku ya saba)? Je, hivi ni vipindi vya saa 24 au ni kitu kingine? Je, Yom jinsi limetumika hapa linamaanisha kipindi kisichojulikana cha wakati?

Tunaweza kuamua jinsi yom linaweza kufasiriwa katika Mwanzo 1:5-2:2 kwa kuchunguza mazingira ambayo sisi hulipata neno na kisha kulinganisha mazingira yake na jinsi sisi huona matumizi yake mahali pengine katika maandiko. Kwa kufanya hivyo sisi huruhusu maandiko kujitafsiri yenyewe. Kiebrania neno yom limetumika mara 2301 katika Agano la Kale. Nje ya Mwanzo 1, yom pamoja na idadi (limetumika mara 410) daima linaonyesha siku ya kawaida, yaani, kipindi cha saa 24. Maneno "jioni" na "asubuhi" pamoja (mara 38) daima yanaonyesha siku ya kawaida. Yom + "jioni" au "asubuhi" (23 times) daima inaonyesha siku ya kawaida. Yom + "usiku" (52 times) daima inaonyesha siku ya kawaida.

Mazingira ambayo neno yom limetumika katika Mwanzo 1:5-2:2, likielezea kila siku kama "jioni na asubuhi," linaiweka wazi kabisa kwamba mwandishi wa Mwanzo alimaanisha vipindi vya saa 24. Rejeleo la "jioni" na "asubuhi" hazileti maana isipokuwa zirejelee masaa 24 halisi ya siku. Hii ndio ilikuwa kiwango tafsiri cha siku za Mwanzo 1:5-2:2 hadi miaka ya 1800 wakati mabadiliko ya dhana ilitokea ndani ya jamii ya kisayansi, na tabaka ya mwamba wa dunia ilipotafsiriwa upya. Ambapo awali tabaka ya mwamba ilifasiriwa kama ushahidi wa gharika ya Nuhu, mafuriko yalitupiliwa mbali na jamii ya kisayansi na tabaka za mwamba zilifasiriwa upya kama ushahidi kwa ajili ya dunia ya zamani. Baadhi ya maana nzuri lakini huchukuliwa kimakosa na Wakristo kisha kutaka kupatanisha pingamizi hili mpya mafuriko, na tafsiri pingamizi za Biblia kwa hesabu ya Mwanzo na kutafsiri yom kwa kuwa na maana kubwa, vipindi visivyojulikana ya wakati.

Ukweli ni kwamba wengi wa tafsiri za dunia ya zamani zinajulikana kutegemea mawazo mbaya. Lakini tusiruhusu ukaidi wa mafikirio finyu wa wanasayansi ushawishi jinsi tunavyosoma Biblia. Kulingana na Kutoka 20:9-11, Mungu alitumia siku sita kuumba dunia ili kutumika kama mfano wa kuigwa kwa wiki ya kazi ya mwanadamu: Fanya kazi siku sita, na pumzika moja. Hakika Mungu angeweza kuumba kila kitu katika wakati mmpja kama Angetaka. Lakini inaonekana Alikuwa na picha yetu katika mawazo yake hata kabla atuumbe (siku ya sita) na alitaka kutoa mfano kwetui kuufuata.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mwanzo sura ya 1 inamaanisha saa 24 halisi za siku?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries