settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kushinda hofu yangu ya siku za mwisho?

Jibu


Yesu alisema kwamba nyakati za mwisho zitajumuisha matukio ya kutisha; Kwa hakika, "watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu" (Luka 21:26). Watu wengine leo wamejaa hofu tu kufikiri juu ya nini kitatokea. Lakini Bwana hataki tuogope: "Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme" (Luka 12:32).

Njia bora ya kuondokana na hofu ya siku za mwisho ni kuwa tayari kiroho. Kwanza kabisa, lazima uwe na uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo ili uwe na uzima wa milele (Yohana 3:16; Waroma 10: 9-10). Kwa njia Yake tu unaweza kupokea msamaha wa dhambi na kuwa na Mungu milele. Ikiwa Mungu ni Baba yako na Yesu ni Bwana wako, hakuna kitu utakacho hofia (Wafilipi 4: 7).

Pili, kila Mkristo anatakiwa kuishi maisha inayostahili wito tuliyo nao katika Kristo. Waefeso 4: 1¬-3 inafundisha, " Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu." Kumjua Kristo na kutembea katika mapenzi Yake huenda kwa njia ndefu tunaelekea ili kuondokana na hofu ya aina yoyote.

Third, Christians are promised God's deliverance, and it's encouraging. First Thessalonians 4:13–18 notes,

Tatu, Wakristo wanaahidiwa ukombozi wa Mungu, na inatia moyo. Wathesalonike wa Kwanza 4: 13-18 inasema,

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo

Mbali na hofu ya siku zijazo, tunapaswa kuzitarajia kwa furaha. Wale ambao wako ndani ya Kristo watachukuliwa juu ili kukutana naye, na sisi "tutakuwa pamoja na Bwana milele."

Zaidi ya hayo, Maandiko inasema hatupazwi kuogopa siku ya hukumu: "Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu. Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo" (1 Yohana 4: 17-18).

Wale ambao hawamjui Kristo hawana ahadi ya amani kwa siku zijazo. Kwa wasioamini, kuna wasiwasi halisi kwa sababu hawajawahi kutatua suala la ni wapi watakavyoishi milele. Wasioamini hawatachukuliwa katika unyakuzi na watapata shida; Hakika wao wana kitu cha kuogopa. Waumini hawaogopi mwisho wa siku. Badala yake, tunajitahidi kuishi maisha tunayostahili wito wetu, kutarajia kurudi kwa Yesu, na kupumzika katika ujuzi kwamba nyakati zetu ziko mikononi mwake (Zaburi 31:15).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kushinda hofu yangu ya siku za mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries