Swali
Mkristo anapaswa kuitikia aje sifa za Mungu?
Jibu
Mungu hujifunua mwenyewe kwa waumini kupitia kwa Neno lake (biblia) na kupitia kwa Mwana wake (Kristo Yesu). Tunavyo soma Biblia Zaidi, ndivyo tunavyo elewa zaidi sifa za Mungu, safa ambazo yeye humiliki. Kama wanadamu tunatatizika kufahamu nguvu na ukuu wa Mungu ambaye ameumba wakati, anga, vinavyoonekana na maisha yote. "Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu" (Isaya 55:9).
Kwa kusudi la nakala hii tutazingatia juu ya sifa kuu tatu za Mungu na itikio la Mkristo kwa kila moja yapo.
Pengine sifa muhimu ya Mungu ni sifa adilifu ya utakatifu wake. Isaya 6:3 na Ufunuo 4:8 zinaelezea aina tatu za utakatifu wa Mungu. "Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja." Ni punde tu mtu anapopata ufunusi wa utakatifu wa Mungu kwa mjibu wa hali ya dhambi ya mwanadamu kunaweza kuwa na tumaini lolote la toba ya kweli. Tunapogundua kadri ya madhara ya dhambi na kuzingatia kwamba Mwana wa Mungu ambaye hakuwa na dhambi aliteseka kwa ajili yetu, itatufanya kupiga magoti. Utakatifu wa Mungu hutukimya mbele zake, tunagugumizwa na hofu kutokana na ile utakatifu unahitaji. Kama vile Ayubu alisema, "Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu" (Ayubu 40:4). Kuelewa utakatifu wa Mungu unatusababisha kusifu ukarimu wake (2Wakorinto 1:3), neema (Warumi 9:15), na msamaha (Warumi 5:17) wake kwetu. "Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe" (Zaburi 130:3-4).
Pengine tabia ya Mungu inayopendeza zaidi ni upendo. Upendo unahitaji uhusiano na milele yote Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wameishi pamoja katika uhusiano. Mungu alituumba kwa mfano wake, na tuliumbwa ili tuwe na uhusiano Naye (Mwanzo 1:27); Warumi 1:19-20). Huo ndio ukadri wa upendo wa Mungu kwamba alimtuma Mwanawe wa pekee ili atukomboe kutoka dhambini. "Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu;" (1Yohana 3:16). "Mungu ni upendo... Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza" (1Yohana 4:16-19). Mungu alitoa suluhisho ya dhambi katika utu wa Kristo Yesu. Yesu alikuja kuchukua adhabu ya dhambi na kuridhisha haki ya Mungu (Yohana 1:1-5,14,29). Kule Kalvari upendo wa Mungu kamilifu na haki yake kamilifu zilikutana. Tunapoanza kuelewa upendo mkuu wa Mungu, itikio letu litakuwa unyenyekevu, toba na upendo kwa wenginge. Kama mfalme Daudi tutaomba kuwa Mungu ataumba ndani yetu moyo safi na roho wa kubondeka (Zaburi 34:18; 51:10,17). Mungu huishi mahali pa juu na patakatifu, lakini pamoja naye ni wahumini ambao wamebondeka na kuvunjika katika Roho (Isaya 57:15).
Hatimaye, tutaangazia Ukuu wa Mungu (Zaburi 71:16; Isaya 40:10). Mungu ni wa milele, milele hata milele (Zaburi 90:2). Yeye ndiye chanzo cha kila uai (Warumi 11:33-36). Yeye yu huru kutokana na viumbe vyake (Matendo 17:24-28). Ibrahimu, Samueli, Isaya, Danieli, na Daudi wote walimtambua Mungu kama Bwana wao: "Uhimidiwe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele. Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote. Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote. Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu" (Maneno ya Daudi katika 1Mambo ya Nyakati 29:10-13). Muumini humtukuza Mungu Mkuu ambaye ametuleta na kunyenyekea kwake kwa hiari (Yakobo 4:7; Yuda 1:4).
Mfalme Daudi kwa ufasaha alieka katika mkutasari sifa za Mungu: "Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike; Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele…Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu. Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele" (Zaburi 93:1-2,4-5).
Baadhi ya mababa wa imani wamekuwa na nafasi ya kipekee ya kushuhudia uwepo wa Mungu, kupata Mungu kunena nao moja kwa moja. Hivi ndivyo baadhi waliitikia:
Musa aliuliza kuona utukufu wa Bwana, na Bwana akakubali kufanya wema wake kutokea mbele ya Musa. "kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita" (Kutoka 33:21-22). Itikio la Musa lilikuwa kuinama katika kuabudu (Kutoka 34:6-8). Kama Musa, waumini watipiga magoti na kumwabudu Bwana, wakijazwa na hofu ya Mungu wanapotafakari utukufu wa Mungu.
Ayubu hakupoteza Imani yake katika Mungu, hata katika hali ngumu za kuvunja moyo ambazo zilimjaribu. "Tazama, ataniua; sina tumaini; ila hata hivyonitaithibitisha njia yangu mbele yake" (Ayubu 13:15). Ayubu alinyamazishwa na Mungu wakati alimsungumzia katika mawimbi. Ayubu alikiri kwamba alisungumza mambo ambayo hakuelewa, mambo yaliyo juu ya fahamu yake. "Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu" (Ayubu 42:6; angalia Ayubu 42:1-6). Kama Ayubu vile vile itikio letu kwa Mungu linafaa kuwa utiifu nyenyekevu and tumaini, kunyenyekea kwa mapenzi Yake, iwe tunaelewa au la.
Isaya alikuawa na maono ya Bwana akiwa ameketi enzini nay a malaika ambao walilia, "Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake" (Isaya 6:3). Maono haya yalikuwa mazito hadi Isaya akapasa sauti, "Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi" (Isaya 6:5; angalia pia Isaya 6:1-6). Isaya aligundua kwamba alikuwa mwenye dhambi mbele za Mungu Mtakatifu, na itikio lake lilikuwa toba. Maono ya Yohana ya kiti cha enzi cha Mungu mbinguni yalimtia ndani yake kumcha Mungu. Yohana alianguka chini kama mwenye amekufa chini ya miguu ya Bwana aliyeinuliwa (Ufunuo 1:17-18). Kama Isaya na Yohan, tunanyenyekea mbele za Ukuu wa Mungu.
Kunazo sifa zingine nyingi za Mungu ambazo zimefunuliwa katika Biblia. Uaminifu wa Mungu hutuongoza kuwa na tumaini kwake. Neema yake husababisha shukrani ndani yetu. Nguvu zake hujipusha mshangao ndani yetu. Ufahamu wake unatufanya kuuliza hekima (Yakobo 1:5). wale ambao wanamjua Mungu watatembea katika utakatifu na heshima.
English
Mkristo anapaswa kuitikia aje sifa za Mungu?