settings icon
share icon
Swali

Sifa za wazee na mashemasi ni gani?

Jibu


Bibilia ina sifa wazi za shemasi na mzee na nafasi zao katika mwili wa waumini. Afisi ya shemasi ilianzishwa ili kukabiliana na suala halisi katika kanisa: "Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani "(Matendo 6: 2). Neno lililotafsiriwa "kusubiri" ni neno la Kigiriki diakonein, ambalo linatokana na neno linalomaanisha "mtumishi, mhudumu, au anayehudumu kwa mwingine." Kuwa "shemasi" ni kutumikia. Mashemasi wa kwanza walikuwa kikundi cha wanaume saba katika kanisa la Yerusalemu ambao waliteuliwa kufanya kazi katika usambazaji wa kila siku wa chakula. Kwa hivyo, shemasi ni mmoja ambaye hutumikia wengine kwa uwezo rasmi katika kanisa.

Neno la Kigiriki linalotafsiriwa "Askofu" ni episkopos. Askofu ni msimamizi, mwangalizi, au afisa mtendaji kwa ujumla anayesimamia kongamano lote. Katika Bibilia Maaskofu pia huitwa "wazee" (1 Timotheo 5:19) na "wachungaji" (Waefeso 4:11).

Sifa za Askofu / Mzee / Mchungaji hupatikana katika 1 Timotheo 3: 1-7: "Ni neno la kuaminiwa: mtu akitaka kazi ya askofu, anatamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi. "Paulo pia anamwagiza Timotheo juu ya mambo ambayo yanaonyesha mafundisho ya muhudumu mzuri. Kuanzia 1 Timotheo 4:11 na kuendelea hadi 6: 2, Paulo anampa Timotheo vitu kumi na mbili ambavyo anapaswa 'kutoa amri na kufundisha.'

Mtume Paulo anarudia sifa za askofu / mzee / mchungaji katika barua yake kwa Tito. "ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii. Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu; bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake; akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga"(Tito 1: 6-9).

Sifa za shemasi ni sawa na zile za askofu / mzee / mchungaji. "Vivyo hivyo, mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu; wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika Imani iliyo katika Kristo Yesu "(1 Timotheo 3: 8-13). Neno lililotafsiriwa kuwa "shemasi" katika kifungu hiki ni aina ya neno la Kigiriki lililotumika katika Matendo 6: 2, kwa hivyo tunajua tunazungumzia afisi moja.

Sifa hizi ni rahisi na za moja kwa moja. Shemasi pamoja na askofu/mzee/mchungaji anapaswa kuwa mwanaume, mume wa mke mmoja, wa tabia mzuri, na mtu anayeongoza nyumba yake mwenyewe kwa njia ya kibiblia. Sifa hizi pia zinakusudia kwamba mtu anayetafuta afisi hiyo ni muumini aliyeokoka na anatembea katika utii wa Neno la Mungu. Tofauti kubwa kati ya hizi aina mbili za sifa ni kwamba askofu / mzee / mchungaji lazima awe "na uwezo wa kufundisha," ilhali mafundisho hayajatajwa kuwa lazima kwa mashemasi.

Bwana Yesu mwenyewe anaitwa "Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu" (1 Petro 2:25). Hivi vyeo ni vya kuvutia. Neno mchungaji ni tafsiri ya neno la Kigiriki poimen, lililotafsiriwa "muhubiri" mahali pengine (kwa mfano, Waefeso 4:11). Huyu Poimen ni mtu anayeongoza kundi la mifugo na ametumiwa kimajazi kama wachungaji wa Kikristo kwa sababu wachungaji wanapaswa kuongoza "kundi" la Mungu na kuwapa Neno la Mungu. Neno lililotafsiriwa "Mwangalizi" ni lile neno moja, episkopos, lililotumiwa na mtume Paulo katika 1 Timotheo na Tito.

Kwa wazi, afisi za mzee na shemasi ni muhimu katika kanisa. Kuwahudumia watu wa Mungu kwa neno na matendo ni jukumu kubwa kwa mtu kutekeleza, na halipaswi kufanywa kwa wepesi. Mtu asiyestahili kibiblia hapaswi kuchukua nafasi ya afisi ya mzee au shemasi; kanisa linastahili bora.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Sifa za wazee na mashemasi ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries