settings icon
share icon
Swali

Je! Mkristo anapaswa kuwa na kozi?

Jibu


Kozi ni kitu tunachofanya nje ya kazi yetu ya kawaida kwa furaha au kupumzika. Kwa mfano, huenda ikawa ni kutembea, useremala, kucheza chombo, kusoma, kucheza michezo, au mambo mengine mengi. Mungu anajua tunahitaji kupumzika mara kwa mara na kufurahi, lakini tunahitaji kuwa na furaha safi na ya kiungu, si furaha ya kidunia, ya dhambi. Kwa hiyo ni makosa kwa Wakristo kuwa na kozi? Si lazima. Mazoea mengi ya hati hati, yaneweza kuwa sahihi au si sahihi. Kitu muhimu ni mtazamo wa mtu anayehusika katika kozi.

Paulo aliandika hivi, "Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye" (Wakolosai 3:17). Pia aliandika, "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" (1 Wakorintho 10:31). Kigezo cha kweli cha kupima matamanio yetu kinapaswa kuwa kama kinavutia mawazo yetu kwa Mungu, au kutoa mawazo yetu kutoka kwa Mungu. Viburudisho vyetu vingi hii leo vina mizizi katika dhambi, vinaitukuza na kutimiza tamaa ya mwili na tamaa ya macho. Tunapaswa kuwa makini kwamba vitendo vyetu havina mizizi katika dhambi.

Kozi inaweza kuwa mabaya ikiwa tunakuwa nazo ili kutoroka kutoka kwa Mungu au kuwa na tabia mbaya. Tunaweza kushiriki katika michezo na kufurahia uhusiano ambao michezo hutoa. Lakini kama ushindani wetu unatufanya tulaani wakati tunapoteza au kucheza vibaya, ikiwa tunadanganya kwenye alama, au ikiwa tunaanza kuona wapinzani wetu kama adui, basi hiyo itakuwa mbaya na si kumtukuza Mungu. Michezo yenyewe sio mbaya, lakini ushiriki wetu ndani yao unaweza kuwa wa dhambi kwa sababu ya mtazamo wetu na mbinu yetu kwao. Lakini kama tunapenda kufurahia shughuli hizi kwa mtazamo wa shukrani kwa Mungu na kushiriki kwetu kwao hakupotezi uhusiano wetu na Yeye, basi michezo au kozi ni ya ushawishi mzuri katika maisha yetu.

Jaribio la kozi ni kuzitumia kama chombo cha kutoroka kutoka kwa maisha na kwa hiyo kutoka kwa Mungu. Zinaweza kutunyanganya wakati, kuwa sanamu katika maisha yetu, na kutuzuia kumtukuza Mungu katika kila kitu. Tuna uhuru wa kushangaza katika Kristo, lakini Paulo alitoa tahadhari hii: "Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo" (Wagalatia 5:13).

Tena, vitu vya kupendeza sio vibaya, lakini wakati vinatukua na kuchukua macho yetu mbali na Kristo, basi ni dhahiri kuwa ni mbaya. Hata vitendo visivyo na hatia ambavyo vinatughubika hivyo tunapaswa kuviweka kando kwa sababu vinatuzembeza katika mbio zetu, ambayo ni maisha ya Kikristo (Waebrania 12: 1). Mtihani mzuri ni huu: Je! Hili ni la umuhimu gani kwangu? Je! Bwana peke anatosha? Ikiwa imechukuliwa mbali na mimi, bado nitatosheka katika Kristo? Kwa hiyo, ndiyo, Wakristo wanaweza kuwa na kozi, lakini tunapaswa kuhakikisha kuwa hazijaweza kuchukua nafasi ya Kristo. Hilo ni jaribu, na lazima tuwe na uhakika wa kuepuka.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mkristo anapaswa kuwa na kozi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries