settings icon
share icon
Swali

Je! bado Shetani anaweza kufikia mbinguni?

Jibu


Mbeleni Shetani alikuwa mmoja wa malaika watakatifu wa Mungu, lakini aliasi dhidi ya Mungu na akatupwa kutoka mbinguni (Luka 10:18). Hilo ilikuwa hatua ya kwanza ya hukumu yake. Ufalme wa Shetani umeshindwa msalabani (Yohana 12: 31-32). Baadaye, atakuwa amefungwa kwa shimo kwa miaka elfu moja (Ufunuo 20: 1-3) na kisha atatupwa katika ziwa la moto milele (Ufunuo 20:10).

Hadi hukumu yake ya mwisho, Shetani ni "mkuu wa ulimwengu huu" (Yohana 14:30), lakini inaonekana kwamba bado ana ufikiaji mdogo wa maeneo ya mbinguni. Katika Ayubu 1: 6, Shetani anasimama mbele ya Mungu. Kuna hali kama hiyo katika 2 Mambo ya Nyakati 18: 18-21 inayohusisha "roho ya uongo."

Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu na hana dhambi yoyote (Isaya 6: 3), na kwa kuwa hatizami mabaya (Habakuki 1:13), Shetani anawezaje kuwa mbinguni? Jibu linahusisha kizuizi cha Mungu cha dhambi. Katika Ayubu 1, Shetani alisimama mbele ya Mungu ili kutoa akaunti yake mwenyewe. Mungu alianzisha mkutano, akaongoza mashtaka, na akaendelea kwa udhibiti kamili (mstari wa 7). Matokeo yake ni kwamba uwezo wa Shetani ulikuwa mdogo (mstari wa 12) na Mungu alitukuzwa.

Hapa kuna mambo mengine ya kumbuka: 1) Shetani hana fursa ya wazi mbele ya Mungu. Anaitwa na Mungu. 2) Ziara hiyo ni ya muda mfupi. Wakati wake mbele ya kiti cha enzi cha Mungu ni mdogo. 3) Kwa namna yoyote ile hakuna vile utakatifu wa mbinguni utaharibiwa na uwepo wa shetani mfupi, Mungu alimpangai mwovu kuwepo tangu mwanzo, "ametengwa/karantini", kama ilivyokuwa, kwa nguvu ya udhibiti wa Mungu. Na, 4) Ufikiaji wa Shetani hupewa tu kabla ya hukumu ya mwisho. Baada ya hukumu, Mungu huumba mbingu mpya na dunia mpya (Ufunuo 21: 1), hufuta machozi yote kutoka macho yetu (mstari wa 4), inafunua Yerusalemu Mpya (mstari wa 10), na unaahidi kuwa kamwe hakutakuwa na dhambi (mstari wa 27).

Tunaposema, "Mungu hawezi kuiruhusu dhambi mbinguni," chenye tunamaanisha ni kwamba Mungu hawezi kuruhusu wanadamu ambao bado wako katika dhambi zao kuishi katika uwepo Wake. Lakini inawezekana kwa Mungu kuamuru kiumbe mwenye dhambi kusimama (kwa muda) mbele yake ili ampatie kumwajibisha (Isaya 6), kutoa akaunti kutoka kwake (Ayubu 1-2), au kumhukumu (Ufunuo 20: 11-15) bila kuacha utakatifu wake.

Utakatifu wa Mungu hatimaye utameza dhambi zote. Mpaka siku hiyo, utakatifu wake unasimamia dhambi, na hiyo ina maana kwamba Shetani, wakati mwingine, anaitwa kifupi mbele ya Muumba wake kutoa hesabu ya matendo yake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! bado Shetani anaweza kufikia mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries