settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Shetani alidhani angeweza kumshinda Mungu?

Jibu


Ni vigumu kufikiria kiumbe kama Ibilisi (Shetani) akiamini angeweza hata kupigana vita na Mungu, hata kidogo kumshinda Yeye. Hata akili iliyoharibiwa zaidi inapaswa kuona kwamba kiumbe hakiwezi kushindana na Muumba. Hata hivyo Shetani alijaribu kuuzulu Mungu na anajitahidi hadi leo kukataa amri za Mungu, kuzuia mipango Yake, na kuwasumbua watu Wake.

Labda sehemu ya ufafanuzi ni kwamba kiburi kimemfumba Shetani kwa ukweli. Vifungu viwili vya Agano la Kale (Isaya 14:12-15 na Ezekieli 28:11-19) vinazungumzia nafasi ya kwanza ya Shetani na sababu za kupoteza kwake nafasi hiyo. Wanasema juu ya kiumbe malaika kilichoinuliwa, mmoja wa viumbe wa Mungu, ambaye alikuwa na kiburi. Aliamua kuchukua ufalme wa Mungu kwa ajili yake mwenyewe. Lakini Mungu alimwondoa kutoka nafasi yake.

Ushawishi wa Shetani katika mambo ya kidunia umefunuliwa wazi katika (Yohana 12:31). Shetani ni mwenye akili sana. Kupitia akili yake aliwadanganya Adamu na Hawa na akachukua utawala wa ulimwengu kwa ajili yake mwenyewe (Mwanzo 1:26; 3:1-7; 2 Wakorintho 11:3). Umahiri wake humwezesha kufanya kazi yake ya udanganyifu karibu kwa mapenzi, ingawa nguvu zake ni chini ya vikwazo vya Mungu (Ayubu 1:12, Luka 4:6, 2 Wathesalonike 2:7-8). Yeye ana ushindi fulani-ingawa ndani ya mipaka Mungu ameweka kwa ajili yake-na labda ushindi huo unamruhusu kuendelea na udanganyifu kwamba anaweza kuwa na ushindi juu ya Mungu Mwenyewe.

Udhibiti wa Mungu juu ya shughuli za Shetani unaonyeshwa na ombi la Shetani kwa Mungu kwa idhini ya kumtesa Ayubu (Ayubu 1:7-12). Shetani anaruhusiwa kutesa watu wa Mungu (Luka 13:16, 1 Wathesalonike 2:18; Waebrania 2:14), lakini haruhusiwi kushinda ushindi wa mwisho juu yao (Yohana 14:30-31; 16:33). Sehemu ya tamaa ya Shetani inayoendelea kuwa badala ya Mungu ni hamu yake ya kutamani kuwa na wengine kumwabudu yeye (Mathayo 4:8-9; Ufunuo 13:4, 12). Shetani ni "mwovu" (Mathayo 13:19, 38), ili hali Mungu ni "Mtakatifu" (Isaya 1:4).

Hali ya Shetani ni ovu. Jitihada zake katika kumpinga Mungu, watu Wake, na ukweli Wake ni zisiokwisha (Ayubu 1:7, 2:2; Mathayo 13:28). Yeye daima hupinga maslahi bora ya mwanadamu (1 Mambo ya Nyakati 21:1; Zakaria 3:1-2). Kupitia jukumu lake katika kuanzisha dhambi katika familia ya binadamu (Mwanzo 3), Shetani amepata nguvu za kifo-nguvu ambayo Kristo amevunja kupitia kusulubiwa na kufufuka Kwake (Waebrania 2:14-15). Shetani alimjaribu Kristo moja kwa moja, akijaribu kumwelekeza katika maafikiano kwa kumahidi mamlaka na nguvu ya kidunia (Luka 4:5-8).

Licha ya Shetani kujidanganya kwamba anaweza kumshinda Mungu, Shetani anatakiwa kushindwa. Kushindwa kwake wa mwisho unatabiriwa katika Yohana 12:31, Ufunuo 12:9, na 20:10. Kifo cha Kristo msalabani ni msingi wa kushindwa wa mwisho wa Shetani (Waebrania 2:14-15, 1 Petro 3:18, 22). Tukio hilo lilikuwa kilele kikubwa kwa maisha yasiyo na dhambi wakati Yesu alishinda juu ya adui mara kwa mara (Mathayo 4:1-11; Luka 4:1-13). Shetani pengine alifurahi katika kifo cha Kristo, akiamini kuwa itakuwa ushindi kwake, lakini kama ushindi wake wote, huo, pia, ulidumu kwa muda mfupi. Wakati Yesu alifufuka kutoka kaburini, Shetani alishindwa tena. Ushindi wa mwisho utakuja wakati Yesu atarudi na Shetani atatupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:1-15).

Kifo na ufufuo wa Kristo humpa nguvu muumini kwa ushindi juu ya dhambi. Tuna hakikisho kwamba "Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yako" (Warumi 16:20). Lakini ushindi huo wa kibinafsi hutegemea neema na nguvu ya Mungu katika maisha yetu na mapenzi yetu ya kutoa upinzani dhidi ya majaribu ya Shetani (Waefeso 4:25-27; Yakobo 4:7, 1 Petro 5:8-9). Ili kuwasaidia Wakristo kushinda vita hii dhidi ya Shetani, Mungu ametoa nguvu ya damu ya Kristo (Ufunuo 12:11), sala inayoendelea ya Kristo mbinguni kwa waumini (Waebrania 7:25), uongozi wa Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:16), na silaha mbalimbali kwa vita vya kiroho (Waefeso 6:10-18).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Shetani alidhani angeweza kumshinda Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries