settings icon
share icon
Swali

Je, Shetani yuko Jehanamu? Shetani yuko wapi?

Jibu


Kwa sasa, Shetani hako katika Jahanamu. Badala yake, Shetani huzunguka dunia, akitafuta watu kuwajaribu katika dhambi na hivyo kujitenga na Mungu. Waraka wa Kwanza wa Petro 5: 8 inasema, " Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze." Katika Yohana 14:30, Yesu alimwita Shetani "mkuu wa ulimwengu huu," na mtume Paulo akamtaja kuwa "mtawala wa ufalme wa hewa, roho ambaye sasa anafanya kazi kwa wale wasiotii" (Waefeso 2: 2). Shetani haishi katika Jahanamu; anaishi na kufanya kazi duniani na huku akizunguka mbinguni.

Shetani ni "baba wa uongo" (Yohana 8:44), na anaathiri na kuongoza ulimwengu wa sasa. Shetani anataka kuabudiwa (Mathayo 4: 9), na anatumia udanganyifu na vikwazo kuteka mwelekeo wa mwanadamu mwenyewe. Dunia inamwabudu Shetani kwa njia moja au nyingine, ila kwa wale ambao ni wa ufalme wa Mungu na kwa hiyo huitwa nje ya udanganyifu wa Ibilisi. Ikiwa mtu si mtoto wa Mungu, yeye ni mtoto mdogo wa Shetani (ona Yohana 8:44; Matendo 13:10). Waraka wa Kwanza wa Yohana 3:10 inatuambia jinsi ya kutofautisha wawili: "Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake." Yakobo 4: 4 anaelezea kwamba yeyote ambaye ni rafiki wa ulimwengu ni adui wa Mungu.

Hii ni muhimu kujua, kwa sababu hivi karibuni Yesu atarudi duniani na kukusanya kile ambacho ni chake Yeye. Yeye atawashinda wafuasi wa Shetani na kudai wateule Wake Mwenyewe. Hatimaye, Shetani atatupwa katika ziwa la moto na "atateswa mchana na usiku milele na milele" (Ufunuo 20:10). Baadaye, Yesu atawahukumu wasioamini kulingana na yale waliyoyafanya wakati wa maisha yao. Mtu yeyote ambaye jina lake halitapatikana limeandikwa katika Kitabu cha Uzima atatupwa katika ziwa la moto ambako Shetani na watoto wake watakuwa wakati huo (Ufunuo 20:13, 15). Jahanamu na kifo pia hutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:14), kwa hiyo, kwa kusema kitaalam, hakuna wakati wowote Shetani anaishi katika Jahanamu. Lakini atafungiwa na kudumu katika mahali pa moto sana ambayo inaweza kunaweza kaa kama "kuzumi hivi" mahali, atateswa milele.

Kitu muhimu cha kila mtu ni kuhakikisha jina lake limeandikwa katika Kitabu cha Uzima ili awe na uzima wa milele mbinguni, badala ya kutengwa milele na Mungu katika ziwa la moto.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Shetani yuko Jehanamu? Shetani yuko wapi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries