settings icon
share icon
Swali

Je! Shetani ana uwezo wa kudhibiti hali ya anga?

Jibu


Idadi kubwa ya majanga ya asili na dhoruba kali zimewashanga wengi huku wakijiuliza, je ni nani hudhibiti hali ya anga, Mungu au Shetani? Wengine huangazia maelezo ya Shetani kama "mkuu wa nguvu za anga" katika Waefeso 2: 2 na "mungu wa ulimwengu huu" katika 2 Wakorintho 4: 4 kama ushahidi wa Shetani kuwa na udhibiti wa hali ya anga. Uchunguzi wa Maandiko unafafanua kwamba ushawishi wowote wa Shetani na malaika wake wa pepo juu ya hali ya hewa unadhibitiwa na Mungu mwenye uwezo. Ibilisi, "adui" wetu, lazima alichukuliwe kwa uzito; tunapaswa kutambua kuwepo kwake na uwezo wake mdogo juu ya ulimwengu wa kidunia. Wakati huo huo, Shetani, malaika aliyeshindwa na aliyeanguka, ana nguvu lakini hana mamlaka, yeye ni mwenye uwezo tu ambao Mungu ataruhusu (2 Wathesalonike 2: 6-11).

Ikiwa Shetani angeweza kuathiri hali ya anga, ingekuwa tu kwa ruhusa ya Mungu, ambayo ina kipimo fulani, kama ilivyo katika Ayubu. Shetani aliruhusiwa na Mungu kumtesa Ayubu ili amjaribu, na hii ilijumuisha "moto wa Mungu" (pengine radi) ambao "ulianguka kutoka mbinguni ukachoma kondoo na watumishi" (Ayubu 1:16). Hii ilifutiliwa na "upepo mkali" (labda kimbunga) ambayo iliangamiza nyumba ya mwanawe mkubwa na kuua watoto wa Ayubu (mistari 18-19). Kwa hivyo ni kama moto kutoka mbinguni na kimbunga ilikua inasababishwa na Shetani, lakini bado ilikua chini ya udhibiti wa Mungu kwa madhumuni Yake.

Ni Mungu, wala sio Shetani, ambaye hudhibiti hali ya aga (Kutoka 9:29; Zaburi 135: 6-7; Yeremia 10:13).
Mungu anadhibiti mbingu na mvua (Zaburi 77: 16-19).
Mungu hudhibiti upepo (Marko 4: 35-41; Yeremia 51:16).
Mungu anashikilia na kuimarisha ulimwengu (Waebrania 1: 3).
Mungu ana nguvu juu ya mawingu (Ayubu 37: 11-12, 16).
Mungu ana nguvu juu ya radi(Zaburi 18:14).
Mungu ana nguvu juu ya asili yote (Ayubu 26).

Mungu ana udhibiti wa vitu vyote, ikiwa ni pamoja na hali ya anga. Kwa njia ya kukimu yake, Mungu hukimu na kulinda watoto wake, lakini pia anaruhusu Shetani, mapepo, na wanadamu kutekeleza mapenzi yao kwa kiwango fulani, kufanya vitendo vya dhambi, na uovu. Viumbe hivyo vinasababisha kwa majanga na maafa yote yanayopangwa na binadamu. Tunajua kwamba Mungu amekamilisha chochote kitakachofanyika (Waefeso 1:11, Warumi 11:36), na kwa hiyo mkono Wake usioonekana ni katika maumivu yetu, ingawa hawezi kutenda dhambi au kuwa mhalifu wa uovu (Yakobo 1: 13-17) ).

Hatuwezi kuwa na mateso isiyo na maana kwa mwamini, ikiwa mateso husababishwa na watu au kwa tukio la asili. Hatuwezi kujua kwa nini matendo maovu au maafa ya asili hutokea, lakini tunaweza kuwa na uhakika kwamba katika majaribu na mateso yetu yote Mungu anafanya kazi pamoja kwa ajili ya utukufu wake na kwa wema wetu wa milele (Waroma 8: 18-28).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Shetani ana uwezo wa kudhibiti hali ya anga?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries