settings icon
share icon
Swali

Sheria ya Kristo ni gani?

Jibu


Wagalatia 6: 2 inasema, "Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo" (msisitizo umeongezwa). Ni nini hasa sheria ya Kristo, na ni jinsi gani inatimizwa kwa kubebeanaa mzigo kila mmoja? Wakati sheria ya Kristo imetajwa pia katika 1 Wakorintho 9:21, Biblia haipo mahali ambapo inaelezea hasa ni sheria ya Kristo. Hata hivyo, walimu wengi wa Biblia wanaelewa sheria ya Kristo kuwa kile ambacho Kristo alisema kuwa amri kubwa zaidi katika Marko 12: 28-31, "..."Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye.'"

Sheria ya Kristo, basi, ni kumpenda Mungu kwa moyo wetu wote na kupenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe. Katika Marko 12: 32-33, mwandishi ambaye alimwuliza Yesu swali hili anajibu, "na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia." Katika hili, Yesu na mwandishi walikubaliana kwamba amri hizo mbili ni msingi wa sheria nzima ya Agano la Kale. Sheria yote ya Agano la Kale inaweza kuwekwa katika makundi ya "kumpenda Mungu" au "kumpenda jirani yako."

Maandiko mbalimbali ya Agano Jipya yanasema kwamba Yesu alitimiza Sheria ya Agano la Kale, na kuileta katika utimilifu na mwishowe (Warumi 10: 4; Wagalatia 3: 23-25; Waefeso 2:15). Badala ya Sheria ya Agano la Kale, Wakristo wanapaswa kutii sheria ya Kristo. Badala ya kujaribu kukumbuka amri za kibinadamu zaidi ya 600 katika sheria ya Agano la Kale, Wakristo wanafaa kuzingatia kumpenda Mungu na kuwapenda wengine. Ikiwa Wakristo wangeitii amri hizi mbili kwa kweli na kwa moyo wote, tutaweza kutimiza kila kitu ambacho Mungu anataka kwetu.

Kristo alitukomboa kutoka utumwa wa mamia ya amri katika Sheria ya Agano la Kale na badala yake anatusii tuwe na upendo. Waraka wa Kwanza wa Yohana 4: 7-8 inasema, "Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo." Waraka wa Kwanza wa Yohana 5: 3 inaendelea na kusema, "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito."

Wengine hutumia ukweli kwamba hatuko chini ya Sheria ya Agano la Kale kama sababu ya kutenda dhambi. Mtume Paulo anasema suala hili sana katika Warumi. "Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha!" (Warumi 6:15). Kwa mfuasi wa Kristo, kuepuka dhambi kutaafikiwa kutokana na upendo kwa Mungu na upendo kwa wengine. Tunafa kutiwa motisha na upendo. Tunapotambua thamani ya dhabihu Yesu alitoa kwa niaba yetu, itikio letu ni kuwa na upendo, shukrani, na utiifu. Tunapoelewa dhabihu ambayo Yesu alitufanyia sisi na wengine, majibu yetu ni kuwa kufuata mfano Wake katika kuonyesha upendo kwa wengine. Nia yetu ya kushinda dhambi inapaswa kuwa upendo, sio tamaa ya utii wa sheria kwa mfululizo wa amri. Tunapaswa kutii sheria ya Kristo kwa sababu tunampenda, sio eti tuweze kuangalia orodha ya amri ambazo tumetii kwa ufanisi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Sheria ya Kristo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries