settings icon
share icon
Swali

Je, ni sheria gani za uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme na zinawezaje kutoa ushahidi kwa uumbaji?

Jibu


Sheria za uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme zinahusika na umeme, nishati ya mitambo na ugeuzi kati yazo mbili. Utaratibu wote wa kimwili, wa kibayolojia na wa kemikali unaojulikana kwa mwanadamu ni chini ya sheria hizi. Sayansi mara nyingi huzungumzia sheria nne za uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme , lakini mbili tu zina uhusiano wa maana na imani ya Kikristo.

Sheria ya kwanza ya uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme, inayojulikana pia kama uhifadhi wa nishati, inasema, "Hakuna kitu kinachokuja kuwepo au kutoweka; kitu chochote kilicho na nafasi ardhini kinaweza kubadilishwa kuwa kitu tofauti, lakini hakuna kuongezeka kwa wavu kwa jumla ya kile kilichopo." ina maana kuwa, hata kama kitu chochote kinabadilishwa kuwa kitu tofauti, hakutakuwa na ongezeko au kupungua kwa Jumla.

Kwa hiyvo swali ni, ikiwa kitu chochote kilio na nafasi ardhini na nguvu za umeme haziumbwi wala haviwezi kuharibiwa, basi vitu vyote ulimwenguni na nguvu za umeme vilitoka wapi? Aidha (a) ulimwengu kwa namna fulani ulikuwepo bila ya Mungu, ingawa sayansi imethibitisha kuwa haiwezekani kitu fulani kutokea bila asili yoyote, (b) kila kitu kilikuwapo katika ulimwengu wote, wazo ambalo sayansi pia imeonenesha kuwa haiwezekani, au (c) Mungu aliiumba. Maelezo ya busara na ya kupendeza ni kwamba Mungu aliumba ulimwengu na kila kitu ndani yake.

Sheria ya pili ya uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme inasema kuwa enturopi ya mfumo wa kufungwa haiwezi kupungua: "Kila mfumo, ukiachwa kwa vifaa vyake, daima unaonekana kuhamia kutoka kwa utaratibu hadi kwa hali isiyo ya utaratibu, nguvu zake za umeme zikionekana kubadilishwa kuwa viwango vya chini vya upatikanaji (kwa kazi), hatimaye kuwa pungufu kwa kiasi kikubwa na kutopatikana kwa ajili ya kazi."Mwandishi na mwanasayansi Isaac Asimov alielezea," Ulimwengu unaendelea kukosa utaratibu! . . . hakuna ile tunayopaswa kufanya, na kila kitu huharibika, huanguka, huvunjika, huzeeka yenyewe tu-na hayo ndiyo sheria ya pili inahusu. "Kwa maneno mengine, baada ya muda, kila kitu huelekea kukosa utaratibu, bila mpangilio wowote, na kutokuwa na mwelekeo.

Mageuzi ya asili yanadai kwamba kila mfumo wa kimwili, kutoka kwa kiini kidogo kabisa mwilini hadi juu, ni matokeo ya mchakato ulio na mpangilio na utaratibu mzuri wa kusanyiko. Darwin alipendekeza kwamba viumbe hai, kwa mfano, vilikuja kwa njia ya uumbaji ulio na asili ndefu ya michakato ya milele, isiyo ya mpangilio.

Ingekuwa ulimwengu ni mfumo wa kufungwa kabisa, maendeleo hayo yangekuwa kinyume cha sheria ya pili ya uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme. Ni muhimu kutambua, hata hivyo, kwamba sayari yetu "haijafungwa," kwa upande wa uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme, hasa kwa sababu ya kupokea nishati kutoka kwa miale ya jua. Ambayo dhana kama mageuzi ya asili yanayotokana na sheria ya pili ya uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme ni kwa mtazamo wa jumla, kwa kiasi kikubwa.

Yanayojiri, kwa mujibu wa sheria hizi halisi, ni kwamba enturopi inaongezeka, na hivyo michakato ya asili inapaswa kuvunjika, si kujengeka (au kuingia katika kitu ngumu zaidi).

Uchunguzi rahisi unaonyesha ukweli wa sheria ya pili ya uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme. Rangi kwenye kuta na paa za nyumba. Vumbi hujenga. Nyumba yenyewe inaporomoka ikiwa hatua za kuzuia hazichukuliwi. Vyote vilivyo hai na hufa uoza kuharibika. Tunaweza kuona matokeo ya sheria ya pili ya uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme mbele ya macho yetu kila siku.

Mageuzi ya asili, hata hivyo, inahitaji zaidi ya mabadiliko rahisi katika enturopi. Mchakato huo sio sawa na kufungia maji kwenye furiji au kuunda fuwele za chumvi au vumbi kukusanya katika mfumo wa jua. Ili kugeuka kutoka yasiyo ya uzima, chochote kilicho na nafasi ardhini, lazima daima, mara kwa mara, na moja kwa moja lipigane dhidi ya nguvu ya enturopi. Hii inaweza kutokea kwa njia rahisi na kwa michakato rahisi katika mfumo wa wazi kama Dunia. Matukio kama hayo yanatokea kwa dakika, yanayohitaji makini, maalum, na imara hauonyeshi jinsi sheria hii inavyofanya kazi katika hali nyingine zote.

Sheria nyingine mbili za uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme hazina maana linapokuja maswali ya uumbaji. Sheria ya tatu inaonyesha kuwa enturopi inakaribia sifuri kama joto la kawaida linateremka hadi sifuri. Sheria ya nne mara nyingi huitwa "sheria ya sifuri" kwa kuwa ni ya msingi. Hii inaonyesha kuwa usawa wa uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme unahusisha; ikiwa mifumo miwili ipo katika usawa na mfumo wa tatu, pia ni sawa na kila mmoja yao.

Kwa wazi, maelezo rahisi, yenye busara zaidi ya sheria za fizikia ni uumbaji. Biblia inasisitiza uumbaji na Mungu mmoja wa kweli katika kitabu cha Mwanzo. Kwa nini wengine wanaamini mabadiliko ya asili badala ya uumbaji? Zaburi 14: 1 inamaliza ikisema hivi: "Mpumbavu husema moyoni mwake, 'Hakuna Mungu.'"

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni sheria gani za uhusiano kati ya aina zote za nguvu za umeme na zinawezaje kutoa ushahidi kwa uumbaji?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries