settings icon
share icon
Swali

Ni tofauti gani kati ya Sheol, Kuzimu, Jahannamu, ziwa la moto, Paradiso, na kifua cha Ibrahimu?

Jibu


Maneno tofauti yaliyotumiwa katika Biblia ya mbinguni na jahannamu-sheol, kuzimu, gehenna, ziwa la moto, paradiso, na kifua cha Ibrahimu-ni mada ya mijadala mingi na inaweza kuchanganya.

Neno "paradiso au peponi" linatumiwa kama kisawe cha "mbinguni" (2 Wakorintho 12: 4; Ufunuo 2: 7). Wakati Yesu alipokuwa akifa msalabani na mmoja wa wezi waliyesulibiwa pamoja Naye msalabani akamwomba huruma, Yesu akajibu, "Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja name peponi" (Luka 23:43). Yesu alijua kwamba kifo chake kilikuwa karibu na kwamba hivi karibuni atakuwa mbinguni na Baba yake. Yesu alizungumza juu ya peponi kama kisawe cha "mbinguni," na neno limekuja kuhusishwa na mahali popote pa upendo wa kweli na kufurahisha.

Kifua cha Ibrahimu kinarejelewa mara moja tu katika Biblia-katika hadithi ya Lazaro na tajiri (Luka 16: 19-31). Lilikuwa limetumika katika Buku la Sheria na Maadili ya Kiyahudi kama kisawe cha "mbinguni." Picha katika hadithi ni ya Lazaro akijinyoosha kwa meza akiegemea kifua cha Ibrahimu – kama vile Yohana alivyoegemea kifua cha Yesu kwenye Mlo wa Mwisho-katika karamu ya mbinguni. Kuna maoni tofauti kuhusu nini hasa kifua cha Ibrahimu kinawakilisha. Wale ambao wanaamini utunzi wa hadithi ni kipindi baada ya kifo cha Masihi na ufufuo wanaona kifua cha Ibrahimu kama kisawe cha "mbinguni." Wale wanaoamini utunzi ni kabla ya kusulubiwa wanaona "kifua cha Ibrahimu" kama neno lingine la "peponi." Utunzi kwa hakika haihusu hoja ya hadithi, ambayo ni kwamba watu waovu wataona wenye haki katika furaha na wao wenyewe katika mateso, na kwamba "ghuba kubwa" ipo kati yao (Luka 16:26), ambayo haiwezi kamwe kushubiri.

Katika Maandiko ya Kiebrania, neno linalotumiwa kuelezea eneo la wafu ni sheol. Linamaanishaa tu "mahali pa wafu" au "mahali pa mioyo/roho zilizoondoka." Neno la Kigiriki la Agano Jipya ambalo linatumika kwa "jahannamu" ni kuzimu, ambalo pia linamaanisha "mahali pa wafu." Neno la Kigiriki gehenna linatumiwa pia katika Agano Jipya kwa "jahannamu" na linatokana na neno la Kiebrania hinnom. Maandiko mengine katika Agano Jipya yanaonyesha kwamba sheol / kuzimu ni mahali pa muda ambapo roho za wasioamini huhifadhiwa wakati wanasubiri ufufuo wa mwisho na hukumu katika hukumu Kuu ya kiti cha Enzi Cheupe. Roho ya wenye haki huenda moja kwa moja mbele ya Mungu-mbinguni / peponi / kifua cha Ibrahimu-wakati wa kifo (Luka 23:43, 2 Wakorintho 5: 8; Wafilipi 1:23).

Ziwa la moto, linatajwa tu katika Ufunuo 19:20 na 20:10, 14-15, ni jahannamu ya mwisho, mahali pa adhabu ya milele kwa waasi wote wasio na toba, wote malaika na wanadamu (Mathayo 25:41). Inaelezewa kuwa ni mahali pa kuchoma salfa, na wale wanalio ndani yake hupata uchungu usiopunguka wa milele, usiosemekana wa asili (Luka 16:24; Marko 9: 45-46). Wale ambao wamemkataa Kristo na wako katika makao ya muda ya wafu katika kuzimu/Sheol wana ziwa la moto kama makusudio yao ya mwisho.

Lakini wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo hawapaswi kuogopa hatma hii mbaya. Kwa imani katika Kristo na damu Yake iliyomwagika juu ya msalaba kwa ajili ya dhambi zetu, tumekusudiwa kuishi milele mbele ya Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni tofauti gani kati ya Sheol, Kuzimu, Jahannamu, ziwa la moto, Paradiso, na kifua cha Ibrahimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries