settings icon
share icon
Swali

Je! Mtu ambaye hajaoa anaweza kuwa shemasi au mzee wa kanisa?

Jibu


Vifungu vinavyohusiana sifa za mzee au shemasi kanisani ni 1 Timotheo 3:2, "Basi, imempasa mwangalizi awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha"; na Tito 1: 6-7 ".. Mzee wa kanisa asiwe na lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu ambaye watoto wake ni waaminio na wala hawashtakiwi kwa ufisadi. Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali ..."

Vifungu hivi vitatu vimetafsiriwa na wengine kuwa mzee au shemasi lazima awe mtu aliyeolewa.

Suala sio hali ya ndoa ya mzee au shemasi, bali maadili na utakatifu wa ngono. Sifa hii inaongoza orodha, kwa sababu ni katika eneo hili ambapo viongozi wengi wanajaribiwa na kuanguka. Wengine huchukua sifa ya mashemasi "shemasi awe mume wa mke mmoja" katika 1 Timotheo 3:12 kamaanisha kwamba ili mtu awe shemasi, lazima awe ameoa. Hii sio maana ya "mume wa mke mmoja." Kwa Kiyunani, kifungu "mume wa mke mmoja" hawa inasomeka "mwanamke mmoja kwa mwanamume." Iili mwanamume azingatiwe kwa nafasi ya uongozi kanisani, na ameoa, lazima ajitoe kwa mke wake. Sifa hii inazungumzia uzinzi katika ndoa na usafi wa kijinsia. Sio sharti la ndoa. Basi ingekuwa kwamba, ni lazima mwanamume aoe na pia awe na watoto, kwa sababu nusu ya pili ya 1 Timotheo 3:12 inasema, "kusimamia watoto wake na watu wa nyumbani mwake vyema." Tunapaswa kuelewa sifa hii kuwa: Ikiwa mwanamume ameoa, lazima awe mwaminifu kwa mke wake. Ikiwa mtu ana watoto, lazima awasimamie vyema.

Wengine wanafikiri kuwa sharti hili linawaondoa wanaume kapera kutoka kwa uongozi wa kanisa. Basi ikiwa hiyo ndiyo ilikuwa nia ya Paulo, angejiondoa mwenyewe (1 Kor. 7: 8). "Mwanamume wa mke mmoja" ni mtu aliyejitolea kabisa kwa mkewe, kudumisha kujitolea kwa mmoja, mapenzi na usafi wa kijinsia katika mawazo na matendo. Kukiuka sifa hii ni kupoteza kutokuwa na lawama na hivyo hawezi kuwa "bila lawama" (Tito 1: 6,7). Kuwa mseja kunasifiwa na Mtume Paulo kwa sababu kunawezesha huduma ya uaminifu zaidi kwa Bwana (1 Wakorintho 7: 32-35). Je! Ni kwa nini Paulo awazuie wanaume kutoka kwa nafasi za uongozi wa kanisa wakati anaamini kwamba "mwanaume ambaye hajaoa anajishughulisha na mambo ya Bwana, jinsi ya kumpendeza Bwana." (1 Wakorintho 7:32)? Katika mistari tisa ya kwanza ya sura hii, Paulo anakauli kwamba wote wanandoa na waseja ni wema na sawa mbele za Bwana. Mzee au shemasi anaweza kuwa ameoa au hajaoa, maadamu anatimiza sifa za utauwa zilizoainishwa katika 1 Timotheo na Tito.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mtu ambaye hajaoa anaweza kuwa shemasi au mzee wa kanisa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries