settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kutambua satui ya Mungu?

Jibu


Swali hili limekuwa likiulizwa na watu wasiowezahesabika katika vizazi vingi. Samweli aliisikia sauti ya Mungu, lakini hakuitambua hadi alipoamuriwa na Eli (Samweli 3: 1-10). Gideoni alikuwa na ufunuo halisi kutoka kwa Mungu, na bado akashuku chenye alikua amekisikia kwa kiwango anauliza ishara, sio mara moja bali ni mara tatu (Waamuzi 6:17-22, 36-40). Wakati tunaisikiza sauti ya Mungu, tutawezaje kujua ni yeye anazungumza? Mwanzo wa yote tuko na kitu ambacho Gideoni na Samweli ambacho hawakuwa nacho. Tuko na Bibilia iliyo kamilika, iliyo na pumzi ya Mungu, tusome, tujifunze, na kulitafakari. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2 Timotheo 3:16-17). Wakati tuko na swali kuhusu somo fulani au uamuzi katika maisha yetu, tuakikishe kuwa Bibilia inasema nini kuhusu hilo swali. Mungu hawezi kutuongoza, au kutuelekeza kinyume na chenye amefunza au ameahidi katika neno lake (Tito 1:2).

Pili, ili tusikie satu ya Mungu lazima tuitambue. Yesu alisema, “Kondoo wangu waisikia satu yangu; nami nawajua, nao wanifuata” (Yohana 10:27). Wale waisikiao sauti ya Mungu ni wale ambao ni wake- wale ambao wameokolewa kwa neema yake kupitia kwa imani katika Kristo Yesu. Hawa ndio kondoo ambao wanaisikia na kuitambua sauti yake, kwa sababu wanamjua kama mchungaji wao na wanaijua sauti yake. Kama tunataka kuitambua sauti yake, lazima tuje kwake.

Tatu, tunasikia sauti yake wakati tunachukua muda wetu katika maombi, kujifunza na kutafakari neno lake. Tunapochukua muda wetu na Mungu na neno lake, ndivyo inavyokuwa rahisi kuitambua sauti yake na uongozi wake katika maisha yetu. Waajiriwa katika benki huwa wanafundishwa jinsi ya kutambua noti pandia kwa kuichungulia noti kwa makini sana hadi wanatambua ile pandia. Pia lazima tulijue neno la Mungu ili anaponena nasi na kutuongoza, iwe wazi ni Mungu anafanya hivyo. Mungu hunena nasi ili tuuelewe ukweli. Mungu anaweza nena kwa sauti na watu, hasa hunena kupitia kwa neno lake na wakati mwingine kupitia kwa Roho Mtakatifu kwa akili yetu, kupitia kwa hali, na kupitia watu wengine. Kwa kukitumia katika maisha chenye tunasikia kutoka kwa maandiko, tunaweza kuitambua sauti yake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kutambua satui ya Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries