settings icon
share icon
Swali

Je! Sanda la Turin ni halisi?

Jibu


Sanda la Turin ni nguo ya kitani ambayo wengine wanaamini kuwa ni nguo ambayo Yesu Kristo alizikwa ndani. Kila kitabu cha Injili nne inasema Yesu alifungwa na kuzikwa katika kitambaa (Mathayo 27:59, Marko 15:46, Luka 23:53, Yohana 19:40). Sanda la Turin "iligunduliwa," au angalau kufanywa kwa umma, katika karne ya 14 A.D. Sanda la Turin inaitwa kwa jina la mji ambao limehifadhiwa huko Turin, Italia.

Hapa ni ukurasa wa wavuti ambao una baadhi ya picha/sanamu ya Sanda la Turin: http://www.shroud.com/examine.htm. Baada ya kuchunguza, Sanda la Turin inaonekana kuwa ya mtu ambaye alikuwa amesulubishwa. Kuna alama katika mikono na miguu ambayo ni sawa na majeraha yaliyotokana na kusulubiwa. Pia kunaonekana kuwa na majeraha sawa na yaliyotajwa katika mateso ya Yesu, karibu na kichwa, mgongo, na miguu.

Je! Sanda la Turin kweli ni nguo Yesu Kristo alizikwa ndani? Kuna mijadala mingi juu ya uhalisi wa Sanda la Turin. Wengine wameridhika kabisa kwamba ni nguo ya mazishi ya Kristo. Wengine wanaamini kwa ubunifu au kazi ya sanaa. Kumekuwa na vipimo vya tangu kwamba tarehe ya Sanda ya Turin hadi karne ya 10 K.K. au baadaye. Vipimo vingine vimegundua vijimbegu/vyavua ambavyo ni vya kawaida kwa Israeli na ambavyo vinaweza rejea kipindi cha karne ya kwanza A.D. Lakini hakuna tarehe kamili namna yoyote.

Kujadili dhidi ya uhalisi wa Sanda la Turin ni ukosefu kabisa wa ushahidi wa Biblia kwa sanda kama hiyo ya mazishi. Kama ilivyoelezwa hapo awali, Biblia inasema kipande kinzima cha kitani kilichotumiwa kuchukua mwili wa Yesu kutoka msalabani. Kitani hiki labda kilitumika pia kusafirisha mwili kwa Yosefu wa Arimathaya karibu na kaburi. Katika kaburi maandalizi ya haraka kwa mazishi yalifanywa; haya ingekuwa ni pamoja na kuosha mwili na kuufunga tena. Luka 24:12 inataja "vitambaa vya sanda." Vitambaaa vivi hivi (wingi) vimetajwa mara mbili katika Yohana 20:5-6. Na Yohana 20:7 inasema kulikuwa na "ile leso iliyokuwako kichwani pake." Maelezo haya ya nguo halisi ya mazishi- "vitambaa" vya kitani, badala ya kitambaa kimoja kikubwa; na kitambaa tofauti cha kufunika kichwa-inaonekana kukanusha madai ya kwamba Sanda la Turin ni Sanda la Kristo kwa mazishi.

Kwa hivyo, tunastahili kufanya nini kwa Sanda la Turin? Inawezekana lilikuwa sanda la mazishi kwa baadhi ya mtu aliosulubiwa, lakini inawezekana haikuwa na uhusiano wowote na kifo cha Kristo. Hata kama ilikuwa nguo halisi ya mazishi ya Kristo, Sanda la Turin haipaswi kuabudiwa au kusujudiwa. Kwa sababu ya hali ya shaka ya Sanda la Turin, haiwezi kutumika kama ushahidi kwa ufufuo wa Kristo. Imani yetu haitegemei Sanda la Turin bali kwa Neno la Mungu lililoandikwa.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Sanda la Turin ni halisi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries