settings icon
share icon
Swali

Ni aina gani ya sala tunapaswa kuomba kwa wasioamini?

Jibu


Tunaweza kujifunza jinsi ya kuombea wasioamini kwa mfano wa maombi ambao Yesu aliomba. Yohana 17 ni sala ya Yesu ndefu zaidi na inatuonyesha jinsi alivyoomba. Mstari wa 3 unasema, " Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma." Aliomba kwamba watu wamjue Mungu Baba. Na njia ambayo wangeweza kumjua Mungu ni kupitia Kristo Mwana (Yohana 14: 6; 3: 15-18). Ikiwa hivi ndivyo Yesu alivyopendelea, tunajua ni sahihi wakati tunapoomba sawia. Sala yoyote ambayo inakubaliana na Mungu ni sala yenye ufanisi (1 Yohana 5:14; Yakobo 5:16).

Petro wa pili 3: 9 pia inatupa mtazamo wa Mungu kwa wasioamini. Inasema, " Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. " Sio mapenzi ya Mungu kwamba mtu yeyote awe mbali na uwepo Wake milele (Waroma 6:23). Tunapoomba toba katika maisha ya wasioamini, tunakubaliana na Mungu. Tunaweza pia kuomba fursa ya kutumika kuwa mikono na miguu ya Yesu ili watu waweze kujua wema Wake (Wagalatia 6:10; Wakolosai 4: 5; Waefeso 5: 15-16). Tunaweza kuomba ujasiri, kama mitume walivyofanya, kwa kuchukua nafasi hizo wakati Mungu anawafanya wawepo (Matendo 4:13, 29; Waefeso 6:19).

Tunaweza pia kuomba kwamba Mungu atatengeneza hali yoyote ambayo ni muhimu ili kugeuza mioyo ya ukaidi kuelekea toba. Zaburi ya 119: 67 inasema, " Kabla sijateswa mimi nilipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako." Mara nyingi huchukua hali mbaya sana kujongea kwake Kristo. Tunapowaombea wapendwa ambao hawajui Yesu, pia tunajaribiwa kumwomba Mungu ulinzi na baraka. Hata hivyo, wakati mwingine ni muhimu kuomba kinyume na hayo ikiwa itasababisha kuvunja ibada ya sanamu maishani yao. Faraja, tamaa za kimwili, usherati, na ulevi ni miungu ya uongo ambayo huweka wasioamini katika utumwa. Kuomba mapenzi ya Mungu yetendeke kunaweza kuhitaji kumwomba aondoe ulinzi na faraja yake ili kuwasukuma mahali ambapo wanapaswa kumtafuta Mungu. Hakuna kitu muhimu zaidi kwa wapendwa wetu wasiookolewa kuliko kwamba wamtafute Mungu na kumpata.

Kuombea wengine hupendeza Mungu (1 Timotheo 2: 1-4). Ni njia moja tunayoonyesha upendo kwa watu wengine (1 Yohana 4: 7). Hata wakati hatujui jinsi ya kuomba, tunaweza kupata faraja katika ahadi ya Warumi 8:26. Mungu anajua hatujui nini cha kuomba kila wakati. Yeye amemtuma Roho Mtakatifu kutuombea ili tamaa za mioyo yetu zipelekwe kwenye chumba cha enzi cha mbinguni.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni aina gani ya sala tunapaswa kuomba kwa wasioamini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries