settings icon
share icon
Swali

Safari ya kiroho ni nini?

Jibu


Safari ya kiroho ni maneno yanayotumiwa na dini mbalimbali kwa kumaanisha maendeleo ya asili ya mtu kama anavyokua katika ufahamu wa Mungu, ulimwengu, na yeye mwenyewe. Ni maisha ya makusudi ya kukua zaidi katika ufahamu na hekima. Lakini safari ya kiroho kuelekea Ukristo ni tofauti kabisa na safari kuelekea aina fulani ya "kiroho" ambayo haijumuishi, au msingi wake hauko katika Mtu na kazi ya Bwana Yesu Kristo.

Kuna tofauti nyingi kati ya safari ya Kikristo ya kiroho na toleo la kizazi kipya. Kizazi kipya huyasema mafundisho ya dini kwa saa kadhaa kwa siku. Biblia inazungumzia kuwa na mazungumzo ya kila siku na Mungu kupitia sala (1 Wathesalonike 5:17).Kiizazi kipya wanaamini kuwa watu wanaweza kuchagua njia yao wenyewe katika safari yao na kwamba njia zote zinaongoza mahala sawa. Biblia inasema kuwa kuna njia moja tu-Kristo (Yohana 14: 6).Kizazi kipya wanaamini kuwa safari ya kiroho inasababisha upatanisho na ulimwengu. Biblia inafundisha kwamba ulimwengu u katika vita (Waefeso 6:12) na sehemu ya safari ni kupigana kwa ajili ya mioyo zingine na mienendo yetu (1 Timotheo 6:12).

Tofauti nyingine ni kwamba Biblia inazungumzia safari ya kiroho na hatua zinazohitajika. Mkristo anaanza kama mtoto (1 Wakorintho 13:11), bado anatazama ulimwengu kwa njia ya macho yasiyo na msimamo, bado ameshawishiwa na mwili, na anahitaji elimu ya msingi kuhusu Mungu na nafasi yao na Mungu (1 Wakorintho 3: 1-2; 1 Petro 2: 2). Na Wakristo wapya hupewa kazi katika kanisa inayofaa nafasi yao kama wachanga katika imani (1 Timotheo 3: 6). Wakristo wanapokua katika kumfahamu Mungu na ulimwengu, wanajifunza zaidi juu ya jinsi ya kutenda na jinsi ya kushirikiana na ulimwengu (Tito 2: 5-8). Mtu aliyekua katika safari yake ya kiroho anakuwa mfano kwa wale wachanga kiroho (Tito 2: 3-4) na, wakati mwingine, kiongozi katika kanisa (1 Timotheo 3).

Ni muhimu kufahamu kwamba ni safari. Hakuna hata mmoja wetu aliye mkamilifu. Mara tunapokuwa waumini, hatutarajiwi kufikia ukomavu wa kiroho. Badala yake, maisha ya Kikristo ni mchakato unaohusisha fikra zetu(2 Wakorintho 7: 1) na kazi ya Mungu ndani yetu (Wafilipi 1: 6; 2: 12-13). Na ina hitaji fursa na makusudi yetu wala sio umri (1 Timotheo 4:12).

Safari ya kiroho iliyojhusisha kuyasema mafundisho tu husababisha moyo usio na kitu. Safari inayohusisha kujifunza Biblia, kutii yale inachosema, na kumwamini Mungu ni safari ya maisha ambayo itasababisha kufahamu ulimwengu na upendo wa kina kwa Muumba wake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Safari ya kiroho ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries