settings icon
share icon
Swali

Ni nini roho ya mpinga Kristo?

Jibu


Kifungu roho ya mpinga Kristo kinapatikana katika 1 yohana 4:2-3: “Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. 3 Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.”

Ni muhimu kuelewa muktadha wa maneno ya Yohana. Mtazamo uliokuwa na maarufu juu zingine wakati aliandika barua hii ulipendekeza kwamba roho tofauti tofauti zilikuwa kazi duniani. Mafundisho mengi ya uongo, dini za ajabu, uzoefu wa kiroho, na Ukristo tofauti ulikuwa unajitokeza kwa wakati huo. Anga ya kiroho haikuwa tofauti na ile ya kisasa katika ulimwengu wetu leo. Watu walipendelea maoni kadhaa kuhusu ukweli.

Yohana aliwasilisha suluhisho kamili kwa kuogelea imani hizi tofauti na mafundisho. Aliwaelekeza wasomaji wake kuwa makini na kujaribu roho: “Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni” (1 Yohana 4:1).

Lakini tutazijaribuje roho? Je, tunawezaje kutambua walimu wanotoa ukweli? Je, tunawezaje kutambua roho ya mpinga Kristo?

Hizi “roho” Yohana aliongelea hazikuwa tu viumbe visivyo vya kawaida, visivyokuwa na mwili. Yohana alifundisha kwamba nabii au mwalimu ndiye sauti kamili wa roho. Mafundisho ya kiroho yanatangazwa kupitia msemaji wa kibinadamu. Walimu wa ukweli wamejazwa na Roho wa Mungu na kwa hivyo ni wakala ambao wananena kwa niaba ya Mungu. Walimu wa uongo wanaeneza “mfundisho ya mapepo” (1 Timotheo 4:1).

Kwa hivyo, jaribio la kwanza linahusiana na theolojia au mafundisho: “Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu” (1 Yohana 4:2). Tunaweza uliza, Je!, maudhui ya mtu anayefundisha yanakiri kwamba Yesu Kristo- Mungu kamili na binadamu kamili- amekuja katika mwili? Ikiwa jibu ni ndio, basi tunajua Roho wa Mungu alimtia moyo huyo mtu. Ikiwa sio hivyo, mafundisho yake yote yangekataliwa. Jaribio hili maalumu lilikuwa la kufaa hasa katika yakati za Yohana, kwa vile uzushi wa Ugnostiki ulikuwa umeenea; Ugnostiki ulifundisha kwamba Yesu alionekana tu kuwa na mwili wa binadamu lakini hakuwa mtu mwenye mwili na damu hasa.

Baadaye, Yohana anasema, “Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni” (1 Yohana 4:3). Yeyote ambaye hamkiri Yesu Kristo jinsi Biblia inavyomwakilisha Yeye ametiwa moyo na roho ya mpinga Kristo.

Neno mpinga Kristo linamaanisha “kinyume na Kristo.” Watu ambao wanasema Yesu hatoki kwa Mungu wanathibitiwa na roho ya mpinga Kristo. Shetani anampinga Kristo, na matumaini yake ni kudanganya watu kupitia mtazamo wa uongo kuhusu Yesu ni nani. Roho wa mpinga Kristo inafundisha kinyume na Kristo. Kugeuza ukweli kuhusu Yesu Kristo ni kuzuia injili. Shetani anafanya kazi kueneza uongo kuhusu Kristo na kuweka watu katika giza: “Wadanganyifu wengi, wasiokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili, wametokea ulimwenguni. Mtu wa namna hiyo ni mdanganyifu na mpinga Kristo” (2 Yohana 1:7).

Roho ya mpinga Kristo ni ndege ambao wanakula mbegu njiani katika mfano wa Yesu (Mariko 4:4, 15). “mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu” (2 Wakorintho 4;4). Ni “baba yenu Ibilisi” (Yohana 8:44). Roho ya mpinga Kristo ni “yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi… aupotoshaye ulimwengu wote.” (Ufunuo wa Yohana 12:9).

Biblia inafundisha ya kwamba hatimaye dunia itatoa mtawala, aitwaye “joka” katika Ufunuo wa Yohana, ambaye atatumia nguvu mingi sana na kuhitaji ibada kwa yeye mwenyewe. Naye atakuwa na “akapewa kusema maneno ya kiburi na kukufuru na kutumia” (Ufunuo wa Yohana 13:5) na amewezeshwa na Shetani (Ufunuo wa Yohana 13:2). Anaitwa “yule mtu wa kuasi … amehukumiwa kuangamizwa kabisa” (2 Wathesalonike 2:3). Hii kupinga ya mwisho atakuwa kilele ya kazi ya uovu wa Shetani kwa karne nyingi. Mpinga Kristo wa nyakati za mwisho atajumuisha udanganyifu na upotoshaji wote wa ukweli kwamba roho wa mpinga Kristo umekuwa ukikuzwa wakati wote. “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi” (2 Wathesalonike2:7). Roho ile ile ambayo itawezesha Mpinga Kristo wa nyakati za mwisho kwa sasa nafanya kazi duniani kuleta mchanganyiko na kudanganywa kwa swala la Yesu Kristo kama mtu na kazi yake. “Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni” (1 Yohana 4:3).

Hata kupewa athiri iliyoenea ya roho ya mpinga Kristo, hakuna haja ya kuogopa. Kwa vile Yohana anatukumbusha, roho wa ukweli anakaa ndani ya waumini wote na anatoa ulizi kutokana na roho ya mpinga Kristo: “Watoto wapendwa, ninyi mmetokana na Mungu, nanyi mmewashinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu” (1 Yohana 4:4).

Tuna njia za wazi za kutofautisha roho wa uongo wa mpinga Kristo kutoka kwa Roho wa kweli wa Mungu: “Wao wanatokana na ulimwengu na kwa hiyo hunena yaliyo ya ulimwengu, hivyo ulimwengu huwasikiliza. Sisi twatokana na Mungu na yeyote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu” (1 Yohana 4:5-6). Wale wanaathiriwa na roho ya mpinga Kristo ni wa dunia. Wana maadili sawa na ya dunia; kwa hivyo, dunia huwasikiza. Wale ambao umkiri Kristo wana Roho Wake wa kweli, na wanakumbatia ujumbe wa mitume. Injili mitume walihubiri haikuwa maarufu katika dunia, lakini hiyo injili ndiyo inashikilia nguvu ya kuokoa, kupitia Roho wa kweli wa Mungu (Warumi 1:16).

Kazi ya muumini ni kujaribu roho kwa makini (1 Yohana 4:1). “Tazama, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo mwe werevu kama nyoka na wapole kama hua” (Mathayo 10:16). Hatustahili kukumbatia ujumbe wa mhubiri au mwalimu yeyote moja kwa moja kwa sababu ya sifa au masomo yake; badala yake, tusikize ukristo wao kwa tahadhari. Wanachosema kuhusu Yesu ni cha muhimu Zaidi.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini roho ya mpinga Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries