settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu alituma roho mbaya kumsumbua Mfalme Sauli?

Jibu


"Basi Roho wa Bwana alikuwa amemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua" (1 Samweli 16:14). Hii pia imetajwa katika 1 Samweli 16: 15-16, 23:18, 10 na 19: 9. Mungu alimtuma "roho mbaya" ya pepo kumsumbua Sauli. Sauli alikosa kumtii Mungu mara mbili (1 Samweli 13: 1-14; 15: 1-35). Kwa hiyo, Mungu aliondoa Roho Wake kutoka kwa Sauli na kuruhusu roho mbaya kumsumbua. Inawezekana, Shetani na mapepo walikuwa wakitaka kumshambulia Sauli, Mungu alikuwa akiwapa ruhusa ya kufanya hivyo.

Jambo hili linazua swali linalohusiana-je, Mungu hutuma roho mbaya kusumbua watu leo? Kuna mifano ya watu binafsi katika Agano Jipya waliosalimishwa kwa Shetani au mapepo kama adhabu. Mungu aliruhusu Anania na Safira kujazwa na roho ya Shetani kama onyo na mfano kwa kanisa la kwanza (Matendo 5: 1-11). Mshirika wa Kanisa la Wakorintho alifanya uzinzi na usherati, na Mungu aliwaagiza viongozi "kumpeana kwa Shetani" ili kuharibu hali yake ya dhambi na kuokoa nafsi yake (1 Wakorintho 5: 1-5). Yesu aliongozwa na Roho kwenda jangwani ili kujaribiwa na shetani (Mathayo 4: 1-11). Mungu pia alimruhusu mjumbe wa Shetani kumtesa Mtume Paulo ili kumfundisha kutegemea neema ya Mungu na nguvu na kutojivunia kwa sababu ya wingi mkubwa wa kweli ya kiroho aliyopewa (2 Wakorintho 12: 7).

Ikiwa Mungu anaruhusu roho mbaya kuwasumbua watu leo, anafanya hivyo kwa lengo la wema wetu na utukufu Wake (Waroma 8:28). Hata kama pepo ni mbaya, bado imo chini ya udhibiti na ukuu wa Mungu. Kama ilivyo katika majaribu ya Ayubu, Shetani na wajumbe wake wanaweza kufanya tu kile ambacho Mungu anawaacha wafanye (Ayubu 1:12; 2: 6). Hawana kamwe kujitegemea kwa mapenzi na madhumuni kamili ya Mungu na madhumuni yake. Ikiwa waumini wanadai kuwa wanateswa na nguvu za pepo, jibu la kwanza ni kutubu dhambi yoyote inayojulikana. Kisha tunapaswa kuomba hekima ya kuelewa kile tunachojifunza kutokana na hali hiyo. Kisha tunapaswa kujisalimisha kwa chochote ambacho Mungu ameruhusu katika maisha yetu, na kuamini kwamba itasababisha kuimarisha imani yetu na utukufu wa Mungu.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu alituma roho mbaya kumsumbua Mfalme Sauli?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries