settings icon
share icon
Swali

Je! Rastafariani ni nini?

Jibu


Neno Rastafariani mara nyingi inaleta picha ya shungi la nywele (msuko ndefu au msuko wa nywele za asili), ganja (bangi), mitaa ya Kingston, Jamaica, na mdundo wa rege ya Bob Marley. Rastafarians hawana viongozi wanaojulikana ulimwengu wote, wala hakuna kanuni za ulimwengu za kufafanua. Ni harakati ya fahamu ya weusi--Afro-Caribbean-na kuna mgawanyiko kati ya dini na kuambatana na ufahamu wake wa kijamii, hivyo watu wanaweza kufahamu kile Rastas wanajaribu kufanya kijamii ingawa hawakubali dini.

Harakati huchukua jina lake kutoka kwa mada "Ras Tafari." Katika lugha ya Kihabeshi (Kiamhari), ras inamaanisha "kichwa," "mwana mfalme," au "jemadari mkuu," na tafari inamaanisha "kuogopwa." Katika mfumo wa Rastafariani, neno hili linarejelea hasa kwa Ras Tafari Makonnen (1892-1975), ambaye alikuwa Haile Selassie I Mfalme wa Uhabeshi (jina lake la ubatizo la Kikristo) wakati wa kutawazwa kwake mwaka wa 1930, wakati Selassie alipokuwa akisifiwa na majina ya "Simba wa Yuda, Mteule wa Mungu, Mfalme wa Wafalme." Hii ilituma wimbi la mshtuko kupitia utamaduni wa Afro-Caribbean. Katika mitaa ya Kingston, Jamaica, wahubiri kama Joseph Hibbert, walianza kutangaza kwamba Haile Selassie alikuwa Masihi aliyekuwa amengojwa kwa muda mrefu, kuja kwa mara ya pili kwa Kristo. Hivyo ilizaliwa alama moja wa Rastafari, ambayo iliona Selassie kama Mungu aliye hai na masihi mweusi ambaye angeweza kupindua utaratibu uliopo na kuongoza utawala wa weusi.

Alama nyingine ya Rasta imetokea pamoja na alama ya masihi. Kikundi hiki kinachora mizizi yake kwa Leonard Percival Howell na ina vipengele vya Hindu vya uhakika. Wakati mwingine mapema hadi katikati ya miaka ya 1930, Howell alizalisha kijitabu cha ukurasa 14, "Ufunguo ulioahidiwa," ambacho kiliweka kazi ya msingi kwa alama ya pili ndani ya Rastafariani inayoathiriwa na Kihindu na Rosicrucianism. Viongozi wengi katika alama hii pia wamekuwa wanachama wa chama cha siri cha kusaidiana. Matokeo yake ni aina ya kuabudu miungu wengi ya Rastafarian ambayo inatafuta "Roho wa Simba ndani ya kila mmoja wetu: roho wa Kristo."

Muhtasari wa teolojia ya Rastafarian, kama inavyothibitishwa katika alama ya kuabudu miungu: imani kwamba "Mungu ni mwanadamu na mwanadamu ni Mungu"; kwamba wokovu ni wa kidunia; kwamba wanadamu wanaitwa kusherehekea na kulinda maisha; kwamba maneno yaliyosemwa kama udhihirisho wa uwepo wa Mungu na nguvu zinaweza [sote] kuumba na kuleta uharibifu; kwamba dhambi ni ya kibinafsi na ya ushirika; na kwamba ndugu wa Rasta ni watu waliochaguliwa kuonyesha nguvu za Mungu na kukuza amani duniani.

Alama zote za Rasta zinatofautiana moja kwa moja na Neno la Mungu lililofunuliwa katika Biblia. Kwanza, Haile Selassie si Masihi. Wale wanaomwabudu kama hivyo wanaabudu mungu wa uwongo. Kuna Mfalme wa Wafalme mmoja tu, Simba wa Yuda mmoja, na yeye ni Yesu Kristo (angalia Ufunuo 5:5, 19:16), ambaye atarudi katika siku zijazo kuanzisha ufalme Wake wa duniani. Kutangulia kuja kwake, kutakuwa na dhiki kuu, baada ya hapo ulimwengu wote utamwona Yesu "akija juu ya mawingu ya mbinguni kwa nguvu kubwa na utukufu mkubwa" (ona Mathayo 24: 29-31). Haile Selassie alikuwa mtu na, kama watu wote, alizaliwa, aliishi, na akafa. Yesu Kristo, Masihi wa kweli, yu hai na ameketi mkono wa kuume wa Baba (Waebrania 10:12).

Alama ya kuabudu miungu ya Rasta ni sawa na uwongo na kulingana na uongo sawa ambao Shetani amekuwa akiwaambia mwanadamu tangu bustani ya Edeni: "utakuwa kama Mungu" (Mwanzo 3:4). Kuna Mungu mmoja, sio wengi, na ingawa waumini wanamiliki Roho Mtakatifu anayekaa ndani na sisi ni wa Mungu, sisi si Mungu. "Maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi"(Isaya 46:9). Zaidi ya hayo, wokovu sio wa kidunia, ambayo ni mwingine wa kupinga-Maandiko, wazo la "wokovu kwa kazi". Hakuna kiasi cha kazi ya kidunia au matendo mema yanaweza kutufanya sisi kukubalika kwa Mungu mtakatifu na mkamilifu, ndiyo sababu alimtuma Mwanaye Mtakatifu na mkamilifu kufa msalabani kulipa adhabu ya dhambi zetu (2 Wakorintho 5:21). Hatimaye, Rastafarians sio watu wateule wa Mungu. Maandiko ni wazi kwamba Wayahudi ni watu wateule wa Mungu na kwamba bado hajakamilisha mpango wake wa ukombozi wao (Kutoka 6:7; Mambo ya Walawi 26:12; Warumi 11:25-27).

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Rastafariani ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries