settings icon
share icon
Swali

Je! Mtu ambaye ameoleka anapaswa kuwa na rafiki wa karibu wa jinsia tofau?

Jibu


Biblia haizuii urafiki wa karibu kati ya wanaume na wanawake. Kama Wakristo, hata hivyo, kuna baadhi ya kanuni ambazo tungelikuwa wenye hekima tutazingatia. Wanandoa hasa wanahitaji kudhaadhari urafiki wa jinsia tofauti kwa sababu majaribu yanaweza kutokea wakati kuna matatizo ya ndoa. Ikiwa rafiki mzuri wa mwanaume ni mwanamke ambaye si mke wake, anaweza kushiriki matatizo haya na yeye, ambayo inaweza kusababisha mshikamano wa kihisia ambao si mzuri. Vivyo hivyo ni kweli kwa mwanamke ambaye ana rafiki mwanaume ambaye si mume wake.

Watu wengi walioolewa ambao wanaohusika na usinzi huwa hawanui kutafuta maslahi ya kimapenzi nje ya ndoa zao. Watu wengi wanasema, "Sikunuia hili litokee; lilitokea tu." Lakini mambo haya "lilikea tu" wakati "tunacheza na moto" na kujiweka katika hali ambazo ni vigumu kudhibiti. Tunapojisikia kuwa mwenzi hasikilizi mahitaji yetu, tunaweza kujihisi kwa urahisi kwamba "tumeingia katika mapenzi" na mtu mwingine ambaye anatupa tahadhari tunayotamani. Tunapojihisi kupuuzika au kutokubaliwa na mwenzi, tunapaswa kuzungumza mapambano yetu na mpenzi na kuepuka hatari ya kutafuta faraja mahali pengine.

Hata ndoa ambayo imejengwa juu ya msingi wa imani katika Kristo na ina matatizo kidogo haizuiliwi kutokana na kuathiriwa na majaribio ya ziada ya ndoa. Ndiyo maana Biblia haituambii tushikamane na tujaribu kupambana na majaribu, lakini hutuambia tuikimbie vile tunavyofanya kutokana na "tamaa za ujana" (2 Timotheo 2:22). Kujaribu kupambana na majaribu inaonekana kuwa ngumu hasa inapofikia suala la mambo ya moyo au tamaa za mwili. Wakorintho Wa Kwanza 6:18 inatuambia kwamba tunahitaji kuepuka dhambi ya ngono, kwa sababu ni rahisi sana kukimbia majaribu kuliko kukaa na kupigana nayo.

Wanaume na wanawake walioolewa wanapaswa kuepuka kujiweka katika hali tatanishi has na jinsia tofauti. Ikiwa wanaonekana pamoja kwa umma, itatoa hisia mbaya. Ikiwa wako peke yao kwa simu au kwa siri, watajitoa kwa na jaribu la hali ya kihisia au ya kimwili. Biblia inatuambia kwamba kila kitu tunachofanya ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu (1 Wakorintho 10:31), hivyo jambo la hekima lingekuwa kushikamana na kumtembelea kama wanandoa au "marafiki wawili wanaochumbiana" na wanandoa wengine, kinyume hatari inayohusiana na urafiki wa karibu na watu wa jinsia tofauti.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mtu ambaye ameoleka anapaswa kuwa na rafiki wa karibu wa jinsia tofau?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries