settings icon
share icon
Swali

Ombi la mwenye dhambi ni gani?

Jibu


Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua yakwamba yeye ni mwenye dhambi na anahitaji Mwokozi. Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu.

Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 yasema hivi, “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.

Hatua ya pili ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu vile ambavyo Mungu amefanya kwa ajili ya kutibu hali ya upotevu wetu dhambini.Mungu alichukua mwili nakufanyika kuwa mwanadamu katika utu wa Yesu Kristo (Yohana 1:1,14). Yesu alitufundisha ukweli kuhusu Mungu na akaishi maisha makamilifu yenye haki na yasiyo kuwa na dhambi (Yohana 8:46; 2 Wakorintho 5:21). Yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu, kwa kuchukua adhabu tuliyostahili (Warumi 5:8). Yesu alifufuka kutoka kwa wafu kudhihirisha ushindi wake juu ya dhambi,mauti,na jehanamu (Wakolosai 2:15; 2Wakorintho 15). Kwa ajili ya haya yote, tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kuahidiwa uzima wa milele Mbinguni-tutakapo weka imani yetu ndani ya Yesu Kristo. Kile tunacho hitajika kufanya ni kuamini ya kwamba alikufa kwa ajili yetu na akafufuka kutoka kwa wafu (Warumi 10:9-10). Tunaweza kuokolewa kwa neema tu, kupitia imani peke yake, kwake Yesu pekee. Waefeso 2:8 yasema, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema,kwa njia ya imani;ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu,ni kipawa cha Mungu.’’

Kusema Ombi hili la mwenye dhambi ni njia ya rahisi ya kumwelezea Mungu yakuwa unamtegemea Yesu Kristo kama mwokozi wako. Hakuna maneno ya kiuganga yenye kuleta wokovu. Ni kwa imani tu ndani ya kifo cha Yesu na kufufuka kwake vinavyo weza kutuokoa. Kama unafahamu yakwamba wewe ni mwenye dhambi na unahitaji wokovu kupitia kwa Yesu Kristo, hapa kunalo Ombi la mwenye dhambi unaloweza kuomba kwa Mungu: “Mungu, najua yakwamba mimi ni mwenye dhambi. Ninajua ya kwamba ninastahili adhabu ya dhambi zangu. Hata hivyo,ninamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wangu. Ninaamini ya kwamba kifo chake na kufufuka kwake ilikuwa ni kwa ajili ya msamaha wangu. Ninamwamini Yesu na Yesu peke yake kama Bwana na Mwokozi wangu. Ahsante Bwana,kwa kuniokoa na kwa kunisamehe! Amina!’’

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ombi la mwenye dhambi ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries