settings icon
share icon
Swali

Je! Ole tatu za Ufunuo ni gani?

Jibu


Ole maana yake ni “huzuni, dhiki, mateso”; ole tatu za Ufunuo ni hukumu ya mwisho ambayo Mungu ataitangaza kwa wenye dhambi wanaoishi duniani ili iwafanye watubu (Ufunuo 9:20). Ole tatu hakika itakuwa wakati dhiki na mateso kwa wale ambao wameapa kumtii Mpinga Kristo wakati wa nyakati za mwisho.

Alama 7 ni ya muhimu katika Ufunuo, na ole tatu zitakuja kuelekea mwishoni mwa miaka saba ya mateso kabla ya ujio wa pili wa Kristo. Hukumu ya Mungu wakati wa dhiki, zinatazamiwa kuwa mihuri saba, ikiwa inafunguliwa moja baada ya nyingine. Muhuri wa saba unafunua baragumu ya hukumu ya saba. Baragumu ya tano, sita na saba ndio zinaitwa ole tatu (Ufunuo 8:13).

Ole la kwanza limefunuliwa baada ya hukumu ya tarumbeta ya tano. Ole hili linahusisha kitu kama nzige ambao wana uwezo wa kuuma kama nge (Ufunuo 9:3). Mara nyingi, huwa haikubaliki kuwa nzige wa kawaida kwa sababu ya kule kuuma kwao na kwa sababu watoka katika kuzimu na wana utawala wa kishetani (Ufunuo 9:3, 7-8, 11). Viumbe hivi vinaruhusiwa kuwadhuru wale watu pekee ambao hawana “muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao” (Ufunuo 9:4). Wale walio na muhuri wa Mungu ni 144,000 (Ufunuo 7:3-4) au, pengine watakatifu wote wa wakati huo (Waefeso 4:30). Nzige hawa wa kishetani wanaruhusiwa kuwadhuru wasio waumini kwa miezi mitano (Ufunuo 9:5) kwa mdungo ulio wa uchungu. Ijapokuwa waadhiriwa watatami wafe (Ufunuo 9:6), na hawatapewa nafasi ya kukufa.

Ole la pili limefunuliwa baada ya hukumu ya tarumbeta ya sita. Ole hili linaanza wakati sauti ya kuamrisha, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati” (Ufunuo 9:14). Malaika hao wane ni maroho ambayo yalitupwa toka mbinguni pamoja na Shetani. Kwa sasa Mungu amawafunga hadi ule wakati uliowekwa (Ufunuo 9:15; soma Yuda 1:6; 2 Petro 2:4). Malaika hawa na jeshi lao ambalo ni milioni mia mbili, wameachiliwa ili wauwe thuluthi moja ya wanadamu (Ufunuo 9:15-16).

Baada ya ole la pili limepita (Ufunuo 11:14), kutatokea mgawanyiko wa wazi katika kitabu cha Ufunuo na tangazo kutoka mbinguni, “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atatawala milele na milele” (Ufunuo 11:15). Kwa maneno mengine, hatua hii ya mwisho ya hukumu itakuwa mwisho na uadilifu utarejeshwa duniani.

Ole la tatu limefunuliwa baada ya hukumu ya tarumbeta ya saba. Ole hili linafanana ile tarumbeta inayolia katika Yoeli 2 na kutoa ishara ya utimilifu wa mpango wa Mungu kwa ulimwengu wote. Ole hili la tatu linaashiria kukamilika kwa hukumu ya Mungu kwa dhambi; ole hili linaangaziwa sana katika mlango wa 19 wa Ufunuo, wakati Ufalme wa Kristo umeanzishwa duniani. Kilichojumuishwa katika ole hili la tatu na la mwisho ni “bakuli” la ghadhabu ya Mungu ambayo imeelezewa katika Ufunuo 16:1-21. Msururu huu wa hukumu ndio tisho kubwa sana wakaaji wa dunia hawajawai ona. Yesu aliesema, “Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka” (Mathayo 24:22).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ole tatu za Ufunuo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries