settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Eliya atarudi kabla ya nyakati za mwisho (Malaki 4: 5-6)?

Jibu


Malaki 4: 5-6 inatoa unabii unaovutia: "Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana." Hadi hii leo, Wayahudi wa Sada (Seders) wanajumuisha ekiti tupu kwenye meza kwa kutarajia kwamba Eliya atarudi kumtangaza Masihi katika kutimiza neno la Malaki.

Kulingana na Malaki 4: 6, sababu ya kurudi kwa Eliya itakuwa "kugeuza nyoyo" za baba na watoto wao kwa kila mmoja. Kwa maneno mengine, lengo litakuwa upatanisho. Katika Agano Jipya, Yesu anafunua kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa utimizaji wa unabii wa Malaki: "Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja" (Mathayo 11: 13-14). Utekelezaji huu pia umetajwa katika Marko 1: 2-4 na Luka 1:17; 7:27.

Hasa inayohusiana na Malaki 4: 5-6 ni Mathayo 17: 10-13: " Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao. Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji."

"Waalimu wa Sheria" walikuwa walimu wa dini wa Kiyahudi, hasa Mafarisayo na Masadukayo, ambao walitoa ufafanuzi juu ya Maandiko ya Kiyahudi. Petro, Yakobo, na Yohana walikuwa wamefahamu mafundisho yao na kumwuliza Yesu kuhusu Eliya baada ya kumwona Yesu na Musa na Eliya wakati wa kubadilika (Matayo 17: 1-8). Yesu alisema waziwazi kwamba Eliya alikuwa amekwisha kuja, lakini, kwa kusikitisha, hakutambuliwa na aliuawa. Yesu kisha alitabiri kwamba Yeye pia atakufa mikononi mwa adui zake (17:12).

Angalia kwa ufupi huduma ya Yohana Mbatizaji inaonyesha njia nyingi ambazo yeye alikuwa "Eliya." Kwanza, Mungu alitabiri kazi ya Yohana kama ile ya Eliya (Luka 1:17). Pili, amevaa kama Eliya (2 Wafalme 1: 8 na Mathayo 3: 4). Tatu, kama Eliya, Yohana Mbatizaji alihubiri jangwani (Mathayo 3: 1). Nne, wote wawili walihubiri ujumbe wa toba. Tano, hawa wanaume wote waliwapinga wafalme na walikuwa na maadui wa juu (1 Wafalme 18: 16-17 na Mathayo 14: 3).

Wengine wanasema kwamba Yohana Mbatizaji hakuwa Eliya aliyekuwa akuje kwa sababu Yohana mwenyewe alisema kuwa hakuwa Eliya. "Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La" (Yohana 1:21). Kuna maelezo mawili dhahiri ya utata huu. Ya kwanza Eliya hakuwahi fariki (2 Wafalme 2:11), rabi wengi wa karne ya kwanza walifundisha kwamba Eliya alikuwa bado hai na angekuja kabla ya kufika kwa Masihi. Wakati Yohana alikanusha kuwa yeye hakuwa Eliya, angekuwa anapingana na wazo kwamba alikuwa Eliya halisi ambaye alikuwa amechukuliwa mbinguni kwa gari la moto.

Pili, maneno ya Yohana yanaweza kuonyesha tofauti kati ya maoni ya Yohana juu yake mwenyewe na maoni ya Yesu juu yake. Yohana huenda hakujiona kama utimilifu wa Malaki 4: 5-6. Hata hivyo, Yesu alifanya hivyo. Hakuna ugomvi, basi; ni nabii mnyenyekevu anatoa maoni ya uaminifu wa nafsi yake mwenyewe. Yohana alikataa heshima (tazama Yohana 3:30), lakini Yesu alimthibitisha Yohana kama utimilifu wa unabii wa Malaki kuhusu kurudi kwa Eliya.

Kama Elia wa mfano, Yohana aliwaita watu kutubu na maisha ya utii, akiwaandaa watu wa kizazi chake kwa ajili ya kuja kwa Yesu Kristo, Yeye aliyekuja "kutafuta na kuokoa kilichopotea" (Luka 19:10) na kuanzisha huduma ya upatanisho (2 Wakorintho 5:18).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Eliya atarudi kabla ya nyakati za mwisho (Malaki 4: 5-6)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries