settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini tuisome/tuichunguze Bibilia?

Jibu


Ni lazima tuisome na kuichunguza Bibilia kwa sababu ni neno la Mungu kwetu. Bibilia ni neno “Lenye pumzi ya Mungu” (2 Timotheo 3:16). Kwa njia nyingine ni neno lake Mungu mwenyewe kwetu. Kuna maswali mengi ambayo wachanganusi wa Bibilia wameuliza ambayo Mungu ametujibu kupitia Bibilia. Kuna lengo gani la kuishi? Je! Nilitoka wapi? Kunayo maisha baada ya kifo? Nitawezaje kufika mbinguni? Ni kwa nini dunia emejawa na maovu? Ni kwa nini nasumbuka kutenda mema? Zaidi ya hayo maswali “makubwa” Bibilia inatupa wosia/ushauri wa wazi kwa sehemu kama: Ninawezaje kuwa mzazi mwema? Mafanikio ni nini na nitawezaje kufanikiwa? Nitawezaje kubadilika? Ni kitu gani cha maana katika maisha? Nitawezaje kuishi ili nisije nikajute baadaye? Nitawezaje kutatua hali ngumu na matukio mabaya katika maisha kwa ushindi?

Lazima tusome na kuchunguza Bibilia kwa sababu ni ya kuwaminika na haina makosa yoyote. Bibilia ni ya ajabu kati ya vitabu vinayoitwa “vitakatifu” kwa kuwa haitoi mafunzo ya nidhamu pekee na kusema, “niamini.” Bali tuko na uwezo wa kujaribu mamia ya unabii yasema, kuwangalia matukio ya kihistoria ambayo yamenakiliwa ndani yake, na kuwangalia tibitisho za kisayansi ambazo yalinganisha. Wale ambao wanasema kwamba Bibilia iko na kasoro, wamefunga masiko yao kuusikia ukweli. Yesu siku moja akaulizwa, ni lipi rahisi kusema, “dhambi zenu zimesamehewa,” au “amka na uchukue malazi yako na uende.” Na hapo akaonesha kuwa ako na uwezo wa kusamehe dhambi (kitu ambacho hatuwezi kiona kwa macho yetu) kwa kumponya yule kiwete (jambo ambalo waliokuwa karibu wanaweza shuhudia kwa macho yao). Vilevile tumepewa uakikisho kuwa neno la Mungu li kweli wakati inazungumzia sehemu za roho ambazo hatuwezi kusihisi kwa hisia zetu, kwa kujionyesha kuwa kweli ambazo tunaweze kuzihisi kama; ukamilifu wa historia, ukamilifu wa sayansi na ukamilifu wa unabii.

Tusome na tiuchunguza Bibilia kwa sababu Mungu habadiliki na kwa sababu hali ya mwanadamu haibadiliki; ni muimu kwetu sawa na wakati ule iliandikwa. Utaaluma wabadilika, hali ya mwanadamu na maitaji yake hayabadiliki. Twapata tunaposoma kurasa za historia za kibibilia kwamba, hata ingawa twazungumzia uhusiano wa mtu kwa mtu, au wa kujamii, “wala jambo jipya hakuna chini ya jua” (Mhubiri 1:9). Ile hali wakati kizazi kizima cha mwanadamu kinaendelea kutafuta upendo na toshelesho katika kokote kubaya, ni muhumu Yesu alikwisha sema, “Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” (Mathayo 4:4). Kwa njia nyingine, kama tunataka kuishi maisha tele, vile Mungu alikwisha panga, lazima tusikize na kutii chenye kimeandikwa katika neno lake.

Ni lazima tusome na kuichunguza Bibilia kwa sababu kuna mafunzo potovu ulimwenguni. Bibilia inatupa kipimio ambacho kwacho tunaweza kutofautisha kati ya kweli na kasoro. Inatueleza Mungu anakaa namna gani. Kuwa na picha mbaya juu ya Mungu ni kuwabudu miungu ya uongo. Tunakiabudu kitu kingine ambacho si Mungu. Bibilia yatwambia kikamilifu vile mtu anaweza fika mbinguni, na si kwa kuwa mwema, au kubatizwa au kwa kitu chochote tufanyacho (Yohana 14:6; Waefeso 2:1-10; Isaya 53:6; Warumi 3:8-10; 5:8, 6:23, 10:9-13). Katika dhana hii neno la Mungu latuonyesha ni jinsi gani Mungu anatupenda (Warumi 5:6-8; Yohana 3:16).

Bibilia yatujenga ili tumtumikie Mungu (2 Timotheo 3:17; Waefeso 6:17; Waebrania 4:14). Inatuzaidia kujua jinsi ya kuokolewa kutoka kwa dhambi zetu na madhara yake (2 Timotheo 3:15). Kuwaza neno la Mungu na kutii mafunzo yake litaleta mafanikio katika maisha yetu (Yoshua 1:8; Yakobo 1:25). Neno la Mungu latufanya kuziona dhambi katika maisha yetu na kutusaidia kuziondoa (Zaburi 119:9, 11). Linatupa mwelekeo katika maisha, na kutufanya kuwa na hekima kuliko walimu wetu (Zaburi 32:8, 119:99; Methali 1:6). Bibilia yatuzuia kupoteza miaka ya maisha yetu kwa mambo yale hayana maana na hayatadumu (Mathayo 7:24-27).

Kusoma na kuichunguza Bibilia inatusaidia kuona mbele ya mvuto “mvuto wa machungu” ama kupata kushikiliwa na dhambi za majaribu, ili tuweze kusoma kutoka kwa makosa ya wengine badala ya kuyafanya kuwa yetu. Uzoefu ni mwalimu mkuu, lakini wakati unafika twajifunza kutoka kwa dhambi, huyo ni mwalimu mkali na mpaya sana. In afadhali kusoma kutoka kwa makosa ya wengine. Kuna baadhi ya wahusika wa Bibilia wengi tunaoweza kusoma kutoka kwao, baadhi ya wengine wako na tabia ya kuiga na wengine si wa tabia ya kuiga. Kwa mfano Daudi kumshinda kwake Goliathi yatufunza kwamba Mungu ni mkuu kuliko kitu chochote atuitishacho uso kwa uso (1 Samweli 17), bali kwanguka kwake kwa majaribu na kufanya uzinzi na Bath-sheba yaonesha vile uovu wa muda waweza kudumu na madhara yake (2 Samweli 11).

Bibilia si kitabu cha kusoma tu pekee. Bali ni kitabu cha kusoma ili yanosomwa yaweze kutumika katika maisha yetu. La sivyo, ni kama kumeza chakula bila kutafuna na kisha baadaye kutapika tena-hakuna ile kinga ya chakula mwili unaweza pata. Bibilia ni neno la Mungu. Kwa sababu hiyo latufunga kama sheria ya uumbaji. Tunaweza kuipuuza, lakini twafanya hivyo kwa madhara yetu wenyewe, vile tukipuuza sheria ya ardhi. Inaweza sizitishwa ya kutosha umuimu Bibilia ikonayo kwa maisha yetu. Kuichunguza Bibilia kunaweza linganishwa kuchimba migodi/dhaabu. Tukiweka bidii kidogo na kwa urahisi “kuvuka mto kwa kutumia jiwe laini” tutapata tu dhaabu kidogo yenye vumbi. Tunavyo zidi kutia bidii kuichimbua Bibilia tutapokea tuzo zaidi kwa bidii yetu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini tuisome/tuichunguze Bibilia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries