settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje nini kuhusu nidhamu ya kanisa / kutengwa?

Jibu


Kutengwa ni kuondolewa rasmi kwa mtu binafsi kutoka uanachama wa kanisa na kujitenga rasmi kutoka kwa huyo mtu binafsi. Mathayo 18:15-20 inatoa utaratibu na mamlaka kwa kanisa kufanya hivyo. Inatuamurisha kwamba mtu mmoja (kwa kawaida upande ule umekosewa) ni kwenda kwa mtu binafsi aliye mkosea. Kama yeye hatatubu, kisha waili au watatu waenda kuthibitisha hali na akatae kutubu. Kama bado hakuna toba, inachukuliwa mbele ya kanisa. Utaratibu huu kamwe "si wa kufurahia," ni kama tu vile baba kamwe hafurahi katika kuwapa nidhamu watoto wake. Mara nyingi, ingawa ni muhimu. Lengo halikusudiwi kuwa na nia mbaya au kuonyesha nia ya kuwa "mtakatifu kuliko wewe". Badala yake, lengo ni urejesho wa mtu binafsi kwa ushirika kamili pamoja na Mungu na waumini wengine. unastahili kufanyika kw upendo kwa huyo mtu binafsi, katika utii na heshima kwa Mungu, na katika hofu; kwa ajili ya wengine katika kanisa.

Biblia anatoa mfano wa umuhimu wa kutengwa katika kanisa- kanisa katika mji wa (1 Wakoritho 5:1-13). Katika fungu hiki, mtume Paulo pia anatoa baadhi ya madhumuni hasa ya kutengwa kibiblia. Moja ya sababu (haipatikani moja kwa moja katika kifungu hiki) ni kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu Kristo (na kanisa lake) mbele ya mahakimu wasioamini. Wakati Daudi alitenda dhambi pamoja na Bathsheba, moja ya matokeo ya dhambi yake ni kwamba jina la Mungu mmoja wa kweli lilitukanwa na maadui wa Mungu (2 Samweli 12:14). Sababu ya pili ni kwamba dhambi ni kama saratani; kama imeruhusiwa kuwepo, inaenea kwa wale wa karibu katika njia sawa na "chachu kidogo kazi kwa donge lote la unga" (1 Wakorintho 5:6-7). Pia, Paulo anaeleza kuwa Yesu alituokoa ili tuweze kutengwa mbali na dhambi, ili tuweze kuwa "wasiochachwa" au huru kutoka kwa kile ambacho husababisha kuoza kiroho (1 Wakorintho 5:7-8). Tamanio la Kristo kwa ajili ya bibi wake, kanisa, ni aweza kuwa safi na isiye na hitilafu (Waefeso 5:25-27).

Kutengwa pia ni ustawi wa muda mrefu wa mmoja anaye pewa nidhamu na kanisa. Paulo, katika 1 Wakorintho 5:5, anasema kwamba kutengwa ni njia ya kutoa mwenye dhambi asiyetubu "kwa Shetani, ili hali ya dhambi iangamizwe na roho yake iokolewe siku ile ya Bwana." Hii ina maana kwamba kutengwa kunaweza kuwa kwamba kunahusisha Mungu kwa kumtumia Shetani (au mojapo wa mapepo yake) kama chombo cha nidhamu hufanya kazi katika maisha ya mwenye dhambi kimwili huleta toba ya kweli katika / moyo wake.

kwa matumaini hatua za kinidhamu ya kanisa ni mafanikio katika kuleta huzuni wa kiungu na toba ya kweli. Wakati hili hutokea, mtu anaweza kurejeshwa kwa ushirika. Mtu kushiriki anayehusika katika 1 Wakorintho 5 kifungu kilitoa toba, na Paulo anawatia moyo kanisa kumrejesha kwa ushirika na kanisa (2 Wakorintho 2:5-8). Kwa bahati mbaya, hatua za kinidhamu, hata wakati zinafanyika katika upendo na katika njia sahihi, si kila mara zote zina mafanikio katika kuleta urejesho huo. Lakini hata wakati nidhamu ya Kanisa inashindwa kufikia lengo lake la kuleta toba, bado inahitajika kukamilisha malengo mengine mema yaliyotajwa hapo juu.

Kuna uwezekano sisi wote tulishuhudia tabia ya kijana ambaye ameruhusiwa kufanya kama apendavyo na hakuna hatua thabiti za kinidhamu. Sio jambo jema. Wala ulezi kama huo si wa upendo, kwa maana humpotosha mtoto kwa maisha mabaya baadaye. Tabia kama humfanya mtoto kutengeneza uhusiano usio wa maana na kufanya vyema katika mazingira yoyote. Vile vile, nidhamu katika kanisa, kamwe haitakuwa ya kufurahisha au rahisi, si eit ni ya muhimu tu pekee, bali nay a upendo pia. Hata hivyo imeamuriwa na Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje nini kuhusu nidhamu ya kanisa / kutengwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries