settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini asili ya dhambi ?

Jibu


Swali la zamani la ni wapi na ni jinsi gani dhambi ilianza limechunguzwa na kujadiliwa na baadhi ya watu wenye tajiriba kubwa ya historia, na bado hakuna anayeweza kutoa jibu la uhakika kabisa au la kuridhisha. Baadhi hunukuu Isaia 45:7, wakitafuta kumfanya Mungu kuwa mwanzilishi wa dhambi: “Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza, ninaleta mafanikio na kusababisha maafa. Mimi, Bwana, huyatenda haya yote.” Neno uovu, kutoka katika neno la awali la Kiebrania rah, litatafsiriwa vyema kama “msiba.” Muktadha wa kifungu hiki unahusu ukuu wa Mungu juu ya misiba ya asili. Mungu ni mkuu juu ya vitu vyote (Kutoka 4:11), lakini Yeye si mwanzilishi wa dhambi (1 Yohana 1:5; taz. Yakobo 1:13). Anachukia dhambi (Mithali 8:13). Uovu wa kiadili ulitokana na kiumbe na sio Muumba.

John Calvin aliandika, “Bwana alikuwa ametangaza kwamba ‘kila kitu alichokifanya…kilikuwa kizuri sana’ (Mwanzo 1:31). Basi uovu huu unatoka wapi kwa mwanadamu, hata amwache Mungu wake? Ili tusije tukafikiri kwamba yanatokana na uumbaji, Mungu alikuwa ameweka muhuri Wake wa kibali juu ya kile kilichotoka kwake. Kwa nia yake mbaya, basi, mwanadamu aliharibu asili safi aliyopokea kutoka kwa Bwana; na kwa kuanguka kwake aliingiza wazao wake wote pamoja naye kwenye maangamizo. Ipasavyo, tunapaswa kutafakari sababu dhahiri ya hukumu katika asili potovu ya ubinadamu-iliyo karibu zaidi nasi-badala ya kutafuta sababu iliyofichika na isiyoeleweka kabisa katika maamuzi ya Mungu” (Institute/Taasisi, 3:23:8). Kwa maneno mengine, dhambi haikuwa sehemu asili ya uumbaji, wala haikuamuliwa na mapenzi ya Muumba.

Mwanadamu wa kwanza, Adamu, alitenda dhambi, na kosa lake likawaingiza wanadamu katika dhambi, lakini hiyo haikuwa asili ya dhambi. Ezekieli 28:13-15 inasema kwa njia ya kimfano juu ya Shetani, ambaye mwanzoni aliumbwa bila dosari, kama vile vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu. Mstari wa 15 unatupa dokezo kuhusu chanzo cha dhambi: “Ulikuwa mnyofu katika njia zako tangu siku ile ya kuumbwa kwako, hadi uovu ulipoonekana ndani yako.” Isaya 14:12-14 inayonyesha zaidi kwamba Shetani (Lusifa) alitenda dhambi kwa kiburi chake na kutamani kwake kiti cha enzi cha Mungu. Alipomwasi Mungu, Shetani alifukuzwa kutoka mbinguni (Ezekieli 28:15-17; taz 1 Timotheo 3:6).

Hii inatuleta kwa swali, je, uovu ulijidhihirishaje katika kiumbe mkamilifu? Inaweza kuwa vyema kutaja kwamba uovu si kitu kilichoumbwa-sio kiumbe na hauna kiumbe huru. Pia, ouvu hauna kiwango kama vile wema; ni upungufu, ukosefu, kukosa kufikia kiwango cha wema kamilifu wa Mungu. Dhambi zote, hata kama zinaonekana kuwa ndogo kiasi gani, zinapungukiwa na ukamilifu wa kiadili. Mungu daima yuko katika hali Yake kamilifu (Kumbukumbu 32:4). Kwa hivyo, dhambi zote lazima zitoke kwa kiumbe, na tamaa ya uovu inatoka ndani ya kiumbe (Yakobo 1:14-15). Dhambi “ilipatikana” ndani ya Lusifa kwa sababu ya chaguo ambalo malaika alifanya la kutafuta kitu mbali na kile Mungu alikuwa amemchagulia. Wakati wowote tunatafuta “kingine” zaidi na mapenzi ya Mungu, tunafanya dhambi.

Kusema kuwa dhambi ilianza ndani ya viumbe vya Mungu haimaanishi Mungu alishangazwa nayo. Ingawa Mungu hakuleta dhambi, kwa hakika aliiruhusu au haingekuwepo, kwa kuwa Mungu ni mkuu juu ya vitu vyote. Ni kweli kwamba angeweza kuzuia dhambi, lakini hiyo ingemaanisha kuuvua uumbaji wake uhuru wa hiari (Danieli 4:17; taz Zaburi 33:1011). Njia zake zote ni bora. Ndani Yake “hamna giza lolote” (1 Yohana 1:5), na sasa hivi anafanya mambo yote kwa mapenzi yake mema (Warumi 8:28; taz. Isaya 46:9-10).

Siri ya uovu na ni kwa nini Mungu ameruhusu uhalisi wake pamoja na mateso yote yanayosababishwa nayo huenda isijulikane kikamilifu katika ulimwengu huu, lakini Maandiko yanahakikisha kwamba uovu ni wa muda tu. Pindi kilele cha mpango wa ukombozi wa Mungu kitakapokamilika, Yesu Kristo atakuwa ameharibu kazi ya shetani milele (1 Yohana 3:8).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini asili ya dhambi ?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries