settings icon
share icon
Swali

Ni kitu gani wanandoa Wakristo wameruhusiwa/hawajaruhusiwa kufanya katika ngono?

Jibu


Bibilia yasema kwamba “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu” (Waebrania 13:4). Maandiko hayasemi ni kitu gani ambacho mume na mke wanastahili/hawastahili kufanya kimapenzi. Mume na mke wameamriwa, “Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda” (1 Wakorintho 7:5a). aya hii huenda yanakili kanuni za uhusiano wa mapenzi katika ndoa. Cho chote kinachofanywa, lizima kifanyika katika mapatano. Kusiwe na mtu ambaye ameshawishiwa au kushurutishwa kufanya jambo ambalo hakubaliana nalo au analifikiri ni baya. Kama mume na mke wote wamekubaliana kwamba wanataka kujaribu jambo fulani (kwa mfano, mapenzi ya mdomo, kwa njia mbalimbali, mifano ya ngono ya vidude na kadhalika), basi Bibilia haitoi sababu yoyote ya kutofanya hivyo.

Kuna vitu vichache, isipokuwa, haviruhusiwi kamwe kwa wanandoa. Mazoea ya “kubadilishana” au “kujumulisha wengine wengi” (wengine watatu, wengine wane) ni dhahiri kuwa huo ni uzinzi (Wagalatia 5:19; Waefeso 5:3; Wakolosai 3:5; 1 Wathesalonike 4:3). Uzinzi ni dhambi, hata kama mwenzi wako katika ndoa anauruhusu au kuuitikia au kuufanya. Ponografia yahuitaji “tamaa ya mwili na tamaa ya macho” (1 Yohana 2:16) na kwa hivyo imeshutumiwa vilevile na Mungu. Mume na mke kamwe wasilete ponografia katika ushirika wao wa ngono. Mbali na haya mambo mawili, hakuna kitu cho chote ambacho maandiko yanakataza mume na mke wasifanye wao wenyewe kama wamekwisha kubaliana.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kitu gani wanandoa Wakristo wameruhusiwa/hawajaruhusiwa kufanya katika ngono?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries