settings icon
share icon
Swali

Je! Neema ya kuokoa ni nini?

Jibu


Kama lahaja, "neema ya kuokoa" inamaanisha "ubora wa ukombozi" ambao hufanya mtu au kitu kukubalika. Lakini hiyo sio maana ya kibiblia. Neno neema katika Biblia linamaanisha "usaidizi wa Mungu usiostahili unaopewa watu kwa ajili ya kuzaliwa upya au utakaso" au "ukarimu wa Mungu kwa wasiostahili." Kibiblia, "neema ya kuokoa" ni neema ya Mungu inayookoa mtu.

Maandiko yanasema kuwa neema, neema ya Bwana isiostahili, ni muhimu "kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya Sheria" (Warumi 3:20). Njia pekee ya kupokea neema ya kuokoa ya Mungu ni kupitia imani katika Kristo: "Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo Sheria. . . haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio"(Warumi 3:21-22).

Neema ya kuokoa husababisha utakaso wetu, mchakato ambao Mungu anatufanya sawa na sura ya Kristo. Wakati wa wokovu, kwa neema kupitia imani, Mungu hutufanya viumbe vipya (2 Wakorintho 5:17). Naye anaahidi kamwe kuwaacha watoto Wake: "Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu" (Wafilipi 1:6).

Hatuna chochote ndani yetu ambacho kitatupongeza kwa Mungu (Warumi 3:10-11) -Hutuna "neema ya kuokoa" peke yetu. Kwa kuwa kimsingi hatukubaliki kwa Mungu, tunaomba, pamoja na wanafunzi wa Yesu, "Tunawezaje kuokolewa?" Jibu la Yesu linathibitisha: "Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu" (Luka 18:26-27). Wokovu ni kazi ya Mungu. Anatoa neema tunayohitaji. "Neema yetu ya kuokoa" ni Kristo Mwenyewe. Kazi yake msalabani ndiyo inatuokoa, sio sifa zetu wenyewe.

Ni rahisi kufikiria kwamba, kwa imani yetu, tunachangia katika njia fulani kidogo kwa wokovu wetu. Baada ya yote, sifa ya Kristo inapaswa kutumiwa kwetu kwa imani, na inaonekana imani yetu inakuja kutoka kwetu. Lakini Warumi 3:10-12 inasema kwamba hakuna hata mmoja wetu anayemtafuta Mungu. Na Waefeso 2:8 inasema, "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu." Waebrania 12:2 inasema kwamba Yesu ndiye mwandishi na mkamilizi wa imani yetu. Neema ya kuokoa ya Mungu ni kipawa chake kamili. Hata uwezo wetu wa kukubali neema Yake ya kuokoa ni kipawa kingine tu kutoka kwa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Neema ya kuokoa ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries