settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini sola gratia ni muhimu?

Jibu


Sola gratia ni muhimu kwa sababu ni moja wapo ya sifa zinazotofautisha au mambo muhimu ambayo hutenganisha Injili ya kweli ya kibiblia na injili za uwongo ambazo haziwezi kuokoa. Kama moja wapo ya sola tano ambazo zilifafanua masuala muhimu ya Mageuzi ya Kiprotestanti, fundisho hili ni la muhimu sana jinsi na namna lilivyokuwa enzi hizo. Neno la Kilatini sola humaanisha "pekee yake" au "pekee," na fundisho muhimu la Kikristo liliwakilishwa na vifungu hivi tano vya Kilatini kwa ustadi vinatoa muhtasari wa fundisho la kibiblia juu somo hili muhimu: sola scriptura- maandiko pekee-sola fide-imani pekee, sola gratia-neema pekee, sola Christus-Kristo pekee na sola Deo gloria- kwa utukufu wa Mungu pekee. Kila moja wapo na la muhimu, na zote zimehusiana kwa karibu sana. Kupotoka kutoka kwa moja yake itaelekeza katika kukosea katika fundisho muhimu, na matokeo kila wa wakati ni injili potovu ambayo haina nguvu ya kuokoa.

Sola gratia kwa ufupi ni kukubali kuwa Biblia inafundisha kuwa ujumla wa wokovu wetu ni karama ya neema kutoka kwa Mungu. Vile Waefeso 2:8-9 inavyosema, "Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu. Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu." Ni kubalio kwamba kuokolewa toka kwa ghadhabu ya Mungu ni juu ya neema na huruma za Mungu na sio kitu chochote kizuri ndani yetu. Sababu moja ni kwa nini watu wengi wanakataa fundihso hili muhimu ni kwamba hawataki kukubali chenye Biblia inafunza wazi kuhusu hali ya kimsingi ya mwanadamu tangu kuanguka kwa Adamu. Biblia inasema kuwa nyoyo zetu ni "danganyifu" na "ovu" (Yeremia 17:9) na kuwa "Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: "Hakuna hata mmoja aliye mwadilifu! Hakuna mtu anayeelewa, wala anayemtafuta Mungu" (Warumi 3:10-11). Badala ya kukubali kuwa sisi wenyewe hatujiwezi na hatuna tumaini bila neema yake Mungu, watu wengi wanataka kuamini kuwa wana jukumu katika wokovu wao. Lakini Biblia ii wazi kuwa hatuwezi pata kibali cha Mungu kwa matendo yetu; ni kwa neema Yake tu.

Ukweli wa sola gratia au wokovu kwa neema pekee ndio kitu kilimtia moyo Yohana Newton kuandika wimbo wa ajabu "Neema ya Ajabu." Ni neema iliyo ya ajabu kwamba inaweza okoa mwovu kama mimi. Ni neema ya ajabu Mungu alidhihirisha "Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu" (Warumi 5:8). Fundisho hili ni la muhimu sana kwa sababu linawasilisha kweli kwamba Mungu anatuokoa kwa sababu ya huruma na wema Zake na sio kwa sababu ya chochote kinachotufanya kutamanika na Mungu au kuwa wa dhamani ili tuokolewe. Hatuwezi elewa jinsi neema ya Mungu ilivyo ya ajabu katika wokovu hadi kwanza tuelewe jinsi tulivyo wenye dhambi.

Sola gratia ni muhimu kwa sababu ikiwa tutaikataa, tunakataa Injili pekee inayookoa. Njia mbadala kuliko ile ya sola gratia ni injili ambayo inategmea wema wa mwanadamu badala ya neema ya Mungu, ambayo si injili. Sola gratia ndio huifanya Injilie kuwa "habari njema." Inatusaidia kuelewa kwamba huku Bibli ikisema hakuna "hata mmoja anayemtafuta Mungu" (Warumi 3:11), habari njema ni kuwa Mungu anawatafuta wenye dhambi. Yesu alisema kuwa alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea (Luka 19:10), na sio kwa kungoja kilichopote kimtafute. Ni Mungu anachukua hatua wa kwanza, ni Mungu huwavuta waovu kwake, ni Mungu apeanaye maisha mapya kwa mtu ambaye "amekufia makosa na dhambi zake," ni Mungu humsababisha mtu "kuzaliwa tena" ili mtu huyo aweze "kuutafuta ufalme wa Mungu."

Mwishowe, sola gratia ni muhimu kwa sababu ndio msingi wa uhakikisho wetu wa wokovu kama wenye dhambi mbele za Mungu. Ikiwa tutaikata sola gratia, basi hatuwezi kuwa na hakikisho lolote la wokovu wetu. Jinsi kila kitu tunachofanya kimeharibiwa na dhambi, tunawezaje kuwa na ujaziri kuwa tuna Imani ya kutosha kuokolewa? Bahati nzuri, Biblia inafunua Injili sio kwa misingi ya kile tunachofanya bali kwa kile Yesu Kirsto amefanya. "Habari Njema" ni kuwa Kristo alikuja, akaishi maisha matakatifu, akafa msalabani na kufufuka kutoka kwa wafu ili awape maisha mapya wenye dhambi wafu, awakomboe kutoka kwa dhambi zao na kuwapa uzima wa milele pamoja Naye. Hii ndio sababu tunaweza kujua kuwa Yesu hawezi kumpoteza yeyote kati ya wale Baba amempa, bali atawafufua siku ya mwisho (Yohana 6:39).

"Katika neema ya Yesu, nimeokolewa,
Nilipotea dhambini, nilikuwa kipofu rohoni
Bali neema ya Yesu yanitosha sana
Ilinifumbua macho yangu, ikanifungua
Kilikuwa mwenye hofu nilifungwa nazo
Nimefunguliwa sasa kwa neema ya Yesu
Nitamsifu Bwana wangu maishani mwote,
Kwani nnina ushirika msalabani mwake.
Tutakapofika wote Mbinguni kwa Mungu
Tutashukuru neema ya Yesu milele.
Katika neema ya Yesu, nimeokolewa, Nilipotea dhambini, nilikuwa kipofu rohoni"

—"Neema ya Ajabu" ulitungwa na John Newton.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini sola gratia ni muhimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries