settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema chochote kuhusu kufanikisha ndoa ya pili?

Jibu


Ibrahimu ndiye mtu peke yake katika Biblia ambaye anaelezewa hasa kuwa alioa tena baada ya kifo cha mke (Mwanzo 25: 1), lakini Biblia haizungumzii jinsi ndoa hio ya pili ya Abrahamu ilivyokuwa. Biblia haizungumzii mtu aliyeoa tena baada ya talaka. Lakini, ikiwa ndoa ya pili ni kutokana na ndoa ya awali ambayo iliisha kwa talaka au kifo cha mwanandoa, kuna kanuni za kibiblia ambazo hutumika kufanya ndoa ya pili kufanikiwa.

Ikiwa ni ndoa ya kwanza, ya pili, au ya tatu, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kwa dhabihu (Waefeso 5:25) na wake wanapaswa kuwatii kwa wema waume zao (Waefeso 5:22). Mume na mke wake wanapaswa kuona ndoa kuwa ya kudumu na sio kutenganishwa ila tu kwa kifo (Mathayo 19: 6). Wanaume na wake wanapaswa kupendana, kusameheana, na kuheshimu na kuelewana (Waefeso 5:33, 1 Petro 3: 7).

Mara nyingi ndoa za pili husababisha familia zilizochanganyika, na hiyo yenyewe inaweza kusababisha matatizo mengi. Kanuni ya kuondoka na kushikamana ni muhimu sana. Ndoa yafaa kuwa kipaumbele zaidi ya mahusiano mengine ya familia, ni katika ndoa tu ambapo ni watu wawili walio na mwili mmoja. Migogoro ambayo mara nyingi hutokea ndani ya familia ziliyochanganywa inapaswa kushughulikiwa kwa umoja.

Ni muhimu sana kwamba waume na wake katika ndoa za pili wasifananishe wanandoa wao wapya na wanandoa wao wa hapo awali. Kufanya hivyo husababisha chuki, wivu, na matarajio yasiyo ya kweli. Mwanandoa wa sasa sio sawa na mwanandoa wa kwanza na hatarajiwi kuwa sawa. Ikiwa ndoa ya awali ilikuwa nzuri au ya kutisha, hisia na maumivu haipaswi kupelekwa kwenye ndoa ya pili.

Zaidi ya yote, la msingi kufanikisha ndoa ya pili ni kuisalimisha ndoa kwa Mungu na kumtegemea kwa neema na nguvu zinazohitajika. Ndoa inalenga kuonyesha Kristo na kanisa (Waefeso 5: 29-32). Ni katika Kristo tu ambapo ndoa inaweza kuwa vile ambavyo Mungu analenga iwe. Pia, katika ndoa yoyote, wakati matatizo yanapojitokeza, wanandoa wanapaswa kutafuta ushauri wenye hekima kutoka kwa mchungaji na / au mshauri wa Kikristo (Mithali 15:22). Kuelewa kile Mungu anasema kuhusu ndoa na kuwasilisha ndoa kwake mungu ni msingi wa kufanya ndoa yoyote kufanikiwa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema chochote kuhusu kufanikisha ndoa ya pili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries