settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu ndoa isiyo na furaha?

Jibu


Jambo moja tunajua kwa kweli: kuwa katika ndoa isiyo na furaha sio misingi ya Biblia ya talaka. Katika Marko 10: 11-12 Yesu alisema, "Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini. "Kulingana na Biblia, tunaona kwamba watu hawana haki ya kuvunja ndoa isiyo na furaha. Mungu alitaka ndoa iwe ya kudumu milele.

Waefeso 5 inaonyesha ndoa kama picha ya uhusiano wa Mungu nasi. Hii ni mojawapo ya sababu kwa nini Mungu ana nia ya kuweka ndoa imara. Ndoa na nyumba zilizovunjika ni mbaya kwa mume na mke, na vilevile kwa watoto wanaohusika. Uharibifu wa kifedha ni moja tu ya matokeo mabaya ya talaka. Kitengo cha familia ni msingi wa jamii yoyote, na talaka ina athari kubwa juu ya utamaduni wote.

Hii haimaanishi kwamba Mungu anataka kutulazimisha kubaki milele katika ndoa isiyo na furaha. Haimaanishi kwamba tunafaa tuteseke katika hali hiyo. Wakati Mungu anaangazia matatizo ya ndoa, anafanya hivyo kwa mtazamo wa jinsi ya kuzibadili, sio jinsi ya kuvunja ndoa. Kwa mfano, Paulo anaandika kuhusu athari za pepo katika ndoa (1 Wakorintho 7: 5). Anasema kwamba wanandoa wanapaswa kuwa na uhusiano wa ngono ili Shetani asiweze kuwajaribu. Petro anawahimiza waume kuwatendea wake zao kwa ufahamu ili sala zao zisizuiliwe (1 Petro 3: 7). Kutoka kwa vifungu hivi tunaweza kuona kwamba ndoa ni uwanja wa vita vya kiroho. Inahitaji bidi kuwa na uhusiano mzuri, si kupigana katika uhusiano.

Mungu anatutia moyo kuelekea upatanisho. Mathayo 18: 15-16 inahimiza mazungumzo ya wazi yenye, uaminifu yanayotatua maumivu yaliosababishwa na dhambi. Hata hutuhimiza kupata msaada ili kutatua matatizo. Mungu pia anatuita sisi kupata furaha yetu au furaha ndani yake (Wafilipi 4: 4). Furaha ya Bwana ni kitu ambacho unaweza kuwa nacho haijalishi hali ilivyo. Katika miongozo yote ya Mungu ya kupata furaha, hakuna hata moja inayehitaji mwenziwe afanyie kazi. Mke hawezi kudhibiti uwezo wetu wa kuwa na furaha au amani. Yakobo 1: 3-4 inatuambia kuwa furaha ya kudumu inabakia kama tunapovumilia kupitia majaribu tukisaidiwa na Mungu, na kama imani yetu inakua na kuimarika.

Kitabu cha Wafilipi ni funzo kubwa katika tofauti kati ya furaha na tabasamu. Imeandikwa na Mtume Paulo wakati alifungwa gerezani huko Roma. Kitabu hiki kinatumia maneno furaha, kufurahi, na tabasamu mara 16 na kutufundisha jinsi ya kuwa na kuridhika kweli katika Yesu Kristo, licha ya hali zetu. Katika minyororo, Paulo anazungumzia juu ya imani yake katika Kristo na jinsi ilivyobadilisha mtazamo wake wote juu ya mateso.

Mungu amewapa waume maelekezo wazi katika Waefeso 5: 25-28: "Wanaume, wapendeni wake zenu, kama Kristo pia alivyopenda kanisa, akajitoa mwenyewe kwa ajili yake. . . . Kwa hivyo wanapaswa kupenda wake zao kama miili yao wenyewe. Anayependa mkewe anajipenda mwenyewe." Kwa wake, maagizo ya Mungu ni kunyenyekea kwa uongozi wa waume zao (mstari wa 22) na kuwaheshimu waume zao (mstari wa 33). Wanapaswa kunyenyekeana katika kicho cha Kristo (Waefeso 5:21). Ikiwa wote wawili wanaishi kulingana na majukumu yao ya kibiblia, kutakuwa na furaha katika ndoa. Mwanamke mgani hawezi kuheshimu na kunyenyekea kwa mtu anayempenda kama vile Kristo anapenda kanisa lake? Na ni mume gani hawezi kumpenda mwanamke anayemheshimu na kunyenyekea? Ukosefu wa furaha ambayo iko katika ndoa nyingi sana mara nyingi husababishwa na moja au pande zote mbili kukataa kumtii Mungu na kutii mapenzi Yake ya ndoa ambayo yamewekwa wazi. Wakati mwingine hali ya ukosefu wa furaha imeongezeka kwa masuala yasiyotatuliwa ya mume au mke ambayo huingia kwenye ndoa. Katika matukio hayo, ushauri wa kibinafsi unaweza kuwa na manufaa pamoja na ushauri wa ndoa.

Hata kama ndoa isiyo na furaha inasababishwa na muumini anayeolewa na asiyeamini, daima kuna uwezekano wa mwanandoa anayeamini anaweza kumwongoza asiyeamini kwa mwenendo wake safi na mwenendo mzuri. " Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu." ( 1 Petro 3: 1). Biblia inazungumzia hasa wale walioolewa na wasioamini katika 1 Wakorintho 7: 12-14: "... ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe."

Hatimaye, tunapaswa kumbuka kwamba "macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya."(1 Petro 3:12). Mungu anajua uchungu wa ndoa isiyo na furaha, na anaelewa tamaa za kimwili, lakini ametupa Neno lake juu ya suala hili na anaomba utii. Kumtii Mungu daima huleta furaha (Warumi 16:19).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu ndoa isiyo na furaha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries