settings icon
share icon
Swali

Je! Ndama mwekundu ni ishara ya nyakati za mwisho?

Jibu


Kutimiza masharti ya sheria ya Agano la Kale, ndama mwekundu alihitajika kusaidia kutimiza utakazo kutoka kwa dhambi-hasa, jivu la ndama mwekundu lilihitajika. Ndama mwekundu alikuwa ngome kwekudnu-hudhurungi, angalau wa miaka miwili. Alifaa awe, "hana doa lolote au udhaifu" na awe hajawai kubeba nira. Dhabihu ya ngombe mwekundu ilikuwa ya kipekee katika sheria kiwango kwamba ilitumia ngombe wa kike, alitolewa dhabihu mbali na lango la kuingia katika hema ya ibada, na hiyo ndio ilikuwa dhabihu pekee ambayo mnyama wa rangi alikubaliwa.

Uchinjaji wa ndama mwekundu umeelezewa katika Hesabu 19: 1-10. Eleazari kuhani alipaswa kusimamia ibada nje ya hema ya Waisraeli. Baada ya mnyama kuuliwa, Eleazari alipaswa kunyunyiza sehemu ya damu yake kuelekea upande wa mbele wa hema ya ibada mara saba (Hesabu 19: 4). Kisha aondoke kambini tena na akasimamie uchomaji wa mzoga wa ndama mwekundu (Hesabu 19: 5). Wakati ndama mwekundu ilipochomeka, kuhani aliamriwa kuongeza "kuni za mwerezi, husopo na sufu nyekundu" katika moto huo (Hesabu 19: 6).

Majivu ya ndama mwekundu yalikusanywa na kuhifadhiwa "mahali safi nje ya kambi." Majivu hayo yalitumika "kutumiwa na jumuiya nzima ya Israeli kutengeneza maji ya kuondoa najisi, ili kuondoa dhambi" (Hesabu 19: 9). Sheria inaendelea kuelezea kwa kina ni lini na ni jinsi gani majivu ya ndama mwekundu yatatumika kutakasa wale waliogusana na maiti: "Mtu akigusa maiti ya mtu yeyote, atakuwa najisi kwa siku saba. Siku ya tatu na ya saba mtu huyo atajiosha kwa yale maji ya utakaso, naye atakuwa safi. Lakini akiacha kujitakasa katika siku ya tatu na ya saba, mtu huyo atabaki kuwa najisi" (Hesabu 19: 11-12). Utaratibu wa utakaso ulihusisha majivu ya huyo ndama mwekundu kwa njia hii: "Kwa ajili ya wale waliojitia najisi watachukua majivu ya sadaka ya kuondoa dhambi iliyoteketezwa, majivu hayo yatachanganywa na maji ya mtoni katika chungu. Mtu aliye safi atachukua husopo, halafu ataichovya katika maji hayo, kisha atainyunyizia hema… pia mtu aliyegusa mfupa wa mtu, au mwili wa mtu aliyeuawa au aliyekufa kifo cha kawaida, au aliyegusa kaburi" (Hesabu 19: 17-18).

Taswira ya ndama mwekundu ni aina nyingine ya mfano wa dhabihu ya Kristo kwa dhambi ya waumini. Bwana Yesu alikuwa "hana dhambi," kama vile ndama mwekundu hakufaa kuwa nayo. Vile ndama alivyotolewa dhabihu "nje yah ema" (Hesabu 19:3), Yesu alisulubiwa nje ya Yerusalem (Waebrania 13:11-12). Na kama vile jivu la ndama mwekundu liliwatakaza watu kutokana na kuguza maiti, ndivyo dhabihu ya Kristo inatuokoa kutoka adhabu ya kifo na uharibifu.

Tambiko la ndama mwekundu lilianzishwa katika sheria ya Musa; katika kipindi hicho tangu wakati huo, Uyahudi umeongeza viwango vingi kwa yale ambayo hapo awali yalikuwa maagizo ya moja kwa moja, rahisi. Tamaduni ya Talimudi inazungumzia juu ya aina ya kamba ambayo ndama mwekundu angefungwa nayo, sehemu ilipaswa kuangalia wakati wa kuchinjwa, maneno yaliyosemwa na kuhani, kuvaa viatu wakati wa ibada, nk sheria za marabi ziliorodhesha vitu vingi ambavyo vinaweza kumzuia ndama nyekundu asitolewe dhabihu: ikiwa alikuwa amepandwa au kuegemewa, ikiwa alikuwa na vazi lililowekwa juu yake, ikiwa ndege alikuwa ametua juu yake, na ikiwa alikuwa na nywele mbili nyeusi au nyeupe, kati ya masharti mengine mengi.

Kwa mjibu wa tamaduni za kirabii, kumekuwa na ndama wekundu tisa kutolewa dhabihu tangu enzi za Musa. Tangu kuharibiwa kwa hekalu la pili, hamna ndama mwekundu amewai chinjwa. Mwalimu Maimonides kutoka mwaka wa (1135-1204) alifunza kwamba ndama mwekundu wa kumi atatolewa dhabihu na Masihi mwenyewe. Wale wanaonuia kujengwa kwa hekalu la tatu waka na hamu ya kumpata ndama mwekundu ambaye atatimiza masharti yote, kwa sababu ya jivu la ndama mwekundu litakuwa la manufaa katika kutaza hekalu jipya. Wengi huchukulia kuwa kuonekana kwa ndama mweusi atatangaza kujengwa kwa hekalu na kurudi kwa Kristo. Kulingana na taasisi ya Hekalu, kikundi ambacho kinapendekeza kujengwa kwa hekalu la tatu, ndama mwekundu asiye na mawaa alizaliwa mwezi wa Nane mwaka wa 2018 kule Israeli.

Kulingana na ratiba ya wakati ujao ya eskatolojia, kwa kweli kutakuwa na hekalu la tatu la Mungu huko Yerusalemu. Yesu alitabiri kuchafuliwa kwa hekalu wakati wa dhiki (Mathayo 24:15; taz. 2 Wathesalonike 2: 4); ili hilo litukie, ni dhahiri itabidi kuwe na hekalu huko Yerusalemu ili lichafuliwe. Kudhani kwamba wale wanaoweka wakfu hekalu la nyakati za mwisho wanafuata sheria ya Kiyahudi, watahitaji majivu ya ndama mwekundu, lililochanganywa na maji, kwa utakaso wa kitamaduni. Ikiwa ndama mwekundu asiye na mawaa amezaliwa kweli, inaweza kuonekana kana sehemu moja hakika imetendeka kwa ajili ya kusababisha utimilifu wa unabii wa kibiblia.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ndama mwekundu ni ishara ya nyakati za mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries