settings icon
share icon
Swali

Nani alihusika na kifo cha Yesu? Nani alimuua Yesu?

Jibu


Jibu kwa swali hili lina njia nyingi. Kwanza, hamna shaka, viongozi wa dini wa Israeli walihusika na kifo cha Yesu. Mathayo 26:3-4 inatuambia "Wakati huo makuhani wakuu na wazee wa watu walikutana pamoja katika ukumbi wa Kayafa, kuhani mkuu. Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue." Viongozi wa Kiyahudi walidai kwa nguvu kutoka kwa Warumi kuwa Yesu auwawe (Mathayo 27:22-25). Hawangeweza kumruhusu kuendele kutenda ishara na maajabu kwa sababu hiyo iliwatishia vyeo vyao na nafasi yao ya kidini katika jamii walioitawala (Yohana 11:47-50), kwa hivyo "walifanya mipango ya kumwua Yesu" (Yohana 11:53).

Warumi ndio waliomsulibisha (Mathayo 27:27-37). Kusulubiwa ilikuwa njia ya Kirumi ya kunyonga, iliyoidhinishwa na kutekelezwa na Warumi chini ya mamlaka ya Pointio Pilato, gavana wa Kirumi ambaye alimhukumu Yesu. Askari wa Kirumi waligongerea msumari kwa mikono yake na miguu, kikosi cha Kirumi kilisimamisha msalaba na askari wa Kirumi alimdunga mkuki upavuni mwake (Mathayo 27:27-35)

Watu wa Israeli pia waliridhika na kifo cha Yesu. Wao ndio wapasa sauti, "Asulubiwe! Asulubiwe!" aliposimama mbele ya Pilato (Luka 23:21). Pia waliomba mwizi Baraba afunguliwe badala ya Yesu (Mathayo 27:21). Petro anadhibitisha hili katika Matendo 2:22-23 wakati aliwaambia wanaume wa Israeli, "nanyi mkamuua kwa kuwaachia watu wabaya wamsulubishe." Hakika kuuwawa kwake Yesu ilikuwa ni njama iliyowahuzisha Rumi, Herode, na viongozi wa Kiyahudi na watu wa Israeli, makundi tofauti ambayo hayakuwai fanya kazi pamoja tangu mwanzo, lakini wakaja pamoja wakati huu mmoja kufanya njama na kutekeleza lile lisilofikirika: mauaji ya Mwana wa Mungu.

Mwoshowe, na pengine kiajabu, ilikuw ni Mungu aliyemfanya Yesu kufa. Hili lilikuwa tendo la juu sana la haki ya kiungu liliwai fanyika "Kufuatana na mpango wake mwenyewe Mungu" (Matendo 2:23) na kwa kusudi kuu. Kifo cha Yesu msalabani kulituhifadhia wokovu mara milioni isiyohesabika na kupeana njia pekee ambayo Mungu angeweza kusamehe dhambi bila kuaibisha utakatifu Wake na haki Yake kamilifu. Kifo cha Yesu ulikuwa mpango kamilifu wa Mungu wa ukombozi wa milele wa walio wake. Mbali na kuwa ushindi kwa Shetani, vile wengine wamekisia, au mkasa usiostahili, lilikuwa tendo kuu la neema ya wema na huruma ya Mungu, dhihirisho la juu la upendo wa Baba kwa wenye dhambi. Mungu alimfanya Yesu afe kwa sababu ya dhambi zetu ili tuweze kuishi bila dhambi na haki mbele zake, haki iwezekanayo pekee kupitia kwa msalaba. "Kristo hakuwa na dhambi, lakini Mungu alimfanya ahusike na dhambi kwa ajili yetu, ili sisi kwa kuungana naye, tupate kuushiriki uadilifu wake Mungu" (2 Wakorintho 5:21).

Kwa hivyo sisi ambao tumekuja kwa Kristo kwa imani tuna hatia ya damu yake iliyomwagika msalabani kwa ajili yetu. Alikufa ili alipe adhabu ya dhambi zetu (Warumi 5:8; 6:23).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nani alihusika na kifo cha Yesu? Nani alimuua Yesu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries