settings icon
share icon
Swali

Ni nani aliyeandika Biblia?

Jibu


Ni sahihi kusema kwamba Mungu aliandika Biblia. Kulingana na 2 Timotheo 3:16, Maandiko "yana pumzi ya" Mungu. Katika Biblia, ni dhahiri kwamba Mungu ananukuliwa: zaidi ya mara 400 katika Biblia, tunaona maneno, "Bwana asema hivi." Biblia inajiita Neno la Mungu mara nyingi (kwa mfano; Zaburi 119; Methali 30:5; Isaya 40:8; 55:11; Yeremia 23:29; Yohana 17:17; Warumi 10:17; Waefeso 6:17; Waebrania 4:12). Biblia inasemekana inatoka kinywani mwa Mungu (Kumbukumbu la Torati 8:3; Mathayo 4:4).

Walakini kusema kwamba Mungu aliandika Biblia haimaanishi kwamba alichukua kalamu mkononi, akachukua ngozi na kuandika maandishi ya Maandiko. "Uandishi" wake wa Biblia haukua kitendo halisi. Badala yake, uandishi wa Mungu ulikamilishwa kupitia mchakato wa ushauri, binadamu walipokuwa wanaandika ujumbe wa Mungu.

Kwa hivyo, ni sahihi kusema kwamba watu wa Mungu walioongozwa na Roho waliandika Biblia. Mafundisho ya upuzio wa maandiko kimsingi yanafundisha kwamba Mungu "aliwasimamia" waandishi wa kibinadamu wa Biblia ili mitindo yao ya kibinafsi ihifadhiwe lakini matokeo ya mwisho ndio haswa yale Mungu alitaka. Kwa mfano, wakati Mathayo aliketi na kuandika hadithi ya huduma ya yesu, alitegemea ufahamu wake (yeye alikuwa shahidi wa matukio aliyosimulia) akisaidiwa na Roho Mtakatifu (Yohana 14:26), na kutilia maanani wasomaji waliokusudiwa (Mathayo aliandika kwa ajili ya wasomaji Wayahudi). Matokeo yake yakawa ni Injili ya Mathayo- hadithi iliyojaa msamiati wa Mathayo, sarufi ya Mathayo, sintaksia ya Mathayo, na mtindo wa Mathayo. Hata hivyo, lilikuwa Neno la Mungu. Roho aliongoza uandishi wa Mathayo kwamba kila kitu Mungu alitaka kusema kilisemwa, na hakuna kilichojumuishwa ambacho Mungu hakukusudia kusema.

Petro alielezea mchakato wa upuzio hivi: "Ingawa manabii ni wanadamu, walinena kutoka kwa Mungu walipokuwa wanaongozwa na Roho Mtakatifu" (2 Petro 1:21). Nabii Yeremia alizungumza juu ya upuzio kana kwamba ni kulazimika kuandika ujumbe wa Mungu: "Moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia" (Yeremia 20:9). Haikuwezekana kuepuka; Mungu alitaka kuwasiliana, kwa hivyo Yeremia alilazimika kuandika.

Sio kila kitabu cha Biblia ambacho hutaja ni nani aliyekiandika. Kwa mfano, mwandishi wa kitabu cha Waebrania hajulikani. Hakuna njia ya hakika ya kujua waandishi wa kibinadamu wa vitabu vyingi vya Biblia. Lakini hio haibadilishi tunachojua kwa hakika, yaani mwandishi wa Kimungu wa Biblia.

Katika historia, waandishi mashuuri walitumia karani au makatibu kutoa fasihi zao. Mshairi John Milton alikuwa kipofu alipokuwa na umri wa 44. Fasihi yake inayojulikana kama Paradise Lost ilisomewa marafiki na jamaa -yeyote ambaye angemwandikia-na hivyo ndivyo hadithi yake ilirekodiwa (jumla ya mistari 10,550 ya mashairi). Ingawa Milton mwenyewe hakufanya uandishi huo, hakuna anayeshuku kwamba fasihi ya Paradise Lost ilikuwa kazi yake. Tunaelewa kazi ya makarani. Ingawa Mungu hakuandikisha Neno lake kwa waandishi wa kibinadamu, kanuni iliyotumika ni sawa. Mungu, ambaye ndiye Mwandishi wa Biblia aliwatumia wanadamu kama "makarani" na matokeo yake yakawa ni Neno lililotiwa pumzi na Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nani aliyeandika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries