settings icon
share icon
Swali

Nadharia ya Kuzimia ni nini? Je! Yesu aliponea kusulubiwa?

Jibu


Nadharia ya Kuzimia ni imani kwamba Yesu kwa hakika hakufa wakati wa kusulubiwa kwake lakini alikuwa amepoteza ufahamu tu wakati alilazwa kaburini na huko alirudisha fahamu. Kwa kadiri, kijitokeza Kwake baada ya siku tatu katika kaburi ulikuwa tu umeonekana kuwa maonyesho ya ufufuo. Kuna sababu kadhaa kwa nini nadharia hii ni batili na inaweza kuthibitishwa kwa urahisi kuwa ya uongo, na kulikuwa na angalau watu watatu tofauti au makundi yaliyohusika katika kusulubiwa kwa Yesu ambao wote waliridhika kuhusu ukweli wa kifo Chake msalabani. Wao ni walinzi wa Kirumi, Pilato, na Wakuu wa Makuhani.

Walinzi wa Kirumi — Kulikuwa na makundi mawili tofauti ya askari wa Kirumi waliopewa kazi ya kuhakikisha kifo cha Yesu: wauaji na walinzi wa kaburi. Askari waliohusika na utekelezaji walikuwa wataalamu katika adhabu ya kifo, na kusulubiwa ilikuwa aina moja ya ukatili zaidi ya utekelezaji katika historia. Yesu alipigiliwa misumari kwa msalaba baada ya kustahamili kupigo cha kutisha kwa mikono ya wataalamu hawa mashabiki wa kifo, na kila mtu aliyeuawa kwa njia ya kusulubiwa alikuwa anashughulikiwa na askari hawa. Kazi yao ilikuwa kuhakikisha kazi ilikuwa imekamilika. Yesu hangeweza kuponea kusulubiwa, na askari hawa walihakikisha kwamba Yesu alikuwa amekufa kabla mwili Wake kuruhusiwe kuchukuliwa kutoka msalabani. Waliridhika kabisa kwamba Yesu alikuwa amekufa kweli. Kikundi cha pili cha askari kilipewa kazi ya kulinda kaburi la Yesu kwa sababu ya ombi lililofanyika kwa Pilato na Sanhedrini. Mathayo 27:62-66 inatuambia, "Hata siku ya pili, ndivyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato, wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa angali hai, "Baada ya siku tatu nitafufuka." Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza. Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo. Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi." Walinzi hawa walihakikisha kwamba kaburi liko salama, na maisha yao yanategemea kukamilika kwa misheni yao. Ufufuo wa Mwana wa Mungu tu ungewatoa kutoka kwa kazi yao.

Pilato — Pilato alitoa amri ya Yesu kusulubiwa na akakabidhi kazi hii kutekelezwa na mkuu wa jeshi la Kirumi, kamanda aliyeaminika na kuthibitishwa wa askari 100 wa Kirumi. Baada ya kusulubiwa, ombi la mwili wa Yesu lilifanywa na Yusufu wa Arimathaya, ili mwili wake uweze kuwekwa kaburini. Kisha baada ya mkuu wa jeshi kuthibitisha kifo cha Yesu Pilato aliacha mwili chini ya utunzaji wa Yusufu. Marko 15: 42-45: "Hata ikiisha kuwa jioni, kwa sababu ni Maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya sabato, akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza ya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu. Lakini Pilato akastaajabu, kwamba amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo. Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule akida, alimpa Yusufu yule maiti." Pilato alikuwa ameridhika kabisa kwamba Yesu alikuwa amekufa kwa kweli.

Wakuu wa Makuhani – Wakuu wa Makuhani lilikuwa baraza la utawala la Wayahudi, na waliomba kwamba miili ya wale waliosulubiwa, ikiwa ni pamoja na Yesu, ichukuliwe msalabani baada ya kifo chao kwa sababu ya siku ya Sabato iliyofuata. Yohana 19:31-37: "Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae misalabani siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulubiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli ili ninyi nanyi mpate kusadiki. Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena andiko linguine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma." Wayahudi hawa ambao walitaka Yesu kusulubiwe, hata kwenda Zaidi kupendekeza upinzani ikiwa angesulubiwa, kamwe hawangeruhusu mwili wa Yesu kuondolewa msalabani ikiwa hakuwa amekufa. Wanaume hawa walikuwa wameridhika kabisa kwamba Yesu alikuwa amekufa kweli.

Kuna ushahidi mwingine kwamba Nadharia ya Kuzimia ni batili, kama vile hali ya mwili wa Yesu baada ya ufufuo. Katika kila muonekano, mwili wa Yesu ulionyeshwa kuwa katika hali ya utukufu, na alama pekee iliyobaki kama ushahidi wa kusulubiwa Kwake ni alama ya misumari aliyomuuliza Tomaso kugusa kama ushahidi wa yule Yeye alikuwa. Mtu yeyote alipitia kile Yesu alipitia angehitaji miezi kupona kimwili. Mwili wa Yesu ulikuwa na alama tu za misumari katika mikono na miguu Yake. Njia ambayo mwili wa Yesu uliandaliwa baada ya kusulubiwa ni ushahidi zaidi wa kukataa nadharia. Ikiwa Yesu alikuwa amepoteza ufahamu tu, kitani ambacho alikuwa amefungiwa ndani haingewezekan kwa Yeye kuepa kutoka, ikiwa alikuwa tu mtu. Njia ambayo wanawake walihudumia mwili wa Yesu ni ushahidi zaidi wa kifo chake. Walikuja kaburini siku ya kwanza ya juma ili kupaka mafuta mwili wake zaidi na kutia dawa ya lihamu kwa kuwa walikuwa na muda mchache wa kuandaa mwili wake kabla ya kuanza kwa Sabato. Ikiwa Yesu alikuwa amezimia tu kama nadharia inavyodai, wanawake wangeweza kuleta zana za matibabu ili kusaidia katika ufufuo Wake.

Madhumuni ya Nadharia ya Kuzimia sio kupinga kifo cha Yesu, lakini badala yake, inatafuta kupinga ufufuo Wake. Ikiwa Yesu hakufufuka, basi Yeye si Mungu. Ikiwa Yesu alikufa kweli na kufufuka kutoka kwa wafu, nguvu Yake juu ya kifo inathibitisha kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu. Ushahidi unahitaji uamuzi: Yesu kweli alikufa msalabani, na Yesu kweli alifufuka kutoka kwa wafu.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nadharia ya Kuzimia ni nini? Je! Yesu aliponea kusulubiwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries