settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nani mzuizi katika 2 Wathesalonike 2:6?

Jibu


Wanafunzi wa unabii wa kibiblia wana mitazamo tofauti juu ya utambulisho wa mzuizi katika 2 Wathesalonike 2:6-7. Yeyote yule huyu mzuizi yuko, yeye ni mtu aliye na nguvu zaidi ambaye anazuilia kuendelea kwa Mpinga Kristo na kuzuia ufalme wa kishetani kutoka na kukandamiza ulimwengu.

Katika nyaraka yake ya pili kwa Wathesalonike, Paulo alilihakikishia kanisa kwamba walikuwa bado hawakuwa wanaishi nyakati za Siku ya Bwana, ambayo kwamba hukumu ya nyakati za mwisho haikuwa bado imeanza. Katika 2 Wathesalonike 2: 3 anasema, "Mtu yeyote na asiwadanganye kwa namna yoyote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza, na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa." Kulingana na ratiba ya Mungu, Siku ya Bwana na hukumu inayoambatana nayo haitaanza mpaka mambo mawili yatokee: uasi wa kiulimwengu unatokea na Mpinga Kristo anafunuliwa. Halafu Paulo anataja kile kinachozuia uovu kwa sasa: "Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake" (2 Wathesalonike 2: 6-8).

Paulo hataji moja kwa katika kumtambua huyu mzuizi ni nani, kwa kuwa Wathesalonike walikuwa wanamjua. Wasomi wengi wa Biblia hukisia utambulisho wa huyu mzuizi, huku wakimwita huyu mzuizi nguvu kama vile 1) serikali ya Kirumi; 2) kuhubiri injili; 3) kufungwa kwake Shetani; 4) majaliwa yake Mungu; 5) taifa la Kiyahudi; 6) kanisa; 7) Roho Mtakatifu; na 8) Mikaeli malaika mkuu. Tunaamini kuwa mzuizi sio mwingine isipokuwa Roho Mtakatifu, au tunaweza kusema kuwa ni Roho Mtakatifu anayefanya kazi kupitia kanisa la Agano Jipya.

Kuunga dhana kuwa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa ndie mzuizi ni hoja kwamba mzuizi anarejelewa kuwa kitu (kisicho na jinsia, aya ya 6) na kama mtu wa (jinsia ya kiume, aya ya 7). Pia, nguvu inayochelewesha mpango wa Shetani wa kujifunua kama masihi wa uwongo lazima iwe ni Mungu. Itakuwa ni busara zaidi kusema kwamba Roho Mtakatifu anamzuia Ibilisi kuliko taasisi ya kisiasa au hata malaika. Roho Mtakatifu wa Mungu ndiye Mtu pekee aliye na nguvu ya kutosha (isiyo ya kawaida) kufanya uzuiaji huu.

Kwa kweli, Roho hufanya kazi kupitia waumini kutimiza haya. Kanisa, lililojazw na Roho wa Mungu, daima limekuwa sehemu ya kile kinachozuia jamii kutokana na ongezeko la kuishi bila sheria. Wakati mwingine, Paulo anasema, Roho "ataacha" kiasi kufanya kazi Yake ya kuzuia, akiruhusu dhambi itawale wanadamu. Wathesalonike wa Pili 2: 7 inaweza kutafsiriwa kihalisi, "Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa." Tunaamini hili "kutoweka kutoka katikati" itatokea wakati kanisa linaondoka duniani wakati wa unyakuo. Roho Mtakatifu bado atakuwepo duniani, kwa kweli, lakini ataondolewa mbali kwa maana kwamba hatakuwa akitimiza huduma yake ya kipekee ya kuzuia dhambi-kupitia kwa watu wa Mungu-ataondolewa (ona Mwanzo 6: 3).

Wathesalonike wa Pili mlango wa 2 uu wazi kuwa kuondolewa kwa ushawishi wa mzuiaji unafuata kufunuliwa kwa Mpinga Kristo. Akipewa uhuru wa kutawala wakati wa dhiki, mtu mwasi ambaye "hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo" kuwadanganya watu duniani (2 Wathesalonike 2:9-10). Baada ya wakati wa Mpinga Kristo umeisha, Bwana Yesu atarudi na kumwondoa mtu wa dhambi kwa "atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake" (2 Wathesalonike 2:8). Dhambi imezuiliwa kwa sasa; kipindi cha kanisa kimeisha, kuzuiliwa kwa uovu kutaondolewa na mwasi ataonekana kushinda; walakini, kuna uhakikisho kuwa mwisho dhambi itaangamizwa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nani mzuizi katika 2 Wathesalonike 2:6?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries