settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kuwa mwanamke wa Mungu?

Jibu


Mwanamke wa Mungu kwanza ni binti wa Mungu. Kuwa mtoto wa Mungu hufanyika kupitia uhusiano wa kuokolewa na Yesu Kristo (Yohana 1:12; 3: 16-18, 36). Tunapomtegemea Yesu kwa ajili ya wokovu, tunakuwa viumbe wapya (2 Wakorintho 5:17). Mungu anatupa Roho Wake Mtakatifu anayefanya kazi ndani yetu na kutubadilisha kuwa zaidi kama Kristo (Yohana 14: 15-17, 1 Yohana 4:13, 2 Wakorintho 3:18). Kwa kuongezea tu, mwanamke wa Mungu ni mwanamke ambaye ameokolewa na Yesu Kristo na ambaye ananyenyekea kwa kazi ya Roho Mtakatifu aliye ndani yake. Je! Hii inaonekana vipi kwa vitendo?

Mwanamke wa Mungu atatafuta kumjua Mungu zaidi kwa kusoma Neno Lake, akizungumza naye katika sala, kushirikiana na waumini wengine, na kusikiliza mafundisho mazuri. Anajua kwamba Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema" (2 Timotheo 3: 16-17), hivyo yeye anataka kujua vile Neno la Mungu linavyosema. Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. (2 Timotheo 2:15). Pia anasikiliza onyo la Yakobo: "Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. " (Yakobo 1:22).

Yeye hufanya kile Neno linavyosema kwa kuwa na maisha ya maombi. Paulo anatueleza, "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu" (Wafilipi 4: 6-7). Vivyo hivyo, 1 Wathesalonike 5: 16-18 inasema, "Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. " Mwanamke wa Mungu humkaribia Mungu kwa moyo wenye shukrani na kutoa wasiwasi kwake Mungu (1 Petro 5: 7). Anategemea uwezo wa Mungu na upendo wake, na hivyo hupeana ibada yake na wasiwasi wake kwenye kiti chake cha enzi (Waebrania 4: 14-16).

Mwanamke wa Mungu anatii amri za Mungu kupenda wengine vizuri. Maneno yake ni ya kujenga na kuwahimiza wengine, sio kuwadharau au kujazwa na uvumi au nia mbaya (Waefeso 4:29, 1 Petro 2: 1-3). Yeye ni mwenye fadhili, mwenye huruma, mwenye kusamehe (Waefeso 4:32). Anasaidia kubeba mizigo ya waumini wengine (Wagalatia 6: 2; Warumi 12:15). Akipata fursa, yeye anajaribu kuwatenda mema wote, hasa wale walio katika familia ya Mungu (Wagalatia 6:10). Yeye hajisifu lakini anaishi na roho ya unyenyekevu (Warumi 12:10, 16; Wafilipi 2: 5-11). Yeye hanung'uniki au kusababisha ugomvi, lakini badala yake anajaribu kuishi na umoja na wengine (Warumi 12:16, 18; Wafilipi 2:14).

Mwanamke wa Mungu anafuata mafundisho ya Petro kwa "mioyoni mwenu mheshimu Kristo kama Bwana, Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. "(1 Petro 3: 15-16). Anajaribu "kujiepusha na tamaa za mwili zipiganazo na roho. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa." ( 1 Petro 2: 11-12).

Mwanamke wa Mungu hufanya kazi kwa bidii ambayo Mungu amempa (Warumi 12:11). Ikiwa yeye ni mwanamke mzee, yeye huwa mfano kwa wanawake wadogo (Tito 2: 3-5). Anatumia muda na waumini wengine, kuwahimiza na kuhimizwa nao (Waebrania 10: 24-25). Ananyenyekea, kumaanisha anawapa wengine nafasi ya kwanza, kama vile Wakristo wanaagizwa kufanya.

(Waefeso 5:21). Anasikiliza amri ya Petro ya "Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema. Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu. Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme."

(1 Petro 2: 13-17). Anajua kwamba ana thamani sana katika Kristo (Wagalatia 3:28) na anachagua kumwiga kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake. Ikiwa ameolewa, anaruhusu mumewe kuongoza familia (Waefeso 5: 21-33; 1 Petro 3: 1-2). Anawaheshimu wazazi wake (Waefeso 6: 1-3), na, ikiwa ana watoto, anawajali (Tito 2: 3-5; 1 Timotheo 5:14). Anasimamia nyumba yake vizuri na kulingana na kanuni za kimungu (Tito 2: 3-5; Mithali 14: 1; 31).

Mwanamke wa Mungu ana utu wa moyoni "yaani utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu." (1 Petro 3: 3-4). Hatimaye, mwanamke wa Mungu ni kazi inayoendelea, kiumbe cha Mungu, aliyeokolewa na neema yake kupitia imani (Waefeso 2: 8-10), na kuwa zaidi kama Yesu huku akijisghulisha na kumjua na kumtii Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kuwa mwanamke wa Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries