settings icon
share icon
Swali

Ni kitu gani Mkristo mzazi anastahili kufanya kama wako na mwana mpotevu (au binti)? Njia?

Jibu


Kunao uasili katika hadhiti ya mwana mpotove (Luka 15:11-32) kanuni nyingi ambazo mzazi Mkristo anaweza kutumia kwa hali ambayo watoto wake wanatembea kinyume na njia ambazo wamelea nazo. Wazazi wanastahili kukumbuka kwamba pindi tu watoto wao wanapofika umri wa utu uzima, hawako tena chini ya mamlaka ya wazazi.

Katika hadhiti ya mwana mpotevu, yule kijana mdogo anauchukua urithi wake na kusafiri nchi ya mbali na anaharibu mali yake. Katika kesi ya mtoto ambaye hajaokoka, hili ni tendo ambalo linakuja bila kupenda. Kwa kesi cha mtoto ambaye wakati mmoja alikiri imani yake katika Kristo, tunamwita mtoto huyu “mwana mpotevu.” Maana ya neno hili ni “mtu ambaye amayatumia mali yake vibaya,” elezo zuri la mwana anayetoroka nyumbani na kuupoteza urithi wa kiroho ambao wazazi wake wamemwekea akiba. Miaka yote ya ulezi, mafunzo, upendo, na ulinzi imesaahulika na mtoto huyu anaasi kinyume na Mungu. Kwanza uasi wote ni kinyume na Mungu na unajidhihirisha katika uhasi kinyume na wazazi na mamlaka yao.

Kumbuka kwamba baba mzazi katika mfano hamkomeshi mtoto wake kutoraka nyumba. Vilevile hamfuati nyuma kujaribu kumkinga. Bali huyu mzazi kwa uaminifu anakaa nyumbani na kuomba, na wakati huyo mtoto “amerudi katika hali yake ya mawazo” na kugeuka na kurudi nyumbani, mzazi anakesha na kungoja na anakimbia kumkumbatia mwanawe bado “akiwa mbali.”

Wakati mwana na binti wanapoifuata njia yao-wakidhani kuwa ni ya haki yao katika kisasi hiki kufanya hivyo- na kufanya maamuzi ambayo tunayajua yatawaletea madhara, wazazi lazima wawaruhusu kuendelea. Mzazi hamfuati baadaye, na vilevile mzazi haingilii katika madhara yake. Bali, mzazi anakaa nyumbani, na kuendelea kuomba kwa imani na kungoja kwa ishara ya kutubu na ugeuzo wa mwelekeo. Hadi hayo yafike, mzazi wanaendele na ushauri wao, hawaungu uasi mkono na haingilii (1 Petero 4:15).

Pindi tu watoto wamefika umri wa utu uzima, wako chini ya mamlaka ya Mungu na mamlaka ya serikali (Warumi 13:1-7). Kama wazazi, tunaweza wapa msaada watoto wetu wapotevu kwa upendo na maombi na tuwe tayari kuja karibu nao pindi tu wanapofanya uamuzi wao kumrudia Mungu. Mungu kila mara hutumia magumu ambayo tunayojitakia kutuleta katika hekima, ni jukumu la kila mtu kutii inavyostahili. Kama wazazi, hatuwezi waokoa watoto wetu- ni Mungu pekee anaweza kufanya hivyo. Mbaka muda huo uje, lazima tukeshe, tuombe na kumwachia mambo hayo Mungu. Hii inaweza kuwa wakati wa uchungu, lakini wakati linapochukuliwa Kibilia, litaleta amani ya akili na moyo. Hatuwezi wahukumu watoto wetu, ni Mungu pekee anayeweza kufanya hivyo. Kwa haya kuna faraja kubwa: “Mhukumu ulimwengu wote asiende haki?” (Mwanzo 18:25b).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kitu gani Mkristo mzazi anastahili kufanya kama wako na mwana mpotevu (au binti)? Njia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries