settings icon
share icon
Swali

Wana wa Mungu na binti za wanadamu ni nani katika Mwanzo 6:1-4?

Jibu


Mwanzo 6:1-4 inaelezea wana wa Mungu na binti za wanadamu. Kumekuwa na mapendekezo mengi kuwa ni nani hawa wana wa Mungu na ni kwa nini watoto waliozaa na binti za wanadamu walikua na kuwa kizazi cha majitu (hili ndilo neno Nephilim laoneka kuashiria)

Mitazamo mitatu ya kimsingi yatambua wana wa Mungu kama 1) walikuwa malaika walionguka, 2) ni viongozi wa wanadamu walio na mamlaka, au 3) walikuwa kizazi cha Mungu cha Sethi walio oana na kizazi kidhaifu cha Kaini. Kuupa uzito mtazamo wa kwanza ni hoja kwamba katika Agano la Kale mstari “wana wa Mungu” kila mara wamaanisha malaika (Ayubu 1:6; 2:1; 38:7). Kasoro iliyo kwa sababu ya haya katika Mathayo 22:30 ambayo yaonyesha kuwa malaika hawaoi. Bibilia haitupi sababu yoyote ya kuamini kwamba malaika wako na lengo au wako na uwezo wa kuzaa. Mitazamo mingine miwili haileti shida hii.

Udhaifu wa mtazamo wa 2) na 3) ni kwamba, mwanadamu wa kiume wa kawaida anamuoa mwanamke wa kike wa kawaida haifafanui ni kwa nini uzao ulikuwa wa “majitu” au “mashujaa wa kale, wa wanadamu wanaojulikana.” Zaidi, ni kwa nini Mungu aliamua kuleta ghalika duniani (Mwanzo 6:5-7) wakati Mungu hakuwa amewakataza wana wa kiume wa wanadamu au kizazi cha Seth kuoa wanawake wa kawaida au uzao wa Kaini? Hukumu ijayo ya Mwanzo 6:5-7 imehuzishwa na chenye kilitokea Mwanzo 6:1-4. Ni ndoa isiyo halali ya malaika na binti za wanadamu ionekanayo kuthibitisha hukumu hii kali.

Vile imekwisha nakiliwa udhaifu wa mtazamo wa kwanza ni kwamba Mathayo 22:30 yasema, “Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.” Ingawa ujumbe huu hausemi kuwa “malaika hawana uwezo wa kuoa.” Bali wasema kuwa malaika hawaoi. Pili, Mathayo 22;30 yaashiria “malaika mbinguni.” Haiashirii malaika walioangukua, wenye hawajali juu ya mpangilio wa Mungu wa uumbaji na kwa bidii yao wakitafuta kuharibu mpango wa Mungu. Hoja kwamba malaika watakatifu wa Mungu hawaoi au kuwa na tendo la ndoa haimanishi kuwa hiyo nayo ni sawa kwa Shetani na mapepo wake.

Mtazamo 1) ni msimamo unaokubaliwa. Naam, ni jambo la kufurahisha “utatanisho” kusema kwamba malaika hawafanyi nkono na kusema kwamba “wana wa Mungu” walikuwa malaika ambao walizaa na binti za wanadamu. Ingawa malaika ni viumbe wa kiroho (Waebrania 1:14), wanaweza kuwa katika umbo la mwili (Mariko 16:5). Wanaume wa Sodomu na Gomora walitaka kuonana kwa mwili na malaika wawili wenye walikua na Loti (Mwanzo 19:1-5). Inawezekana malaika wanaweza kujukua mwili, kiwango wanaweza kufanya mapenzi na mwanadamu na kuzaa. Ni kwa nini hawa malaika walioanguka kufanya hivi kila mara? Ni uwezekano kuwa Mungu aliwapeleka mateka hawa malaika walioanguka waliofanya dhambi, ili malaika wengine wameanguka wasirudie (vile imeelezwa katika Yuda 6). Wafafanusi wa kwanza wa Kiibrania na unabii wa mafumbo na uandishi wa jumla wote wako pamoja wakishikilia mtazamo kuwa, malaika walioanguka walikuwa “wana wa Mungu” vile imetajwa katika Mwanzo 6:1-4. Hili kwa vyovyote vile linafunga mjadala. Bali mtazamo kuwa Mwanzo 6:1-4 wahuzisha malaika walioanguka wakifanya tendo la ndoa na binti za wanadamu liko na msingi wa kidondoo, lugha, na historia.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wana wa Mungu na binti za wanadamu ni nani katika Mwanzo 6:1-4?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries